Vichekesho Vya Kuadisia
Cheki kilichonipata sasa, ungekua wewe ungefanyaje?
Siku moja katika pitapita zangu nikakutana na mtoto mmoja mkali balaa yaani ni mzuri sanaaaa, moyo ukanituma nimuimbishe mtoto akakubali kwamba nitafute siku tukae tuongee vizuri akasema nimpe namba yangu ya simu.
Ebwana si akatoa simu hiyo inauzwa laki sita mimi hapa nina kisimu cha tochi tena nimefunga na rababendi
Je, wewe ungeendelea kumtajia namba zako!!!
Kweli shilingi yaua, Huyu jamaa kapatikana, angalia anachomjibu mke wake,
Jamaa alikuwa anagombana na mkewe,hatimae
akamwambia kwa ukali
“Unajua nimechoka sasa, haya kusanya nguo
zako na……..
Kabla hajamalizia sentensi simu
ya mkewe ikaita, kumbe alikuwa ni baba yake.
Basi mzee akaanza kuongea na binti yake huku
jamaa anasikia
“Aisee mwanangu nimebahatika kuuza ile
nyumba yangu sasa nimeona niwatumie milioni
20 mjaribu kuanzisha mradi na mwenzio.
Haya mwambie yeye nitampigia kesho kama
ana mradi mwingine nimpe hela kidogo”.Baada
ya simu kukatwa mke akamgeukia jamaa
akamuuliza,”eeenhee!!! ulikuwa unasema
umenichoka nikusanye nguo zangu halafu
iweje? Jamaa kwa upole akajibu “Nilikuwa
nasema ukusanye nguo zako na unipe nifue”.
Huyu mwanamke kazidi sasa
Jamaa: Mambo honey, upo ok?
Mrembo: Sipo ok my dear
Jamaa: Una tatizo gani baby?
Mrembo: Nimetoka hospitali kupima, nna mimba.
Jamaa: Weeh usiniletee balaa hiyo mimba imeingiaje wakati huwa tunatumia kinga?
Mrembo Kwani nani kakwambia mimba ni yako, hebu tuliza mshono huo.
😆😆😆😆😆😆😆
MTATUUA
Cheka kidogo na wewe hapa
*Kama mtaani kwenu mambo yamekuwa tait , usikimbilie mtaani kwetu kwani huku yamekuwa dera kabisa*😂😂😂😂😂
Jana nilipeleka viatu kwa fundi sasa hivi nimekutana nae amevivaa namuuliza ananiambia eti ni ROAD TEST” 😂😂😁
Unakumbuka hizi enzi za utoto?
Kitambo tukiwa watoto ulikuwa unaitwa uje ule kwa lugha tofauti kulingana na chakula kilichopikwa siku na muda husika
1. UGALI NA KUNDE
Mwitaji : 🗣Joniiiii
Mwitikiaji : Eeeh
Mwitaji : Uje ukule
2. UGALI NA SAMAKI
Mwitaji: 🗣 we Joniiii
Mwitikiaji : Eeeh
Mwitaji : Unaitwa na Mama
3. WALI NA NYAMA/KUKU
Mwitaji: 🗣 Joniiii
Mwitikiaji : Eeeh
Mwitaji : Shauri yako!
😂😂😂😂😂😂
Angalia huyu jamaa alivyowafanyia watu uhuni bar
Jamaa kaingia Bar;
Jamaa: Muhudumu, nipe kinywaji na mpe kila mtu humu ndani kinywaji, maana wakati napata kinywaji lazima kila mtu apate kinywaji. Haraka sana muhudumu akagawa vinywaji,
Jamaa: Muhudumu nipe supu na kila mtu humu ndani mpe supu maana ninapokunywa supu kila mtu lazima anywe supu. Watu wakapewa supu tena safari hii wakapiga makofi.
Jamaa: Muhudumu nipe bili, na kila mtu humu ndani mpe bili maana wakati nalipa bili yangu kila mtu lazima alipe yake. Zogo lilianzia hapo…….
Ungekua wewe ndio mama wa huyu mtoto ungemfanyaje?
Kuna mtoto mmoja aliamka kutoka usingizini alipokuwa kalala na mama yake na kupiga kelele “mamaa” mama yake akaamka na kumwambia nin mwnangu mtoto akajibu “mama nimeota ndoto mbaya sana” ndoto gani hyo mwanangu mtoto akajibu “nimeota tumefungua shule”
😂😂😂😂😂
🌚🌚Kibaooooo nyau wewe
Cheki huyu jamaa anachomfanyia huyu mrembo kanisani
Jamaa kaenda kanisani akakaa karibu na mrembo.
Wakati mahubiri yakiendlea jamaa akaanza kuingiza vocal:
Jamaa: dada mi nakupenda saana
Dem: Kaka naomba umsikilize mchungaji
Jamaa: nipe nafasi uwe msimamizi wa serikali ya moyo wangu…
Dem: niache…
Jamaa: kweli nakupenda mpnz
Dem: (kwa sauti kubwa) nmesema NIACHEEEE!!
Watu wote kanisani wakageuka… Jamaa kaona noma na ili atulize msala
Jamaa: sikuachi hadi ukiri YESU kuwa Bwana na mwokozi wa Maisha yako.
