SMS Nzuri: Meseji za Vituko Vya Mchana Huu
Jinsi Mapenzi yanavyoweza kukupa stress
Mapenzi ni balaa
Mapenzi ujue yanawez kukupa stress adi mama ako akikuuliz what’s wrong🤔-—unawez kumjib MAMA WE BADO MDOGO UWEZ ELEW🤣🤣🤣
Dunia ina mambo! Angalia kilichotokea baada ya mgonjwa kuwekewa macho ya paka
Kuna jamaa alipata ajali akapofuka macho👀, akaenda hospital akawekewa macho ya paka🐈🐱,
dokta akamuuliza: vipi saizi unaona?
jamaa: naona ila naona panya tu
👀🐀🐁🐀👀
Januari kweli ngumu, soma hii
Januari kweli kiboko
Hii january sabuni za kuogea ni zile za kuoshea vyombo, yani unakutana mjini na mtu ana mchicha shingoni…😂
Tofauti ya ukopaji wa mzungu na mswahili
MZUNGU: Hi, I need $100, will pay back on Monday
MSWAHILI: Kaka vipi, shwari? Dah.. hatuonani mzee, mishe vipi, mnatunyima nini? Juzi nimekuona kwa mbaaali… mzee shavu dodo, full kipupwe! Sie tupo bwana, shida tu, afu misiba mingi tu, wife nae kajifungua ghafla. Sasa, kuna cheque naisubiri haijatoka hadi leo, wanasema itatoka next week, hapa nimekwama kweli. Naweza pata ‘Laki Moja’ ya karibu hapo nitarudisha mwisho wa mwezi…?😂😂😂😂😂
Majibu ya mkato ya kuchekesha Kutoka Kenya
Njeri: Roysambu ni ngapi?
Makanga: Roysambu ni moja tu. Pengine kama Chinese wamejenga ingine.
Odhis: Hii gari haina watu bana.
Makanga: Kwani hao wawili wenye wamekaa hapo ndani ni ng’ombe?
Man: Wekeni nyimbo za Yesu tafadhali.
Makanga: Yesu bado hajatoa album. Akitoa tutaeka.
Mwikali: Excuse me conda…gari za Mwingi zinapandiwa wapi?
Makanga: Ziliacha kupandwa juu hazimei.
Man: Kwani mwisho wa gari ni wapi?
Makanga: Mwisho ni hapo penye number plate iko.
Karis: Ruaka ni how much?
Makanga: Sijaskia Ruaka ikiuzwa. But nikiskia nitakwambia.
Passenger: Shukisha dere.
Makanga: Tukishukisha dere utaendesha gari?
Johnny: Maze, hii gari iko na joto sana.
Makanga: Basi shuka upande fridge
Angalia huyu mwanafunzi anachomjibu huyu mwalimu wake
1. Ticha:”Punda ni mnyama anaefugwa nyumbani,lakini akiwa mwituni anaitwa pundamilia….Je sungura anayeishi mwituni anaitwaje?”
ZUZU:”Sunguramilia.”
2.Ticha:”Rais wa kwanza wa kenya aliitwa KENYATTA…Je rais wa kwanza wa
Tanzania aliitwaje?”
ZUZU:”TANZANIATTA.”
3. Ticha:”Kuku yuko katika jamii ya NDEGE…Je samaki yuko katika jamii ya nini?”
ZUZU:”MELI.”
4. Ticha:”Coach wa Arsenal anaitwa ARSENE,wa Man-city anaitwa MANCINI….Je wa
Liverpool anaitwaje?
ZUZU:”LIVER.”
5 Ticha:”Ukiwa na mbuzi 10,wezi waje waibe 5,utabaki na nini?”
ZUZU:”Hasira nyingi sana!”
Kifahamu Kidada kimbea kilichofukuzwa kazi
Unafahamu?
Kile kidada kimbea kinachosemaga salio lako halitoshi kimefukuzwa kazi saivi kupiga simu ni bure mjulishe na mwenzako
📲 📲
Cheki masifa yalivyomponza huyu, Sifa nyingine ni mbaya jamani
Mbongo, Mganda, na Mkenya walikamatwa na makosa Uchina.
Wakaambiwa adhabu ni ama kifo cha moja kwa moja au adhabu nyingine ambayo atakayeifaulu atakuwa huru, atakayeshindwa atauawa.
Basi wao wakaomba wapewe hiyo adhabu nyingine wajaribu bahati yao.
Wakapelekwa msituni wakaambiwa kila mmoja aende kwa njia yake halafu arudi na matunda kumi ya kufanana.
