Ujumbe kwa mpenzi wako kumwambia hutopenda mwingine zaidi yake
Si vibaya mimi kukusifia kwani wewe ni wangu, nivingi umejaaliwa, vinavyouvutia moyo wangu, ama hakika uzuri wako umedhibiti matamanio yangu “SINTOMPENDA MWINGINE ZAIDI YAKO”
Si vibaya mimi kukusifia kwani wewe ni wangu, nivingi umejaaliwa, vinavyouvutia moyo wangu, ama hakika uzuri wako umedhibiti matamanio yangu “SINTOMPENDA MWINGINE ZAIDI YAKO”
Furaha yangu ni kuwa nawe kwani u zaid ya mboni
yangu,najisifu kuwa nawe maishani mwangu naamini itatokea
kutokuwa mbali nawe mpz wangu,unisahaulishe machungu na
karaha za huu ulimwengu .nakupenda dia.
teke la kuku halimuumzi mwanaye sawa na dhati ya mapenzi
haiumzi moyo wa ampendaye,tugombane sasa hivi tupatane
badaye,najua hakuna wasiogombana ,kama wapo siku
wakigombana wataachana.
Nitafute wakati una huzuni, nitafute wakati hamna wa
kukusikiliza. Sijali kama mimi ni kimbilio lako la mwisho,
bali sipendi ulie peke yako.
Kila unachokifanya natamani niwepo, nikitumainia kila
ndoto yako itimie kila muda na sehemu, niwepo nikikutakia
mafanikio mema kwasababu nakujali.
Penzi lako ndiyo pumzi yangu nawezaje kukuacha laazizi,
ina maana nife??? Siwezi kukuacha nakupenda. Nitakupenda
mpaka mwisho wa uhai wangu.
Neno Nakupenda Hutamkwa Kwa Lugha Legeeevu Yenye
Kuambatana Na Hisia Nzito Zilizofikicha Mioyoni
Mwetu,hutamkwa Kwa Kauli Bashasha,nakshi Na Hofu Ndani
Yake.raha Yake Umpate Anayekujali Kama Mi Ninavyokujali
Nakupenda Mpz
Kila mtu anataka kuwa jua linalong’arisha maisha yako,
lakini ni afadhali niwe mwezi, ili nikuangazie wakati wa
giza ambapo jua limechwea na haliangazi tena.
Umbo lako kama sayari, lizungukapo umbile la jua
ni kama upendo wa thamani usioweza kuuzika.
Recent Comments