Vichekesho Vya Jumapili
Duh, hii sasa kazi
Wakati unafikiria dingi yako afe ili urithi nyumba, dingi nae anafikiria uanze kufa ili apangishe chumba unacholala.. hiyo inaitwa kufa kufaana.. πππππππππ #Hatutaki ujinga
Kwa nini vitu vunavyoanza na “K” ni vitamu sana?
Zuzu kaniuliza, “Anko, unajua vitu vinavyoanzia na K ni vitamu sana.”
Nikashtuka, “Astaghafilulah we mtoto! Niondolee wehu wako hapa!”
Zuzu akatabasamu. Akaendelea kuongea kabla sijafanikiwa kumzuia. “Kweli kabisa anko. Vitu vinavyoanza na K ni vitamu sana kwa mfano kuku, kalimati, keki, kabab, katleti, kashata, kisheti na karoti.”
Nikashusha pumzi. “Ahaa! Kumbe ndo hivyo, ni kweli!”
Zuzu akanitupia swali. “Kwani we anko ulidhani nini?”
Cheka kidogo na wewe hapa
*Kama mtaani kwenu mambo yamekuwa tait , usikimbilie mtaani kwetu kwani huku yamekuwa dera kabisa*πππππ
Jana nilipeleka viatu kwa fundi sasa hivi nimekutana nae amevivaa namuuliza ananiambia eti ni ROAD TEST” πππ
Soma hii, Nani haelewi kati ya hawa?
Dogo: Bro naomba nitumie hela.
Bro: Tumia tu mpaka uchoke.
Dogo: Hujanielewa,nitumie hela.
Bro: We ndo hunielewi, nimesema tumia tuβ¦!!!
Bangi si mchezo, Angalia kilichowakuta hawa
Bangi si mchezo!
Jamaa kaikoleza si ikamtuma avue nguo!
Akavua nguo zote akaenda kwenye kioo, kujitazama akaona kama kavaa suti!
then akaenda kama alivyo zaliwa kwa masela wenzake akawauliza vp suti imenikaa? Mvuta bangi mwenzie akamwambia “imekutoa kinyama ila tai umeifunga chini sana”.
Wachaga kweli kiboko: Mcheki huyu mchaga na mbuzi!!!
Mchaga alinunua mbuzi akamwambia mpishi Nyama nusu ipike pilau na ingine itie kwenye friza. Kichwa fanya supu, miguu fanya mchuzi chukuchuku. Ngozi usitupe tutafanya mswala, utumbo pikia ndizi na mifupa tutawauzia wenye mbwa. Kinyesi kihifadhi kwa mbolea ya bustani.
Mpishi akamuuliza Hutaki na sauti ya mbuzi tufanye ring tone kwenye simu yako? Mchaga akajibu Yesuu! hivi inawezekana? bac fanya hivyo tuwauzie na wengine hiyo ringtone. ππ
Hii ndio ndoto ya harusi ya kila msichana anayotamani
GIRL: Baby, hebu niambie harusi yetu itakuwaje?
BOY: Yaani hii haijawahi kushuhudiwa, ngoja nikupe kionjo kidogo tu
GIRL: Enheeβ¦
BOY: Kwanza siku ya kupeleka mahari nitaswaga zizi zima la ng’ombe napeleka kwa babu yako
GIRL: Ooh baby u care..
BOY: Siyo hivyo tu, baba yako ntamnunulia Range Rover Sport na mama mkwe ntampa Range Rover Evoque
GIRL: Baby u are awesomeβ¦
BOY: Halagu mdogo wako wa kiume ntampa Prado Tx, na hapo nimesukutua tu mdomo sijaanza kulaβ¦.
GIRL: Enheeβ¦na sisi??
BOY: Sisi tutachukua mtaa mzima Oysterbay, kila wiki tutaishi nyumba tofauti
Halafu siku ya harusi yetu tutakodi zile meli zinabeba makontena ndiyo iwe ukumbi wetu, itatupeleka hadi Maldives
GIRL: Baby I love you
BOY: Tukitoka hapo tunaenda honeymoon Bahamasβ¦.halafu tunaenda Taiwan shopping ya fenicha, kisha Japan shopping ua electronics, halafu tunaenda Dubai nikununulie vito vya thamani
GIRL: Ooh my sweetheartβ¦halafu tukitoka huko??
BOY: Tukitoka huko nachukua ndoo ya maji nakumwagia uzinduke usingizini na ndoto yako imeishia hapo
Mambo ya pesa haya..
MAMBO YA FEDHA AISEEβ¦β¦. Kuna jamaa alipewa shilingi 983628763600/= β¦acha uvivu, najua hujasoma ni kiasi gani hicho cha fedha na mbaya zaidi hujagundua kwamba katikati ya namba hizo kuna herufi Aβ¦ safi sana, najua umeangalia tena kuiona hiyo herufi, bahati mbaya hujaiona. πππππππ
Hii sasa kali kweli kweli!!
MCHUNGAJI alitangaza kila mwanaume aliye na mke atoe sadaka kulingana na uzuri wa mke wakeβ¦bac watu wakaanza kutoa 50,000/= 30,000/= na 20,000/=.
Kuna jamaa akatoa 500/=.
MCHUNGAJI akamuita ofisin akamuuliza.
