Ujumbe wa mapenzi kwa umpendaye kwa dhati
Nakupenda usiku na mchana
Nakuwaza siku zote za maisha yangu
Nakupenda usiku na mchana
Nakuwaza siku zote za maisha yangu
Mpenzi kila tunapokuwa chumbani huwa napenda kuwa mbunifu,
huwa najitahidi kuepuka udhaifu, ili
mapenzi yangu yasikukifu, ENDELEA KUFURAHIA MAPENZI YANGU.
Mchana mwema
Unaweza kutuma Ujumbe huu kwa Umpendaye hapa
Mawingu yametanda napanda kwenye kitanda, macho nayaangaza, taratibu navuta shuka na kujitanda, mishumaa pembezoni inaniangaza, mziki laini wanibembeleza kitu pekee nilichokikosa ni joto lako na vijimambo vyako kunako kitanda!
Unaweza kutuma Ujumbe huu kwa Umpendaye hapa
Happy birthday mpenzi, nakuombea kwa mwenyezi akupe
maisha marefu na kukuepusha na maradhi,
pongezi kwa wako wazazi
kwa kukuzaa mpenzi,
nakupenda la azizi.
Nitaenda mbali Zaidi ya maono yako
Safarini nitajenga hekalu la pendo letu
Nitapuliza filimbi kama ishara ya utambulisho wako
Na mwanzo wa sherehe ya ndoa yetu
Wewe ni wapekee ninaekupenda, sifikirii kukusaliti na wala sina wazo la kukutenda, nakuomba tuendelee kupendana siku zote habbity wangu
Fikra hutawala mtima wangu,
Kwa madhila yalojaa duniani,
Kwa muhali wa yanayojiri,
Kwa machweo na mawio,
Kwa totoro ama nuruni,
Nao moyo hukosa ukamilifu,
Kwa utashi wa zake hisia,
Zinipazo sababu kuu,
Ya upendo juu yako,
Ya kukufanya daima uwe,
Mawazoni mwangu.
Mawazoni ama ndotoni,
Daima wewe hutawala,
Kila asubuhi niamkapo,
Nao usiku nilalapo,
U chakula changu akilini,
Nalo tulizo langu moyoni,
Daima huuwaza upekee,
Wewe uliojaaliwa,
Na hivyo naihisi furaha,
Daima wewe uwapo,
Mawazoni mwangu.
Utamu wako ni zaidi ya asali, ni wa asili usiohitaji
kuongezewa ladha ya sukari, nitaumiss endapo
kama ukiwa mbali “NIACHE NIKUPENDE SWEET”
sura yako haifutiki usoni mwangu kirahic,ingawa upo mbali
nami lkn penzi lako bado nalikumbuka,hakuna anayeweza
kukata kiu yangu zaidi yako,nakupenda mpenzi.
Recent Comments