Vichekesho Vya Kuadisia

Huyu mtoto kaongea point kweli, angalia anachomwambia baba yake

Mtoto alimwuuliza baba yake,
Mtoto: Baba unaweza kumwachia hilo gari lako house boy/girl akaliendesha?
Baba: siwezi kumwachia gari langu hili aliendeshe ni ghali sana.
Mtoto: je mnaweza kumwachia chumba chenu house boy/girl kikiwa wazi na mkaenda kazini?
Baba: haiwezekani kamwe kuna vitu vya gharama na pia heshima haitakuwepo.

Mtoto: unaweza ukampa house boy/girl ATM CARD yako na namba ya siri ukakuchulie pesa?

Baba: mtoto unatafuta balaa sasa, unataka siku akiiba hii card akachukue pesa zote tuwe maskini, sithubutu.

Mtoto: aahaaaaaa, kumbe hauwezi kumkabidhi chochote chenye thamani house boy/ girl, sasa kwa nini mnanikabidhi mimi kwa house boy/girl na nyie mnaenda kazini mpaka mnarudi kumbe mimi sina thamani kwenu eeeeh!

Usichokijua kuhusu sungura, panya na jamii yao

JE WAJUA?

Sungura, panya na Jamii zao huwa na mwendo wa kukimbia na kuruka muda wote na umri wao wa kuishi ni miaka 15. Kobe ni mnyama mwenda pole, asiye na papara wala pilika, muda mwingi hujificha na kupumzika ndani ya jumba lake akikwepa maadui. Umri wa kuishi kobe hufikia hadi miaka 300.
FUNZO: Mazoezi ni kiinimacho na uongo mtupu. Jipumzikie mwaya!!!
🏃🏾🏃🏿‍

Alichofanya mke baada ya mme wake kupenda kumchunga sana

Alifanya hivi;
Siku ya kwanza

MUME: Halooo vipi mke wangu salama weye?.
MKE: Salama tu
MUME: Uko wapi?
MKE: Jamani si niko nyumbani
MUME: Mhh kama kweli uko nyumbani washa blender nisikie…..mke­ akawasha blender
MKE: Umesikia?
MUME: Okay haya mi natoka kazini naja

Siku ya pili
MUME: Vipi mko salama huko?
MKE: Tupo kama ulivyotuacha
MUME: kwani uko wapi?
MKE: Niko nyumbani napika
MUME: Washa brender kama kweli uko nyumbani
Mke akawasha blender
MKE: Umesikia?
MUME: Poa ntarudi baada ya masaa mawili

Siku sita baadae mume akaamua kurudi bila kumtaarifu mkewe alipofika home kamkuta mdada wa kazi yuko peke yake.
MUME: We mama yako yuko wapi?
MDADA: Sijui ameondoka na blender toka asubuhi

Cheki masifa yalivyomponza huyu, Sifa nyingine ni mbaya jamani

Mbongo, Mganda, na Mkenya walikamatwa na makosa Uchina.

Wakaambiwa adhabu ni ama kifo cha moja kwa moja au adhabu nyingine ambayo atakayeifaulu atakuwa huru, atakayeshindwa atauawa.

Basi wao wakaomba wapewe hiyo adhabu nyingine wajaribu bahati yao.

Wakapelekwa msituni wakaambiwa kila mmoja aende kwa njia yake halafu arudi na matunda kumi ya kufanana.

Wakaingia msituni kila mtu njia yake.

… Mganda akarudi wa kwanza na machungwa kumi. Akaambiwa adhabu yake ni kumeza moja moja likiwa zima bila kufumba macho bila kulia wala kucheka wala kujitikisa mpaka yote kumi yaishe. Akameza la kwanza. Safi. Kumeza la pili, akashindwa kuvumilia akafumba macho. Akapigiwa risasi akafa.

Mkenya akaja. Ana vitunda vidogo vidogo kama pili vilaini. Akasomewa masharti. Akaanza kumeza bila kufumba macho wala kulia, wala nini… alipofika cha tisa akashindwa kuvumilia akaangua kicheko! Akapigwa risasi pia akafa.

Wakiwa kuzimu Mganda akamwuliza Mkenya, “Vipi, mbona ulishindwa kuvumilia wakati kilibaki kitunda kimoja tu?”

Mkenya akamjibu: “Mkuu, nilishindwa kuzuia kicheko maana nilimwona Mbongo anakuja na matikiti maji!”

Shopping Cart
1
    1
    Your Cart
    🏠 Home 📖 Reading 🖼️ Gallery 💬 AI Chat 📘 About