Vichekesho Vya Jumatano

Jinsi ya Kubana matumizi X-mass

Badala yakupika PILAU tutapika TAMBI kwenye Xmas maana tutakua tumeokoa sh.15,000/= Vitunguu swaumu 2000, Vitunguu maji 1000, hiliki 1000, Magome 1000, Michele wa 2000, Soda 3000, Nyama 5000 . Fedha hizi zitatumika kununua mfuko wa cement ili tuanze kujaza kibubu cha ujenzi wa nyumba badala ya kupanga. Karibuni saana maji ya kunywa tumechemsha ndoo nzima.

๐ŸŽ€โœจMarry Xmas & Happy new year.โœจ๐ŸŽ€

Ufugaji wa nguruwe kazi, Cheki jamaa hawa wake walivyompa mtihani

MWANAHARAKATI: Hawa nguruwe unawalishanini?
.

MFUGAJI: Nawalisha mabaki ya chakula toka migahawa mbalimbali
.
MWANAHARAKATI: Hayo ni makosa unawatesawanyama kwa kuwalisha chakula kichafu. Akapigwa fainiโ€ฆ Baada ya siku chache wakaja wanaharakati toka Umoja wa Mataifa
.
MWANAHARAKATI: Hawa nguruwe unawalisha nini?
.

MFUGAJI: Huwa nawaanzia siku na uji wa ulezi, halafu mikate, mchana ugali kwa kabeji na usiku viazi
.
MWANAHARAKATI: Loh watu wanakufa kwa njaa wewe unalisha nguruwe, akapigwa fainiโ€ฆ.siku chache baadae wakaja wanaharakati wa Mazingira
.
MWANAHARAKATI: Hawa nguruwe unawalisha nini?
.
MFUGAJI: (Kwanza akasita kidogo) Hawa huwa nawapa shilingi alfu tano kila mmoja kila siku halafu wao wenyewe wanaenda kununua chakula wanachokitaka.. .

Wanaume wote ni waaminifu

Hii ni kwa wanaume ila mwanamke anaweza kusoma na kujifunza kuwa wanaume wote ni waaminifu.

Mwanaume mmoja alienda kukata miti kwa ajili ya mkaa, bahati mbaya panga likadondokea mtoni, akaanza kulia sana. Malaika akatokea na kumuuliza kwanini analia. Jamaa akajibu; “Panga langu limedondokea mtoni na ndilo ninalotegemea kuendeshea maisha yangu”.

Malaika akazama mtoni na kuibika na panga la DHAHABU na kumuuliza, ndio hili?

Jamaa: Hapana.

Malaika akazama tena na kuibuka na panga la SHABA na kuuliza, ndio hili?

Jamaa: Hapana.

Malaika akazama tena mara hii akaibuka na panga la CHUMA na kuuliza ndio hili?

Jamaa: NDIYO.

Malaika akafurahishwa sana na uaminifu wake hivyo akampa mapanga yote matatu. Jamaa akafurahi sana.

Siku nyingine jamaa alikuwa anatembea na mkewe njiani ghafla mke akadondokea mtoni, jamaa akaanza kulia. Malaika akatokea na kumuuliza: Kwanini unalia?

Jamaa: Mke wangu kadondokea mtoni na nampenda sana.

Malaika akazama mtoni akaibuka na WEMA SEPETU na kuuliza; “huyu ndiye mkeo?”

Jamaa: NDIYO.

Malaika akakasirika sana na kumuuliza: kwa nini umenidanganya?

Jamaa: Nimesema ndiyo kwa sababu ningesema hapana ungezama tena na kuibuka na AUNT EZEKIEL na ningesema hapana tena ungezama na kuibuka na MKE wangu alafu ningesema ndiyo ungenipa wote watatu!

Sasa mimi maskini sina uwezo wa kuhudumia wote hao, ndio maana nikasema NDIYO kwa Wema Sepetu.

*FUNDISHO*
Wanaume huwa hatusemi uongo bila sababu na inakuwa sababu maalumu kwa faida ya wote.

