SMS Nzuri: Meseji za Vituko Vya Uganda

Angalia kilichojiri katika semina ya wanandoa kuhusu upendo

Kulikuwa na semina ya wanawake kuhusu namna ya kuishi kwa upendo katika ndoa.
Mwalimu aliwauliza ni wangapi wanawapenda waume zao? Wote wakanyoosha mikono kama ishara ya kuwa wanawapenda waume zao.
Mwalimu akauliza tena, β€œNi lini mara ya mwisho umemwambia mumeo β€œNakupenda Mpenzi”?

Majibu yalikuwa kama ifuatavyo:
Wengine wakisema Asubuhi ya leo,
Wengine jana,
Wengine wiki iliyopita
Wengine mwezi uliopita
Na wengine wakasema hawakumbuki!
Mwalimu aliwapa kazi kila mwanasemina achukue simu yake na kumtumia mume wake meseji yenye neno β€œNAKUPENDA MPENZI”
Baada ya meseji kwenda aliwaamuru kubadilishana simu kila mtu na jirani yake.
Kila mwanasemina aliambiwa kusoma meseji za majibu kwenye simu aliyoshika

Simu ya 1 – β€œSamahani, nani mwenzangu”!
Simu ya 2 – β€œSamahani, wrong number”!
Simu ya 3 – β€œSi nimekuambia usinitumie messages kwenye namba hii”!
Simu ya 4 – β€œMh! leo mvua itanyesha”!
Simu ya 5 – β€œNikija tutaongea zaidi”!
Simu ya 6 – β€œβ€¦β€¦Imedhibitishwa umepokea Tsh300,000 kutoka kwa ……”!
Simu ya 7 – β€œMe too”!
Simu ya 6 – β€œHuu ujumbe ndio ulikuwa unamtumia huyo hawara yako ee, leo utanikoma”!

Huyu mchaga kazidi sasa, angalia anavyomfanya huyu mbuzi

Mchaga alinunua mbuzi akamwambia mpishi Nyama nusu ipike pilau na ingine itie kwenye friza. Kichwa fanya supu, miguu fanya mchuzi chukuchuku. Ngozi usitupe tutafanya mswala, utumbo pikia ndizi na mifupa tutawauzia wenye mbwa. Kinyesi kihifadhi kwa mbolea ya bustani.

Mpishi akamuuliza Hutaki na sauti ya mbuzi tufanye ring tone kwenye simu yako? Mchaga akajibu Yesuu! hivi inawezekana? bac fanya hivyo tuwauzie na wengine hiyo ringtone. Chezeya mchaga!

Mke alichomfanyia mme wake kabla ya kwenda safari, Chezea mawaifu walokole wewe!

JAMAA alimuaga mke wake mlokole kuwa anaenda semina ya siku tatu, kumbe anakwenda kwa bi mdogo.

Mke akamwambia mumewe; “Tupige magoti tusali”,

Wakapiga magoti…:
MKE: Eee baba msaidie mume wangu afike salama safari yake.
MUME: Emen…

MKE: Mpe nguvu katika yote atakayoyafanya huko.
MUME: Emen…

MKE: Akitaka kufanya uasherati ashindwe.
MUME: Kimya…

MKE: Akifanya uasherati apatwe na janga baya kwa uwezo wako bwana.
MUME: …….!!

MKE: Yaani akifanya uasherati afie hukohuko kwa mateso makali.
MUME: Maombi gani sasa hayo!!?. Haya basi siendi semina ufurahi wewe.

Chezea mawaifu walokole wewe!

Shopping Cart
🏠 Home πŸ“– Reading πŸ–ΌοΈ Gallery πŸ’¬ AI Chat πŸ“˜ About