Vichekesho Vya Krismass
Angalia nilivyookoa maisha ya mtu leo
Nmeokoa maisha ya mtu asubuhi ya leo huwezi amini.Nmekutana na ombaomba nikamuuliza atajisikiaje nikimpa sh.30,000/-
Akasema ATAKUFA kwa furaha.Nikaondoka bila kumpa ili ASIFE.๐๐๐๐
Eti kwa nini Watu hawapostigi hii? Hata selfie sijaonaga
Vijana mkiwa mnaendesha magari mna post mukiwa mpo beach mna post mkiwa kwenye masherehe mna post Lakin mkiwa mmeenda kwa mganga siwaoni kupost mitunguli na vibuyu vya mganga unakuwa je wa zee tena. ๐๐๐๐
Watoto wa siku hizi ni shida! Angalia huyu mtoto anachomwambia baba yake
Ka ni wewe?
DOGO: baba mi siendi tena shule inaonekana walimu hawana uhakika na majibu yao.
BABA: Kwanini unasema hivyo?
DOGO: juzi walisema 3+4= 7, jana wakasema 1+6=7, halafu leo wanasema 5+2=7 sasa huoni kama wanatuchanganya.
ungekua wewe ungemjibu nini
Kweli tamaa ni mbaya, mke wa mtu kaponzwa na tamaa, ndio basi tena
Jamaa kaenda kwa mke wa rafiki yake:
JAMAA: Shem nakupenda!
MKE: Hebu toka hapa! Je rafiki
yako akijua? tena koma!
JAMAA: Ntakupa milioni 1!
MKE: Basi njoo kesho mchana
mume wangu akiwa kazini!
Kesho yake Jamaa kaja
na milioni 1 wakamalizana na mke wa rafki yake,
jioni ilipofika
Mume akarudi home na
kumuuliza Mkewe, “Rafki yangu SAM kaleta hela yangu milioni 1?”
MKE akajibu kwa unyonge, “Ndio!”
MUME: Yes! Ndio maana nampenda SAM kanikopa asubuhi jioni karejesha!!!!
Mke hoiโฆโฆ
Gari na mke nini muhimu?
GARI YA MILIONI 50
UNALAZA NJEโฆ
mke wa laki sita
unalala nae ndaniโฆ.
BANGI SI NZURI JAMAN
๐๐๐๐๐๐๐๐
Haya ndiyo madhara ya kutowapeleka watoto kanisani โช
MTOTO aliibiwa yeboyebo KANISANI akawa analia sana kwa uchungu mpaka MCHUNGAJI akamwambia usilie mwachie MUNGU. MTOTO akajibu Mungu hazimtoshi zile yebo ni ndogo! Usicheke,
Huu ni Mtihani Tuwapeleke Watoto KANISANI Wamjue MUNGU.
Huu ndio uchawi unaweza kufanyika siku mpenzi wako akikutambulisha kwao
๐๐๐๐๐
*UCHAWI* ni nini?
`Uchawi ni pale mpenzi wako anapokupeleka kwao kufika tyu ghafla unakutana na dada yake getini ambaye alikuwa ni mpenzi wako wa zamani, ile kuingia ndani unamuona kaka yake ambaye mlipigana baada ya kukufumania na mke wake, hujakaa vizuri unamuona mama yake ambaye ndiye jimama shangingi lako anayekuweka mjini akupaye jeuri ya kutamba ambapo hata gari unalolitumia alikupa yeye na hataki upajue anapoishi, wakati unataka kuondoka unakutana uso kwa uso na baba yake ambaye alikuwaga wakili wako kwenye kesi ya ubakaji`
๐คฃ๐๐๐๐๐คฃ
Angalia wadada walivyoumbuka kwenye hii test
Ticha katangaza test , Akatoa Masharti; Ukiandika jibu hamna kufuta au kukata.
Swali la kwanza,
Taja vyakula vi3 ambavyo ukienda hotelini umelipiwa utapenda kula (marks 1)
WAVULANA wakajaza; wali, ugali, mihogo.
WADADA wakajaza; burger, pizza, egg chop. Swali la
2: Eleza jinsi ya kupika kila chakula ulichotaja hapo juu. (marks 99)
wacha wadada waanze kuhangaika kukata majibu ya mwanzo!
Cheki huyu mtoto anachosema
sijui hili toto langu nilipeleke wapi, Leo limetoka shule eti nikaliuliza BIBILIA kwa kingereza inaitwaje likaniambia GRANDMOTHER CRY
๐ ๐ ๐ sijui nikabadilishane na kijiko cha chumvi๐ค๐ค๐ค
Recent Comments