WANAUME WOTE NI WAAMINIFU. Hii ndiyo kauli mbiu yetu.
๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€

Angalia wanachokifanya Zuzu na msichana chumbani kwenye giza

Zuzu: Mambo Anna!
Anna: Poa!
Zuzu: Kuna kitu nataka nikuonyesheโ€ฆ
Anna: Kitu gan?
Zuzu: Twende chumbani kwako (wakaenda)
Anna: Haya nionyesheโ€ฆ

Zuzu: Funga mlango na madirisha kwanza (akafunga)
Anna: Haya nionyeshe sasa!..
Zuzu: Zima taa kwanza (akazima)
Anna: Mhmโ€ฆnionyeshe sasa!
Zuzu: Haya njoo hapa kitandaniโ€ฆ
Anna: Ok, nionyeshe!
Zuzu: Ona nimenunua saa ambayo inawaka yenyewe gizaniโ€ฆ Acha mawazo mabaya ww???

Cheki kilichotokea stesheni ya treni, mambo mengine ukipaniki inakula kwako kama huyu jamaa

Jamaa Wawili Walifika Stesheni, wakakuta Treni ndo kwanza inaondoka. Wakaanza Kuikimbiza. Mmoja akafanikiwa kupanda akaondokaโ€ฆ

Yule aliyebaki akaanza kucheka sanaa mpaka machozi yakamtoka. Watu wakamuullza, unacheka nini sasa wakati umeachwa? Akawajibu: “kinachonichekesha, yule aliyepanda alikuwa ananisindikiza.

Angalia kilichompata huyu mwanafunzi kilaza anayejiamini

Teacher: Who is a pharmacist?

Shemdoe raised up his hand.

Teacher: So itโ€™s only Shemdoe that can tell who a pharmacist is in this class? So there is no body else to answer the question except Shemdoe? (There was no reply from the students)

Teacher: Ok now Shemdoe, chukua hii fimbo, charaza vilaza hawa wote kila mmoja viboko kumiโ€ฆ. Shemdoe akiwa amevimba kichwa, akawatwanga viboko kumi kumi vya kushiba darasa nzima

Teacher: Now, my dear Shemdoe tell this dumb students who a pharmacist isโ€ฆ

Shemdoe: Yes, sir. A Pharmacist is a farmer who assists people. Shemdoe saiv amelazwa MOI kwa wataalam wa mifupa ๐Ÿƒ

Angalia huyu jamaa alivyowafanyia watu uhuni bar

Jamaa kaingia Bar;
Jamaa: Muhudumu, nipe kinywaji na mpe kila mtu humu ndani kinywaji, maana wakati napata kinywaji lazima kila mtu apate kinywaji. Haraka sana muhudumu akagawa vinywaji,

Jamaa: Muhudumu nipe supu na kila mtu humu ndani mpe supu maana ninapokunywa supu kila mtu lazima anywe supu. Watu wakapewa supu tena safari hii wakapiga makofi.
Jamaa: Muhudumu nipe bili, na kila mtu humu ndani mpe bili maana wakati nalipa bili yangu kila mtu lazima alipe yake. Zogo lilianzia hapoโ€ฆโ€ฆ.

Tofauti ya mke na mchepuko!!!

Mke ni kama Tv na Mchepuko ni kama Simu.
Nyumbani unaangalia Tv lakini ukitoka unatoka na simu.

Mara chache unafurahia Tv lakini Muda mrefu unacheza na simu yako.

Tv ni bure kwa maisha yako yote, lakini Simu kama hujalipia hupati huduma.

Tv ni kubwa nzito na wakati wote ni ya zamani. Lakini simu ni nzuri, nyembamba, na ni rahisi kubeba.

Gharama za huduma za tv ni ndogo sana, Lakini gharama za huduma za Simu ni kubwa na pia ni lazima kuzitimiza.

Tv ina remote lakini Simu haina.

Kitu muhimu zaidi simu ina njia mbili za kuwasiliana unaongea na unasikiliza lakini Tv unalazimika kusikiliza hata kama hutaki au unataka.

Unaweza kununua Tv mara moja na ukatumia kwa kipindi kirefu lakini Simu mara zote unabadilisha inategemea na fasheni.

Ya mwisho na ya kuzingatia

Tv haina Virusi lakini Simu inayo.

KUWA MAKINI.

Shopping Cart
22
    22
    Your Cart
    Kitabu cha SMS Maalumu kwa Umpendaye
    Kitabu cha SMS Maalumu kwa Umpendaye
    1 X Sh2,500 = Sh2,500
    ๐Ÿ  Home ๐Ÿ“– Reading ๐Ÿ–ผ๏ธ Gallery ๐Ÿ’ฌ AI Chat ๐Ÿ“˜ About