Kuwa single nao ugonjwa eh, cheki huyu alichokifanya
Et
Umexhawah kuwa single had ukaamua kununua viatu vya kike kixha ukaviweka mlangon ili majiran wakipita wajue una demu ndani…😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂
KUA SINGLE NAO NI UGONJWA EEENH.😉
Lugha za namba ni noma
Leo kuna mdogo wangu nimemtumia meseji nimemuomba aniazime chaja yake ya simu. Akanijibu 21002 Nikawa mkali nikamuambia kuchajia mara moja tu ndio HELA yote hio si bora nikanunue Chaja yangu mpya. Akaniambia nimesema TUMIA TU 😂😂mtatuua na lugha zenu😜
Je, hii ni kweli kwa wale wasichana wasiojibu meseji WhatsApp!!!?
Ukiona hivyo ujue ndio hivi
Mwanaume mwenzangu ukiona unamtext msg msichana WhatsApp kaisoma hajajibu, umetuma ya pili kasoma hajajibu, ukatuma ya tatu hajajibu mmmmmh😨😨 hapo ujue mwenzio kaangalia kwenye profile yako, kakagua picha weee mwishoni akajisemea tu “Huyu.mkaka hapana kwa kweli”🤣🤣🤣🤣🤣🤣
🏃♂🏃♂🏃♂🏃♂🏃♂🏃♂
Kama mpezi wako akikuita MAMITO Unatakiwa umjibu hivi
Akina dada mpenzi wako akikuita MAMITO usikubali
na yeye mwite MAFORONYA kama mbwai na iwe mbwai🤪🤪🤪🤪🤪🤪
Angalia huyu mgeni anachokifanya, wageni wengine ni hatari
Hata kama ni Mgeni this is too much.
Mwenyeji: Karibu mgeni karibu ukae,utapenda chai au soda?
Mgeni: Nipe nianze na soda wakati chai inachemka.
Mwenyeji: Utakunywa fanta au sprite?
Mgeni: Nipe fanta wakati sprite inapoa.
Mwenyeji: Utakunywa na keki au mkate?
Mgeni: Nipe keki mkate nitanywea chai ikishachemka.
Mwenyeji: Utapendelea ndiz au machungwa,
Mgeni: Nipe machungwa ndizi ntakula na wali
mchana.
Chezea mgeni ww.!!!
MAMBO KUMI YA KUFURAHISHA NA HUWEZI KUYAFANYA
1. Huwezi kuosha Macho kwa Sabuni;
2. Huwezi kuhesabu Nywele zako;
3. Huwezi kupumua kwa Pua na huku umetoa Ulimi;
4. Unajaribu kufanya namba 3
6. Umeona inawezekana, sanasana unakuwa Kama Jibwa;
7. Unatabasamu kwa kuwa umejiona Mjinga!
8. Umeruka namba 5;
9. Unahakikisha Kama kweli 5 haipo.
10. Unacheka kwa kuwa nimekubamba!
Angalia kile kitabia cha kufuta namba kwenye simu kilivyomponza huyu jamaa
Jana nilijipa kazi ya kufuta vitu visivyo na umuhimu kwenye sm yangu. Katika futa futa si nimefuta namba ya bosi wangu. Halafu boss mwenyew wa kike. Mida ya Saa mbili usiku nikawa chumbani kwangu. Mara simu ýäñgù ikawa inaita. Kucheki namba ngeni. Nikapokea baada ya salamu. Me→nani mwenzangu?? Boss→we hunijui me ?? Me→usinijbu swali kwa swali Nita kublacklist sasa hiv. Sipendagi ujinga.. Kwa sasa nazurura tu mtaani na roba langu La machupa
Baadhi ya misemo mikali ya leo
1. Mwanaume hata awe bahili vipi, hawezi kumpa mwanamke mimba nusu.
2. Hata uwe na magari mangapi chooni utaenda kwa miguu.
3. Kama ubinadamu kazi mbona hatupewi mishahara?
4. Ukichanganya wali na choroko unapata mseto, lakini hautibu malaria.
5. Hata njiwa nae ana makinda, lakini hawezi kuwa spika wa Bunge.
6. Hata uwe na haraka vipi kwenda Zenj, huwezi kupanda Jahazi ya Yusuph Mzee.
7. Umeme hauna kiuno lakini unaongoza kwa kukatika.
8. Hata uwe kauzu vipi, huwezi kujamba wakati unatongoza.
9. Hata uwe na imani kali vipi, huwezi kusali wakati unafanya mapenzi.
10. Hata kizibo ni mfuniko lakini hauwezi kufunika sufuria.
Huyu Baba ni noma, Cheki anachomjibu huyu mtoto wake
Mtoto: baba eti Botwasna ipo wap?
Baba: angalia itakuwa humo humo kabatini maana mama yako nae kwa kuficha kuficha vitu hajambo…
Cheka na methali
1.Simba mwendapole =Huyo ni Sharobaro
2.Asiyefunzwa na Mamae= Ujue Mama hajapitia Ualimu
3.Zimwi likujualo= Lilikuona Sehemu.
4.Chelewa Chelewa= Ukizikusanya utapata Ufagio.
5.Hakuna Masika= Wakati wa Kiangazi.
6.Mpanda Ngazi= Asiwe Mwoga kuanguka
7.Dua la kuku=
Bismilah rahman rahim
11.Penye wengi= Pana Ajali au Tukio
12.Ukiona vyaelea= Ujue ni vyepesi.
13.Mwenye nguvu= amekula ugal wa dona(…..)
Recent Comments