Vichekesho Vya Kukuchekesha
Misemo ya kina dada
Misemo ya kina dada
walianza na halohalooo!
Wakaja unalo babu weee!
Ikafuata utajijuuu!
Ikafupishwa utajiJJ!
Mara ghafla kantangazeee!
Haikukaa sana kansajiriii!
Ikatoka nyingine nishiiiiida!
Unaijua iliyotoka Leo?
Heh! Heh! Heeeh! MB zenyewe 8 nikudownload unanini?
Wavuta bangi wa Colombia watoa mpya
Asubuhi ya leo huko nchini Colombia baada ya serikali kuidhinisha matumizi ya bangi kuwa halali +++ Wavutaji bangi wamepanda basi la gorofa wengine juu wengine chiniโฆ.
Waliopanda chini wanawauliza wa juu huko speed ni ngapi maana huku ni 80.
Wajuu wakajibu huku mpaka sasa hatujui dereva bado hajajaโฆ. ๐๐๐
Sababu ya mke kupewa dawa badala ya mumewe
Dokta: Mama tumemchunguza mumeo kwa makini sana, jopo lote la madaktari tumekubaliana mumeo anahitaji mapumziko japo ya mwezi. Sasa tafadhali chukua hivi vidonge vya usingizi vitasaidia sana.
Mama: Asanteni sana, sasa niwe nampa mara ngapi?
Dokta: Unatakiwa wewe uwe unakunywa vidonge hivi kutwa mara tatu kwa mwezi mzima, mumeo atapona.
Kilichompata sista duu bishoo wakati akijidai kununua pete
Mwanamke mmoja aliingia duka la vito vya thamani, akaona pete moja ya dhahabu nzuri sana amabayo ilikuwa kwenye shelf ya chini, wakati anainama apate kuitazama vizuri kwa bahati mbaya (au nzuri!), shuzi likamtoka- druuuuuu, soni ikamuingia huku akigeuka haraka kuangalia kama kuna yeyote dukani pale ameliskia shuzi lake, macho yakagongana na mwenye duka ambaye alikuwa karibu huku uso ukiwa umejaa tabasamu zito, mwana mama hakuwa na uhakika kama amesikika au hakusikika, akaona atumie nafasi ile kuyeyushaโฆAkauliza “Hii pete bei gani?” . Jamaa mwenye duka, huku akiangua kicheko, akajibu “Umeiona tu umejamba, je nikikuambia bei yake si utakunya kabisa?”
Hii bahati mbaya hii haifai kusema Samahani
(KIFO NI NIN)
KIFO ni pale unapokosea text na kumtumia
BABA yako kipindi mnakula
“hello Mrembo”๐๐
Kama utazubutu kusema Samahani ๐
Hii dunia ina mambo, cheki kilichotokea wakati mme anakata roho akiwa na mke wake
Bwana mmoja wakati anakata roho alimwambia mkewe hivi:
MUME – mke wangu natubu mbele yako kwamba nimezini na mama yako, dada yako, shangazi yako, mama yako mdogo na mtoto wa shangazi yako.
MKE – nayafahamu yote hayo ndio maana nimekupa sumu.
Biashara ambayo imefeli
*TEACHER*: _nielezee biashara ambayo imefeli kutokana na uzembe
*STUDENT*: Changudoa akipata mimbaโฆ
*TEACHER*: _get Out!!!!!!!!!!!!!!_
๐๐
Simu ilivyozua utata
Mama alichukuwa simu akampa mwanawe. Mama..Mpigie babako mwambie chakula tayari. (Mtoto akachukuwa na kupiga) MtotoโฆMama simu ya baba imepokelewa na mwanamke. (Mama kwa hasira) Akirud atanitambua leo. (Baada ya muda kidogo baba akarud,kufika mlangon tu kapokewa na sufuria ya kichwa. Hajakaa vzur mwiko wa pua) Mama..Mwanangu ulipopiga simu ya babako mwanamke wake alisemaje?? Mtoto..Alisema mteja unaempigia hapatikan kwa sasaโฆ..