MCHUNGAJI:Ina maana mkeo siyo mzuri?. Jamaa akajibu: Ukimuona utanirudishia na chenji.
ππππππππππ
Cheki hawa washikaji wanachokifanya baada ya kuvuta bangi, Bangi si mchezo
Kuna washikaji walikuwa wakivuta bangiβ¦ kiberiti kikawaishiaβ¦ wakamtuma mwenzao akatafute kingineβ¦ bangi lilikuwa limemkoleaβ¦ akazungukazunguka hatimaye akarudi palepale kijiweniβ¦
MSHIKAJI:Β oyaaa wanangu eeehβ¦ niazimeni kiberiti mwanangu mwenyewe β¦..
WENZAKE:Β baharia ee subiria kimtindo kuna mwana tumemtuma akatafute kiberiti.
Huyu mwanamke ni noma cheki alichomwambia mme wake baada ya kumnunulia nguo za ndani
Mume kaingia duka la nguo na kamnunulia mke wake chupi dazeni moja zote za rangi nyeusi, akaenda kumzawadia. Mpenzi akashukuru lakini alipogundua kuwa zote ni nyeusi si akaropoka.
MY HONEY: Sasa umeninunulia chupi zote nyeusi, sasa watu si watadhani nina chupi moja tu sibadili,
Jamaa alifura akawa kama mbogo na hapo ndipo zogo kuu lilipoanza
MUME:Watu gani hao watakaokuambia unachupi moje, inamaana unawaonyesha kitumbua changu? Leo utanambia’
Ungekuwa wewe ungefanya nini?
Pale umapofanya interview huku ukijua hutapata kazi
Pale unaitwa kufanya interview na unajua tuu hutapata kazi tuuβ¦..
Interviewer: where were u born?
Guy: Tanzania Interviewer: okay which part?
Guy: what do u mean which part, the whole body was born in Tanzania..
πππ Cpendagi ujinga mim
Madogo wa sikuizi ni kiboko, cheki huyu alichokifanya akiwa darasani na mwalimu wake
Muda wa kwenda nyumbani ulikuwa umefika, mwalimu
akasema: yeyote atakaye jibu swali langu lolote kwa usahìhi ataondoka asiye jibu atabaki.
Dogo mmoja akatupa begi nje ya dirisha.
Mwalimu akauliza nani katupa ilo begi nje?
Dogo akajibu fasta mimi. Akafungua mlango akaenda kwao.
neno moja kwa dogo
Njia 3 rahisi za kuondoa kitambi
JE, una KITAMBI na unataka kukiondoa?
FANYA HAYA;
1. Kopa mkopo mkubwa benki
2. Nunua gari bovu la biashara
3.Oana na mke mwenye kelele.
Ukiona miezi mitatu hakijaisha basi ujue umevimba BANDAMA sio kitambi..
Amri za chuo
Ndio hizi sasa
1.Hicho ndicho chuo chako usiwe na chuo kingine ila hicho.
2.Usilitaje bure jna la chuo chako mana utawaumiza wengine.
3.Ikumbuke cku uliyochaguliwa na kuiheshimu.
4.Waheshimu tcu, bodi ya mkopo na uongoz wa chuo ili upate kuendelea kuwepo chuon.
5.Usisapu
6.Usidisko
7.Usitumie mkopo ovyo.
8.Usitaman chuo cha mwenzio
9.Usitamani fakat ya mwenzio
10. Usitaman bumu lake wala chochote alichonacho. hahaha chezea chuo weye!
Misemo 17 ya kuchekesha
1) gari la kuvutwa halina overtake
2) kisigino hakikakai mbele
3) wimbo wa taifa haupgwi disko
4) feni haiwashwi beach
5) mshkaki hauchomwi kwa jiko la ges
6) mganga haagiz tembele
7) hata bibi alikuwa bint
8) mke wa mtu sumu,mume wamtu maziwa
9) kipara bila pesa ni kovu
10) mbwa hanenepi migiuu
11) picha ya rais haina bodyguard
12) mjini shule kijiji tuition
13) saa ya ukutani haivaliwi mkonon
14) heshima pesa shkamoo makelele
15) ulinz pesa bastora mzgo
16) kuku ni kuku jogoo mbwembwe
17) kusoma kuelewa kukesha mbwembwe
Januari kweli ngumu, soma hii
Januari kweli kiboko
Hii january sabuni za kuogea ni zile za kuoshea vyombo, yani unakutana mjini na mtu ana mchicha shingoniβ¦π
Dongo kwako kama una degree moja Halafu unachagua kazi
Mtu una degree 1 unachagua kazi! Wakati thermometer ina degree 100, inafanya kazi kwenye kwapa.
πππππ
Ni Utani tuuuuu!
Ulishawahi kukutana na hii? Maana yake ni nini?
Ulishawahi kutana na hiiβ¦.
Issa: mambo
Jeni:poa vp
Issa:poa nambie:
Jeni:poa aje ww:
Issa:poa nambie
Jeni:poa
Issa :bas poa
Jeni:poaβ¦.
Issa:poa badee basi
Jeni:haya
Issa:bai
ππππβ¦β¦..HII KIITALIANO INAITWA LACK OF SOUND ENGINEERING NA HII INASABABISHWA NA UOGAβ¦β¦
Recent Comments