Meseji ya kumsihi mpenzi wako azidi kukupenda
Natambua ugumu wa mapenzi
Mengi ni matamu, mengine ni machachu
Ila nakusihi usikate tamaa ya kunipenda kimoyo
Natambua ugumu wa mapenzi
Mengi ni matamu, mengine ni machachu
Ila nakusihi usikate tamaa ya kunipenda kimoyo
Simu huboa wakati mwingine, kwani ni lazima ufungue meseji
na kuzisoma, kuichaji simu kila mara, lakini usichoke
kwani ndiyo inayotuwezesha tuwasiliane
Mpenzi unawafahamu maadui wa mapenzi yetu ? Ni wale rafiki
zako wanaokuletea maneno ya uongo, ndugu zako
wanaotugombanisha na wachawi wanotuotea mabaya,
tujihadhari tusiwape ushindi. Mapenzi yetu yadumu daima.
Hakika wewe ndiye wangu mahabuba unayejua kunipa huba,
napenda unavyoniganda mithili ya ruba, nahahidi kukupa
mahaba yanayozidi shaba. Nakupenda.
sipo tayari kuukabidhi moyo wangu kwa mwingine zaidi
yako,wewe ni wa pekee maishani mwangu mwenye kujua hisia
moyoni mwangu
mpenzi nipende daima pendo lako nitalienzi, nakupenda
Mpenzi kila tunapokuwa chumbani huwa napenda kuwa mbunifu, huwa najitahidi kuepuka udhaifu, ili mapenzi yangu yasikukifu, ENDELEA KUFURAHIA MAPENZI YANGU. Mchana mwema
Lazima utakuwa mwizi sababu umeiba moyo wangu, umechoka
sababu unakimbia mara zote akilini mwangu, na labda mimi
sina shabaha sababu mara zote nikikulenga nakukosa.
Niliumbwa kwa ajili yako, mbele yako nitakushika mkono, nikuonyesha sayari yangu, pendo langu la undani, na NITAKUHESHIMU milele mpenzi wangu.
Unaweza kutuma Ujumbe huu kwa Umpendaye hapa
nakupenda sana mpenzi wangu ,we ndo wa pekee mwenye kujua
furaha ya moyo wangu nikiwa na majonzi huwa upo karibu
nami,nikiwa na furaha huja kushea nami,ahsante wangu
tabibu ,we ndo wangu wa manani.
Recent Comments