Vichekesho Vya Jumanne
Angalia hawa vichaa walichokifanya, Vichaa bwana, ni noma!
Vichaa walipanga kutoroka, wakakubaliana wamnyonge mlinzi watoroke!
Walipofika getini wakakuta geti lipo wazi na hakuna mlinzi, wakasema “Turudi mipango yote imevurugikaโฆ
Cheki kilichotokea stesheni ya treni, mambo mengine ukipaniki inakula kwako kama huyu jamaa
Jamaa Wawili Walifika Stesheni, wakakuta Treni ndo kwanza inaondoka. Wakaanza Kuikimbiza. Mmoja akafanikiwa kupanda akaondokaโฆ
Yule aliyebaki akaanza kucheka sanaa mpaka machozi yakamtoka. Watu wakamuullza, unacheka nini sasa wakati umeachwa? Akawajibu: “kinachonichekesha, yule aliyepanda alikuwa ananisindikiza.
Tenda Wema Uende Zako
Nimekuta panya ana struggle kuingia chini ya mlango wa jirani yanguโฆ
Nikagonga mlango Jirani kafungua panya akapenya mi nkaenda zanguโฆ..
Tenda Wema Uende Zako!!! Sipendi Ujinga mimi kwanini panya wa watu apate shida
Duh! Hiki nacho chombo cha moto?
_Sheria inasema kila anaetembea na chombo cha moto barabarani sharti awe na leseni._
_Sasa hawa wauza kahawa mbona wanatembea na chombo cha moto lakini hawakamatwi ๐ก._
_Hizi sheria zinapendelea._
๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐
Sio kwa wivu huu
Wanawake nilianza kuwachukia tokea shule ya msingi.
Ni pale mwanamke wangu aliponiacha na kwenda kwa jamaa mwenye kichongeo kipya โฆinauma sanaaโฆ
WANAWAKE SIO WATU WA MCHEZO MCHEZO ASEEE Bac tuu
Huyu jamaa amekomeshwa, majambazi ni shida!
CHEKA KIDOGO
Majambaz waliliteka gar moja lililokua limeshehen abiria
Baada ya abiria kusachiwa na majambaz hao na kukutwa hawana pesa, majambaz wakasema kila m2 atapigwa viboko (bakora) kutokana na namba ya shati alilovaa
Aliyekua hana namba atasalimika
Kaz ikaanza, jamaa alievaa jez ya ROONEY wa Man U akapigwa fimbo 10, mwengine alievaa nguo ya 50cent akapigwa 50, n.k, sasa kwa pemben kulikua na jamaa analia sn yaani kila akijiangalia, kumbe alikua amevaa fulana limeandikwa LOWASA 2015 duuuh! Unajua kilichotokea ngoja niweke cm chaji kwanza.
Angalia alichojibu huyu mwanafunzi, Ungekua wewe ni mwalimu wake ungemfanyaje?
Mwanafunz alikuwa kila siku anachelewa shule, na kila siku alikuwa anachapwa, basi siku moja mwalimu akaona ngoja amuulize.
Mwalimu: Mbona unachelewa kila siku?
Mwanafunzi: Nakaa mbali mwalimu
Mwalimu: (huku ana hasira akauliza)Mbali mbinguni?
Mwanafunzi: Mbinguni kwa mbele๐๐๐๐๐
Recent Comments