Duh, hii sasa kazi
Wakati unafikiria dingi yako afe ili urithi nyumba, dingi nae anafikiria uanze kufa ili apangishe chumba unacholala.. hiyo inaitwa kufa kufaana.. πππππππππ #Hatutaki ujinga
Wakati unafikiria dingi yako afe ili urithi nyumba, dingi nae anafikiria uanze kufa ili apangishe chumba unacholala.. hiyo inaitwa kufa kufaana.. πππππππππ #Hatutaki ujinga
Kuna maprofesa 40 walipanda AIR TANZANIA ili wasafari. Kabla ndege haijaanza kuondoka, Lilipita tangazo kama ifuatavyo:
Ndugu wasafiri wote, ndege unayotarajia kusafiri nayo imetengenezwa na wanafunzi wa Kitanzania.
Baada ya tangazo maprofesa wote waliteremka isipokuwa mmoja alibaki kwenye kiti chake
Walipomuuliza ni kwanini hakuondoka akajibu kwa haraka na furaha kuwa:
Kama ndege hii imetengenezwa na watanzania, hata kuwaka haitawaka!
Kuna siku nilichalala kipesa nikaamua kuomba dem wangu aniazime 10,000/= akanipa.
Baada ya siku mbili nikapata pesa zaidi ya laki nne hivi, nikaamua kumpa 100,000/= mpenzi wangu bila yeye kuniomba.
Baada ya siku 3 akaja kuniambia:- “Bae, ile 10,000/- niliyokuazima mwenyewe amekuja kunidai, so kama unayo naomba unipe nimrudishie maana ananisumbua leo siku ya 3.”
SAA HIZI NIPO ZANGU SINGLE NATAFUTA DEM MWINGINE
Mwalimu aliingia darasani na kuwauliza wanafunzi juu ya ndoto zao za baadae.
MWAL: John we unataka ukiwa mkubwa uwe nani?
JOHN: Nataka niwe daktari wa moyo niwasaidie watanzania wanaougua magonjwa ya moyo.
MWAL: vizuri. Na wewe Rose unataka kuwa nani?
ROSE: Nataka kuwa rubani, niweze kusaidia watu wanapenda kusafiri kw anga.
MWAL: Safi sana Rose. Utakua utakua mfano kwa wasichana wenzio kuwa na bidii kwenye masomo ya sayansi.
MWAL: Na wewe James??
JAMES: mimi nataka kuwa tajiri mkubwa sana. Niwe na nyumba Tanzania, S.Africa, Marekani na Dubai. Niwe na gari 7 za kutembelea. Kila siku nabadilisha. Leo nikipanda hii, siirudii hadi week iishe. Nataka niwe namiliki viwanda, Makampuni, ndege binafsi na mashamba makubwa. Nataka niwe na nguvu serikalini ya kuamua nani awe Rais na nani asiweβ¦β¦”
Akameza mate kisha akaendeleaβ¦.
“Nataka kuwa na walinzi 20 wenye silaha nzito wakinizunguka, na watumishi wakininyenyekea. Nataka kuwa bilionea ninayeogopwa. Lakini pia nataka kuwa na mke mzuuuri sana ambaye nitakuwa natembea nae kila mahali.”
MWAL: ndoto nzuri sn lakini unahitaji bidii sana kutimiza. Haya na wewe Jenny tueleze unataka kuwa nani??
JENNY: Nataka kuwa mke wa James.!!
PAMOJA NA HALI NGUMU YA UCHUMI NCHINI HUWEZI AMINI MSHAHARA WA DHAMBI HAUJABADILIKA HATA KIDOGOβ¦BADO NI MAUTI VILEVILE
ππππ
Ndio nilikuwa nimeshuka kwenye basi la SAI BABA pale Ubungo, nina Begi kubwa Mgongoni na begi Dogo la Lap Top mkononi, sura inatazama Mbele Very Serious kama nipo kwenye Gwaride la Uhuru!..Mabega juu yanafanya Cheers na Mawingu!, natembea kwa madoidoβ¦..leo nimetoka Likizo Moshi,
“Brother Simu ya ukweli hii..kitu cha Tecno C9 bei poa” hii ilikuwa sauti ya Teja mmoja hivi!
Yaani huyu Teja Bwege kweli,anataka kumuuzia nani sabuni? mimi sio wa kuja!β¦kamwe Siwezi kuibiwa hapa Town,hakuna wizi au utapeli nisioujua!, Mimi nimezaliwa Mwananyamala kwa Manjunju, nikalelewa Tandale kwa Mtogole, Shule ya msingi nimesoma Turiani Magomeni, Hivi Mbwa gani aniibie?β¦kwa Style ipi?
Sipendi kabisa Upuuzi!, Wajinga ndio wataibiwa, sio Mimi!β¦sasa Kwa mwendo wa haraka nikatoka nje kabisa ya Stendi ya Ubungo straight mpaka Stendi ya dala dala za Kariakoo, hapo ndipo nikakutana na Vijana wawili wadogo wakiwa na mzani wa kupimia uzito,β¦hakika napenda sana vijana wanaojituma kama hawa na sio ile Mijizi ya kule ndani Stendi!!,β¦.hapa sasa nikapata wazo!
“Dogo mnapima uzito kwa shilingi ngapi?”
“Mia mbili tu Kaka!”
