Kuna watu makauzu ila huyu kazidi.. Soma hii!
Kakubaliana vizuri na msichana fulani hivi kuwa aibuke gheto, mchizi kajipanga vizuri kabisaโฆ. mara saa nne hivi mdada kasema hana nauli.
Mshkaji kajikunja kamtumia Elfu tano maana mwenye shida alikuwa ni yeyeโฆโฆ
Baada ya nusu saa yule dada akamtumia meseji.
“Jamani mpenzi, kumbe baba hatoki nilijua atatokaโฆ sorry bae sitaweza kuja kwa leoโฆ sooo sorry!”
Mshkaji jiii! hajajibu kituโฆ..
Baada ya muda kidogo meseji ikaingia katika simu ya binti, akajua mchizi kajibu. Mh! kutazama ni meseji kutoka Mpesa.
“CA90F0511 IMETHIBITISHWA Tshs 5000 ILIYOTUMWA KIMAKOSA KATIKA ACCOUNT YAKO IMETOLEWA SALIO LAKO NI Tshs 5”
Halafu ndo ikaingia meseji ya mshkaji.
“BASI POA SIKU NYINGINE KAMA VIPI”
#dada wa watu mashavu yakamshukaโฆ hakuamini kilichotokeaโฆ. yaani jamaa keshawapigia Voda na pesa fasta imezuiliwaโฆโฆ
Recent Comments