Vichekesho Vya Kukubadilisha Mood
Mke anamwambia mme wake kuwa angetamani mme wake awe tajiri cheki alichojibiwa
Mke; mme wangu ungekuwa tajiri ningefurahi
Mimi; kwa nini?
Mke; ungekuta na sisi tuna gari nzuri hatutembeu kwa mguu
Mimi; ah wap,unadhani ningekuwa tajiri ningekuwa na wewe?ungekuta natoka na kina wema,zariโฆ
๐๐๐
naona anakusanya nguo zake itakuwa anaenda kufua
Angalia kilichojiri katika semina ya wanandoa kuhusu upendo
Kulikuwa na semina ya wanawake kuhusu namna ya kuishi kwa upendo katika ndoa.
Mwalimu aliwauliza ni wangapi wanawapenda waume zao? Wote wakanyoosha mikono kama ishara ya kuwa wanawapenda waume zao.
Mwalimu akauliza tena, โNi lini mara ya mwisho umemwambia mumeo โNakupenda Mpenziโ?
Majibu yalikuwa kama ifuatavyo:
Wengine wakisema Asubuhi ya leo,
Wengine jana,
Wengine wiki iliyopita
Wengine mwezi uliopita
Na wengine wakasema hawakumbuki!
Mwalimu aliwapa kazi kila mwanasemina achukue simu yake na kumtumia mume wake meseji yenye neno โNAKUPENDA MPENZIโ
Baada ya meseji kwenda aliwaamuru kubadilishana simu kila mtu na jirani yake.
Kila mwanasemina aliambiwa kusoma meseji za majibu kwenye simu aliyoshika
Simu ya 1 โ โSamahani, nani mwenzanguโ!
Simu ya 2 โ โSamahani, wrong numberโ!
Simu ya 3 โ โSi nimekuambia usinitumie messages kwenye namba hiiโ!
Simu ya 4 โ โMh! leo mvua itanyeshaโ!
Simu ya 5 โ โNikija tutaongea zaidiโ!
Simu ya 6 โ โโฆโฆImedhibitishwa umepokea Tsh300,000 kutoka kwa โฆโฆโ!
Simu ya 7 โ โMe tooโ!
Simu ya 6 โ โHuu ujumbe ndio ulikuwa unamtumia huyo hawara yako ee, leo utanikomaโ!
Lugha za namba ni noma
Leo kuna mdogo wangu nimemtumia meseji nimemuomba aniazime chaja yake ya simu. Akanijibuย 21002ย Nikawa mkali nikamuambia kuchajia mara moja tu ndio HELA yote hio si bora nikanunue Chaja yangu mpya. Akaniambia nimesema TUMIA TU ๐๐mtatuua na lugha zenu๐
Angalia nilichokifanya Jana kumkomoa x-wangu
Mwenzenu nilikatiwa umeme jana basi leo si nikaamua kwenda kununua luku ya 10,000. Kufika njiani nikatamani fursana nikaingia kijisupermarket mara sindo nakutana na ex wangu! Mshenzi yule kaniona mimi sijui alikua na mpango wa kununua vocha ya jero eti kabadili kanunua vocha ya buku tano ilimradi nione maisha yake safi tangu tuachane. Mambo ya kijinga spendi kudadeky nimetoa buku kumi nikanunua mipampers nami nijifanye nimeowa nina mtoto halafu huyoo nikashika njia yangu.
Sasa washkaji zangu tafadhalini mwenye mtoto au shida ya pampers naomba anunue kwangu maana leo nalala tena kiza ๐โโ
Angalia huyu Jamaa alichomfanyia mke wake jana
Jana niligombana na mke wng, Akaniambia nibebe kila kitu changu niondoke, Bas kiustaarabu tu nikachukua nguo zangu,mwishoni nikambeba na yeye nikamuweka begani nikaanza kuondoka nae
hua sipendagi ujinga, amesahau na yeye pia ni wangu
Huyu mwanamke kazidi sasa
Jamaa: Mambo honey, upo ok?
Mrembo: Sipo ok my dear
Jamaa: Una tatizo gani baby?
Mrembo: Nimetoka hospitali kupima, nna mimba.
Jamaa: Weeh usiniletee balaa hiyo mimba imeingiaje wakati huwa tunatumia kinga?
Mremboย Kwani nani kakwambia mimba ni yako, hebu tuliza mshono huo.
๐๐๐๐๐๐๐
MTATUUA
Haya ndiyo madhara ya kulala kanisani
Tukiwa kanisani mdada alikuwa amelala , akaamka akasikia Pastor anasema
” SIMAMA”
Yule dada akasimama akashangaaa kanisa zima linamtizima kwa mshangao akiwemo mumewe, akaangalia kanisa zima akashtuka kujiona yeye peke yake ndiye aliesimama
Pastor akaendelea vizur endelea kusimama, tumepata mmoja hadi sasa aliyesimama narudia kwa mara ya mwisho kama hujasikia vizuri
” kama wew umewahi kumsaliti au bado unasaliti ndoa yako SIMAMA”
Binti akazimia
Jamaa amkomesha boss wake
Kuna jamaa alifutwa kaziโฆ
Ikawa kila siku anaenda nyumbani kwa boss wake na kunya mlango wa mbeleโฆ Ikawa hvโฆ
boss: _mbona waja kunya kwangu?_
jamaa: _nataka kukuonesha kuwa silali njaa_
๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐
Hii ya mamba na kiboko kali, Wewe unaonaje?
Eti kati yaย MAMBAย naย KIBOKOย nani kiboko???๐๐๐๐
Mi naonaย MAMBAย ndoย kiboko!๐ณ
Ujinga mbele kwa mbele๐๐๐๐๐๐๐ป๐๐ป๐๐ป๐๐ป๐๐ป
SMS Mafua ndiyo hii
JE UMESHAWAHI KUONA SMS MAFUA?
Cheki hii hapaโฆโฆ..
“Mabo dugu yagu mziba? Bwada nasubuliwa sada na bafua baka dashindwa kuadika beseji do hayo dugu yagu.
Diobeeni dipone
๐๐๐๐๐๐๐๐
Hapana Chezea
Bafua
Recent Comments