Angalia nilichomfanyia huyu dereva sasa
Tulikua kwa basi tunaelekea arusha,ile namcheki dereva kumbe ni best yangu na basi ilikua kwenye spidi hatari, nikaenda kumziba macho nkamuulizaย otea mi ni nani, kabla hajanijibu nikasikia kishindo kikubwa sana
NA SASA HIVI NIMEZINDUKA NIMEONA ABIRIA WOTE TUPO WODI NAMBA 3 HAPA KCMC MOSHI. ๐ค๐ค๐ค๐ค
SODA ZA WAGONJWA PLIIIZ!!! ๐๐๐๐๐
Duh! Wanaume jamaniโฆ
Lakini sisi wanaume hatuko fair โฆ Yani demu anang’ng’ana kujipodoa uso na sisi tunaangalia matako. ๐๐๐mungu anatuona jaman๐๐๐๐๐๐Makeup ya matako iletwe
Cheki huyu jamaa anachomfanyia huyu mrembo kanisani
Jamaa kaenda kanisani akakaa karibu na mrembo.
Wakati mahubiri yakiendlea jamaa akaanza kuingiza vocal:
Jamaa: dada mi nakupenda saana
Dem: Kaka naomba umsikilize mchungaji
Jamaa: nipe nafasi uwe msimamizi wa serikali ya moyo wanguโฆ
Dem: niacheโฆ
Jamaa: kweli nakupenda mpnz
Dem: (kwa sauti kubwa) nmesema NIACHEEEE!!
Watu wote kanisani wakageukaโฆ Jamaa kaona noma na ili atulize msala
Jamaa: sikuachi hadi ukiri YESU kuwa Bwana na mwokozi wa Maisha yako.
Huyu Baba ni noma, Cheki anachomjibu huyu mtoto wake
Mtoto:ย baba eti Botwasna ipo wap?
Baba:ย angalia itakuwa humo humo kabatini maana mama yako nae kwa kuficha kuficha vitu hajamboโฆ
Hakuna siku mbaya maishani kama hii
Hakuna siku mbaya maishan kuona mtu uliyesoma naye darasa moja, anakupita na private car,, afu we umeninginia kwenye daladala,,, tena ulikua unamzid akili ๐๐๐hapo Ndo utajua kwann gunia na dunia vinatofautiana neno moja
Cha kufanya mpenzi wako akikuacha
Kumkomoaโฆ
MPENZI WAKO AKIKUACHA BILA SABABU CHUKUA SIMU MPIGIE MAMA AKE MWAMBIE MWANAO AMEKUFA UWEZIโฆ. KULIA PEKE YAKO๐ค
Kama simu yako ina wifi
Kama simu yako ina Wi-fi ujue uko na mke wa mtuย ๐๐๐๐๐๐๐๐ผ๐๐ผ๐๐ผ๐๐ผ๐๐ผ
Angalia nilichokifanya baada ya kuumwa na meno
Baada ya kuumwa na Meno nikaamua hivi.
mimi sipeรฑdagi ujinga,,,Nmeumwa na jino moja la chini..nimeng’oa meno yote ya chini ili iwe funzo kwa meno ya juu๐ก๐ก
Huyu jamaa amekomeshwa, majambazi ni shida!
CHEKA KIDOGO
Majambaz waliliteka gar moja lililokua limeshehen abiria
Baada ya abiria kusachiwa na majambaz hao na kukutwa hawana pesa, majambaz wakasema kila m2 atapigwa viboko (bakora) kutokana na namba ya shati alilovaa
Aliyekua hana namba atasalimika
Kaz ikaanza, jamaa alievaa jez ya ROONEY wa Man U akapigwa fimbo 10, mwengine alievaa nguo ya 50cent akapigwa 50, n.k, sasa kwa pemben kulikua na jamaa analia sn yaani kila akijiangalia, kumbe alikua amevaa fulana limeandikwa LOWASA 2015 duuuh! Unajua kilichotokea ngoja niweke cm chaji kwanza.
Mimi ndio nimeelewa hivi!
Leo nimepishana na Vitz imeandikwa, “Never trust women”
Nikajua huyu mtu lazima alikuaga na Range Rover
๐๐๐๐๐๐
Kwa nini vitu vunavyoanza na “K” ni vitamu sana?
Zuzu kaniuliza, “Anko, unajua vitu vinavyoanzia na K ni vitamu sana.”
Nikashtuka, “Astaghafilulah we mtoto! Niondolee wehu wako hapa!”
Zuzu akatabasamu. Akaendelea kuongea kabla sijafanikiwa kumzuia. “Kweli kabisa anko. Vitu vinavyoanza na K ni vitamu sana kwa mfano kuku, kalimati, keki, kabab, katleti, kashata, kisheti na karoti.”
Nikashusha pumzi. “Ahaa! Kumbe ndo hivyo, ni kweli!”
Zuzu akanitupia swali. “Kwani we anko ulidhani nini?”
Recent Comments