Swali la kizushi kwa wadada wanaovaa mawigi
Hivi wadada mnaovaa mawigi.
๐๐ฝย Utajisikiaje siku Boyfriend wako anaingia chumbani halafu anatundika NDEVU kwenye henga๐คฃ
Hivi wadada mnaovaa mawigi.
๐๐ฝย Utajisikiaje siku Boyfriend wako anaingia chumbani halafu anatundika NDEVU kwenye henga๐คฃ
Mwalimu aliuliza swali
“Kwanini watu wanapenda MAPENZI kuliko VITA?
Mwanafunzi mmoja akajibu:-
“Kwa sababu CONDOM ni bei rahis kuliko BUNDUKI.
Wanafunzi wote: Ndioooooโฆ!!
Leo nikaamua niingie misa ya asubuhi kwenye kanisa moja la kilokole kulikua na ugeni wa mchungaji kutoka Bulgaria, Mahubiri yameanza saa 1 asubuhi hali ikawa kama hivi:
MCHUNGAJI: My name is Pastor Livingstone
MKALIMANi: Kwa jina naitwa mchungaji Jiwe linaloishi
MCHUNGAJI: We thank God for All goals we set by our hands
MKALIMANI: Tunamshukuru Mungu kwa Magoli yote tuliyoweka kwa Mkono
Hivi navyoongea kanisa halina viti waumini wote tumekimbia nje naona Mkalimani amebaki na kiatu cha kushoto tu.
Sunday joke
CHEKA KIDOGO
Majambaz waliliteka gar moja lililokua limeshehen abiria
Baada ya abiria kusachiwa na majambaz hao na kukutwa hawana pesa, majambaz wakasema kila m2 atapigwa viboko (bakora) kutokana na namba ya shati alilovaa
Aliyekua hana namba atasalimika
Kaz ikaanza, jamaa alievaa jez ya ROONEY wa Man U akapigwa fimbo 10, mwengine alievaa nguo ya 50cent akapigwa 50, n.k, sasa kwa pemben kulikua na jamaa analia sn yaani kila akijiangalia, kumbe alikua amevaa fulana limeandikwa LOWASA 2015 duuuh! Unajua kilichotokea ngoja niweke cm chaji kwanza.
Mzee wa miaka 60 alimwambia mkewe, leo nataka tukumbukie enzi zetu kutongozana, mke akajibu sawa, inabidi unisubiri mwembeni saa 1 usiku nitapita, mzee akafika saa 1 alikaa hadi saa 5 usiku, aliporudi nyumbani akamuuliza mkewe kwa hasira; sasa tumepanga nin halafu haujatokea ?
Mke; leo mama alinikataza nictoke nyumbani usiku nijisomee ! Babu hoiiโฆ
*Jihadharini* na wachapaji wa kadi za harusi. Hakikisha unasoma maandishi yaliyochapwa kabla ya kadi kuchapwa na kusambazwa!
Mchapaji aliombwa aweke 1 Yohana 4:18 katika kadi ya harusi lakini mchapaji kwa makosa aliweka Yohana 4:18.
1 Yohana 4:18 panasema, “Katika pendo hakuna hofu, lakini pendo lililo kamili huitupa nje hofuโฆ”
Lakini Yohana 4:18 tunasoma, “Kwa maana umekuwa na waume watano, naye uliye naye sasa siye mume wako.”
๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐_MKE MTARAJIWA AKAZIMIA HAPA, TUNAMPEPEA_
JAMAA alimuaga mke wake mlokole kuwa anaenda semina ya siku tatu, kumbe anakwenda kwa bi mdogo.
Mke akamwambia mumewe; “Tupige magoti tusali”,
Wakapiga magotiโฆ:
MKE: Eee baba msaidie mume wangu afike salama safari yake.
MUME: Emenโฆ
MKE: Mpe nguvu katika yote atakayoyafanya huko.
MUME: Emenโฆ
MKE: Akitaka kufanya uasherati ashindwe.
MUME: Kimyaโฆ
MKE: Akifanya uasherati apatwe na janga baya kwa uwezo wako bwana.
MUME: โฆโฆ.!!
MKE: Yaani akifanya uasherati afie hukohuko kwa mateso makali.
MUME: Maombi gani sasa hayo!!?. Haya basi siendi semina ufurahi wewe.
Chezea mawaifu walokole wewe!
Jamaa alikuwa na tabia ya kutembea na binamu yakeโฆ.
Alikuwa anasubiri mjomba na mkewe walale tu halafu ananyata mdogo mdogo mpaka chumbani kwa binamu yake.
Siku moja umeme ulikuwa umekatika ikabidi aamue kuvua nguo kabisachumbani kwakeโฆ.
