SMS ya kumsisitiza mpenzi wako asiende kwa mwingine
chekecho la huba ,toka uvunguni mwa moyo wangu
navika moyo wako taji la upendo,na kupulizia marashi ya hubaa ,usimpe mwingine mi ndiye ninayejua kulea.
chekecho la huba ,toka uvunguni mwa moyo wangu
navika moyo wako taji la upendo,na kupulizia marashi ya hubaa ,usimpe mwingine mi ndiye ninayejua kulea.
Nilikuwa nikifiria kwamba ndoto haziwezi kuwa kweli,
lakini nilibadili mawazo yangu pale tu nilipokuona wewe.
Naweza kukuazima mabega yangu upande, masikio yangu
usikilizie mikono yangu ushikie, miguu yangu, utembelee,
lakini si moyo wangu kwani tayari unao wewe.
utamu wa penzi hunogeshwa na pendo la dhati pia utamu wa
penzi ni uwepo wangu na wako,ladha yake ni zaidi ya nazi
kwenye wali au royco kwenye mchuzi au pilipili kwenye
kachumbari, utamu wake ni zaidi ya asali au jam kwenye
mkate ,blueband kwenye uji.penzi tamu halina kifani
Siku zote kwangu ni sherehe ni wewe unishereheshaye,ukweli
usio na kejeli mapenzi yako yanatii kiu yangu,moyoni
mwangu nimeridhia… .nakupenda daima mpenzi!
kila niamkapo mawazo yangu huwa kwako na upepo uvumapo
huhitaji uwepo wako na hasa nikukumbukapo kumbato
lako,nakupenda mpenzi
Kumjali mtu ni rahisi, lakini kumfanya mtu akujali ni
vigumu, nashangaa umewezaje kunifanya nikujali?
Wanasema mtu huanguka katika mapenzi mara moja, jambo
ambalo mimi naliona si la kweli kwa maana kila
ninapokutazama najikuta nakupenda tena na tena.
Anayekupenda ni mimi,watakaokutamani ni wengi,tafuta dunia
nzima penzi langu la kweli huwezi kulipata,penzi langu
kwako ni nuru daima halizimiki.
Recent Comments