”Ok”
Kwa mwendo wa kikakamavu nikapanda juu ya mzani,lengo hapa ni kujua uzito wangu, Mtori niliokula mwezi mzima kule kwa Mshekuu sio mchezo, hapa nahisi nacheza kwenye kg za John Cena,
“Mama wee! Dogo mzani mzima huu kweli? Mbona nina kilo 134?” (Nilihamaki)
“Aaah! Brother huoni umepanda na Mabegi juu ya mzani?”’
Hahaha! kweli nimechanganyikiwa!β¦Sasa nikatoa mabegi yote mawili na kurudi juu ya Mzani, hapa ndipo Uzito ukashuka kutoka kg 134 mpaka kg 56!β¦My God kweli Body la “One Pack ” haliongopi! thats means mabegi yaliniongezea kg 78! duh hii ni hatari!
“Yaani we Dogo kitambi chote hiki kg 56? huu Mzani Mzima kweli?”
Kimyaβ¦
“Dogo huu Mzani vipi?”
Kimyaβ¦
Dogo ana dharau huyu!β¦Sasa ndio nikabandua macho yangu toka kwenye kioo cha mzani ili nimtazame huyu dogo asiyejibu!β¦.ndipo macho yangu yakakutana na Kigoda tupu kilichochongwa Mvomero!β¦Dogo hakuwepo!β¦.na Mabegi pia hayapo!β¦lap top haipo!β¦.NIMEPIGWA!
Ni dhahiri watoto wa Mjini walikuwa wameniacha juu ya Mzani, wamechukua Lap top ya Milioni na wameniachia Mzani chakavu wa elfu 40, what a stress!β¦.sasa nilirudisha macho kwenye kioo cha uzito na sasa kilisoma KG 38!β¦yaani dakika hii hii nimepungua kilo zingine 18, Hakiyamama nahisi hata utumbo wangu wamebeba!β¦niitieni Ambulance!
ππΌππΌππΌππΌππΌππΌππΌππΌππΌππΌππΌ
π π π π π
Jamaa kaenda kanisani akakaa karibu na mrembo.
Wakati mahubiri yakiendlea jamaa akaanza kuingiza vocal:
Jamaa: dada mi nakupenda saana
Dem: Kaka naomba umsikilize mchungaji
Jamaa: nipe nafasi uwe msimamizi wa serikali ya moyo wanguβ¦
Dem: niacheβ¦
Jamaa: kweli nakupenda mpnz
Dem: (kwa sauti kubwa) nmesema NIACHEEEE!!
Watu wote kanisani wakageuka⦠Jamaa kaona noma na ili atulize msala
Jamaa: sikuachi hadi ukiri YESU kuwa Bwana na mwokozi wa Maisha yako.
Babu: Mjukuu wangu ngoja nikusimulie hadithi ya mimi babu yako kwenye vita ya kagera
Mjukuu: Niambie babu
Babu: Kwenye vita ya kagera tulienda sehemu tukakamatwa wote askari na maadui wakatuambia chagueni kuuliwa au kubakwa.
Mjukuu: Sasa babu wewe ulichagua nn?
Babu: Niliuliwa!!!
JE UMESHAWAHI KUONA SMS MAFUA?
Cheki hii hapaβ¦β¦..
“Mabo dugu yagu mziba? Bwada nasubuliwa sada na bafua baka dashindwa kuadika beseji do hayo dugu yagu.
Diobeeni dipone
ππππππππ
Hapana Chezea
Bafua
House girl mmoja alipewa kazi na mzungu mara akavunja sahani.
Mzungu aliporejea,kazin akamuuliza ‘what happened to my plate?
House girl akajbu: ‘The dog wow wow friji paaa, mchuzi mwaaaa the vyombo pangalapangala the sahan ngelengenjeeβ¦β¦the pasuka paaaaaaaa
ππππhadi saiz mzungu bado anasoma dictionary hajui lugha gani imetumika
MCHUNGAJI; “Unakunywa bia!?
MLEVI; “Ndio.
MCHUNGAJI; “Kwa siku unakunywa bia ngapi!?
MLEVI; “Nakunywa bia tano!
MCHUNGAJI; “Bia moja bei gani!?
MLEVU; “2500/
MCHUNGAJI; “Ulianza lini kunywa bia!?
MLEVI; “Miaka 18 iliyopita!
MCHUNGAJI; “Kwa hiyo kwa siku unatumia zaidi ya 10,000??
MLEVI; “Ndio!
MCHUNGAJI; “Kama u gekuwa unatunza hiyo pesa 10,000 kwa siku leo hii si ungekuwa na Range Rover!?
MLEVI; “Samahani, naweza kukuuliza swali!?
MCHUNGAJI; “Uliza!
MLEVI; “Unakunywa bia!?
MCHUNGAJI; “Hapana!
MLEVI; “Nionyeshe Range Rover yako!
MCHUNGAJI; “akasepa”
Kuishi kijijini kunahitaji moyo sana
..unaenda kuoga, unakumbuka kuwa umesahau sabuniβ¦unaenda kuchukua sabuni kurudi bafuni, unakuta ng’ombe amekunywa maji yote..unaamua kufuata mengne,unarudi unakuta mbuzi kala sabuniβ¦ππππ
Mzee wa miaka 60 alimwambia mkewe, leo nataka tukumbukie enzi zetu kutongozana, mke akajibu sawa, inabidi unisubiri mwembeni saa 1 usiku nitapita, mzee akafika saa 1 alikaa hadi saa 5 usiku, aliporudi nyumbani akamuuliza mkewe kwa hasira; sasa tumepanga nin halafu haujatokea ?
Mke; leo mama alinikataza nictoke nyumbani usiku nijisomee ! Babu hoiiβ¦
Recent Comments