Akanyata taratibua akafungua mlango akazama chumbani kwa mjomba ake bila kujua, ghafla umeme ukarudiโฆ
MJOMBA; we mshenzi umefata nini chumbani kwangu tena uko uchi
JAMAA; nimekuja kukuaga kesho naondoka
MJOMBA; ndo uje uchi?
JAMAA; ndio kwasababu nimeshapaki kila kitu kwenye begi
๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐
Kuna jamaa alipata ajali akapofuka macho๐, akaenda hospital akawekewa macho ya paka๐๐ฑ,
dokta akamuuliza: vipi saizi unaona?
jamaa: naona ila naona panya tu
๐๐๐๐๐
โฆUpo kazini umeacha familia yako nyumbani mara ghafla unapigiwa simu kutazama unakutana na no ngeni na kuamua kuipokea ndipo unakutana na Sauti ya msichana ya kuvutia lakin kabla hajasema shida yake anaamua kukata simu. Unashikwa na hamu ya kujua ni nani. Tamaa ya mchepuko inakujia ghafla na kuamua kuipiga ile no tena kwa mara nyingine inakuwa haipatikani.
Siku hiyo hiyo usiku ukiwa umelala chumba kimoja na mkeo meseji inaingia tena kwenye cm yako kwa ile namba iliyokupigia mchana ikikuomba umpigie kwa mida ule na kusisitiza kuwa ana hamu ya kukufahamu. kila ukimtumia meseji ya kumdanganya upo sehemu mbaya hasikii anakubipu mara nyingi. Uzalendo unakushinda, unamuangalia pembeni mkeo kalala fofofo kajifunika shuka hadi usoni. Unaamua kuondoka kwa kunyata mpaka sebuleni kwenda kuipiga Ile namba kwa lengo la Kumwambia kesho mkutane. Ile unafika sebuleni na kuanza kuipiga ile cm ndipo unakutana na sauti hii:-ย MUME WANGU ACHA MCHEPUKO, NILIKUWA NAKUPIMA TU RUDI TU CHUMBANI TULALEย ๐๐๐๐๐๐๐๐ Hapo ndo utajua kwann bata hata ale kokoto anaharisha ๐๐๐๐๐๐๐๐
Miaka 13: Usipende wavulana ni wabaya.
Miaka 18: Sitaki nikuone na yule mvulana tena!
Miaka 23: Lini utatuletea mchumba wako?
Miaka 26: Wenzio wanaolewa.
Miaka 30: Tumekuambia kwamba acha
kuchagua sana wanaume, hutaki kusikia!
Miaka 33: Kuna mtu wa Mungu yupo kule
anaombea unaweza kupata mchumba
Miaka 36: At least pata mtoto mmoja.
Miaka 39: We will take care of all the wedding
billsโฆyeyote ni sawa sisi tutagharamia kila kitu mwanetu wee mlete tu .
Miaka 45: hivi kweli nani alikuroga.?
๐๐๐ changamkia fulsa umri ukifika
Jamaa alimpa ujauzito mwanafunzi akashtakiwa kumbe yule jamaa ana bibi yake mtaalam wamambo yetu ya Jadiโฆ
Jamaa akaongea na bibi yake amuwekee jinsia ya kike ili akashinde Mahakamani na akitoka arudishiwe mambo yake kama kawaida.
Bibi akampachika jamaa jinsia ya kike alipofika mahakamani kuhojiwa akasema mi sijampa ujauzito kwasababu minina jinsia ya kike piaโฆ!
Kwa kuthibitisha akajifunua nguo, basi jamaa akashinda kesi.
Jamaa akawa anarudi Home, lakini wakati anakaribia kufika akaona watu wengi wamejaa home wanalia akauliza kulikoni akaambiwa “Bibi amefariki”!
Vuta picha hapoโฆ!!!
Nimekuta panya ana struggle kuingia chini ya mlango wa jirani yanguโฆ
Nikagonga mlango Jirani kafungua panya akapenya mi nkaenda zanguโฆ..
Tenda Wema Uende Zako!!! Sipendi Ujinga mimi kwanini panya wa watu apate shida
Jana nateremka kwenye BASI UBUNGO nataka nichukue TEKSI hadi KIMARA naambiwa sh.15,000/=.
Wakati niponatafakari hiyo bei, nikasikia “Moro, Moro,Morogoro sh.6,000/=”
Nikaamua nipande niende zangu MOROGORO.
Kwenda na kurudi sh.12,000/=.
Wakati wa kurudi nikamwmbia KONDA aniteremshe KIMARA.
SIPENDAGI UJINGA MIMI NA BEI ZA TEKSI.
๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐
๐คฃ๐คฃ๐คฃ๐คฃ
Recent Comments