Meseji nzuri ya kumtumia mpenzi umpendaye kwa moyo
Katika nyuso za dunia, na kati ya miamba ya jangwani,
Kuna SAUTI! Neno la pendo lako liotapo karibu yangu.
Ni zaidi ya roho iendayo safarini.
Katika nyuso za dunia, na kati ya miamba ya jangwani,
Kuna SAUTI! Neno la pendo lako liotapo karibu yangu.
Ni zaidi ya roho iendayo safarini.
Mwanamke ni yule amfanyaye mwanamme auhisi uanaume wake,
wewe ni mwanamke mwenye sifa hizo.
Lazima utakuwa mwizi sababu umeiba moyo wangu, umechoka
sababu unakimbia mara zote akilini mwangu, na labda mimi
sina shabaha sababu mara zote nikikulenga nakukosa.
Fikra hutawala mtima wangu,
Kwa madhila yalojaa duniani,
Kwa muhali wa yanayojiri,
Kwa machweo na mawio,
Kwa totoro ama nuruni,
Nao moyo hukosa ukamilifu,
Kwa utashi wa zake hisia,
Zinipazo sababu kuu,
Ya upendo juu yako,
Ya kukufanya daima uwe,
Mawazoni mwangu.
Mawazoni ama ndotoni,
Daima wewe hutawala,
Kila asubuhi niamkapo,
Nao usiku nilalapo,
U chakula changu akilini,
Nalo tulizo langu moyoni,
Daima huuwaza upekee,
Wewe uliojaaliwa,
Na hivyo naihisi furaha,
Daima wewe uwapo,
Mawazoni mwangu.
nilivyokutana nawe siku ya kwanza nilikupenda kwa
dhati,nikakueleza ukweli ukanikaribisha moyoni
mwako,siwezi kuchezea nafasi hiyo laaziz,nitakushika
daima.
Uchungu wa kifo hauna tofauti na maumivu nitakayoyapata
ukiniachana, mpenzi usiniache nami siko tayari kukuacha
Niliumbwa kwa ajili yako, mbele yako
nitakushika mkono, nikuonyesha sayari yangu,
pendo langu la undani,
na nitakUHESHIMU milele mpenzi wangu.
pindi nikukumbukapo chozi langu huwa linatoka bila
sababu,kasi Ya mapigo ya moyo Huongezea Pasipo
Sababu,nimegundua Nakuhtaji Naomba Unikubalie.
Ni ngumu kwa watu wawili kupendana wanapoishi Dunia
tofauti, lakini Dunia hizo zikutanapo na kuwa kitu kimoja,
hiyo ndiyo maana ya kuitwa wewe na mimi.
Recent Comments