Wakaingia msituni kila mtu njia yake.
… Mganda akarudi wa kwanza na machungwa kumi. Akaambiwa adhabu yake ni kumeza moja moja likiwa zima bila kufumba macho bila kulia wala kucheka wala kujitikisa mpaka yote kumi yaishe. Akameza la kwanza. Safi. Kumeza la pili, akashindwa kuvumilia akafumba macho. Akapigiwa risasi akafa.
Mkenya akaja. Ana vitunda vidogo vidogo kama pili vilaini. Akasomewa masharti. Akaanza kumeza bila kufumba macho wala kulia, wala nini… alipofika cha tisa akashindwa kuvumilia akaangua kicheko! Akapigwa risasi pia akafa.
Wakiwa kuzimu Mganda akamwuliza Mkenya, “Vipi, mbona ulishindwa kuvumilia wakati kilibaki kitunda kimoja tu?”
Mkenya akamjibu: “Mkuu, nilishindwa kuzuia kicheko maana nilimwona Mbongo anakuja na matikiti maji!”
Huyu mme ni shida
MKE..mume wangu unaweza kuua simba kwasababu yangu???
MME: Hapana mke wangu, sema kingine
MKE:unaweza kunipa nione watsapp yako nione msgs?
MME: Haya sema huyo simba yukwap nikamuue
Huyu kashauzwa!! Angalia kilichomkuta sasa
Jamaa alionekana Mnyooooonge sana ikabidi mpita njia amuulize…
Kaka, mbona u mnyonge hivyo?”
Jamaa : ‘aaaaah we niache tu, kuna rafiki yangu nimemkopesha laki tano akafanye PLASTIC SURGERY ya uso, Mwanaharamu sasa nashindwa kumtambua!!!
😂😂😂😂😂😂
Cheki kilichotokea stesheni ya treni, mambo mengine ukipaniki inakula kwako kama huyu jamaa
Jamaa Wawili Walifika Stesheni, wakakuta Treni ndo kwanza inaondoka. Wakaanza Kuikimbiza. Mmoja akafanikiwa kupanda akaondoka…
Yule aliyebaki akaanza kucheka sanaa mpaka machozi yakamtoka. Watu wakamuullza, unacheka nini sasa wakati umeachwa? Akawajibu: “kinachonichekesha, yule aliyepanda alikuwa ananisindikiza.
Ex wangu kasema tukapime, cheki nilichifanya
Ex wangu leo kaupdate status yake ya watsap et
“NILIOTEMBEA NAO WOTE MKAPIME”
Saizi nipo apa kwa fundi nguo, napimwa kitambaa Harusi sijui lini anapenda kushtukiza huyu
Wadada lenu hili. Mimi sipo
Wadada kama una sura mbaya subiri NEEMA YA BWANA..Sio kutuambia mna uzuri wa Ndani usioonekana..Sisi ni Wanaume,Sio MINYOO
😂😂😂😂
Maisha ya Pwani ni Shidaaaaah
😆😆 😂😂😂😂😂😂 Jamaa kagombana na mkewe, akasusa kula🍽🍨 kurudi kazini kamkuta mkewe amevaa kanga imeandikwa ukisusa wenzio wala ilipofika asubuhi mke akavaa kanga imeandikwa ukitoka 🚶🚶mwenzio anaingia💃💃
jamaa akagoma kwenda kazini 😬😬 mke akabadili kanga na kuvaa iloandikwa nimemdhibiti ndo mana hatoki🚷 jamaa akaenda kuomba ushauri kwa rafiki yake akaambiwa twende nyumbsni kwako, walipofika walimkuta mke kavaa kanga imeandikwa ulidhani rafiki yako kumbe adui yako🤔🤔 jamaa akaamua kusafiri siku tano ili kupunguza hasira. Aliporudi akamkuta mke amevaa kanga imeandikwa ni bora nimpe jirani kuliko kiozee ndani
😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂
hata kama hupendagi ujinga kwa maneno ya kwenye kanga utasanda tu
Wasichana wafupi wanafurahisha
Wasichana wafupi wananifurahisha sana…. Yaan siku ya Valentine, wakivaa magauni mekundu huwa wanakuwa kama Fire extinguishers au mitungi ya Oryx 😁😁😁😁😀
Kapresha kakiamua kuja kanakujaga tuu, cheki kilichompata huyu mme wa mtu mpenda michepuko
Kimchepuko chako kinakuandikia meseji kama hii…
…Samahani baby kama unavyojua nimeokoka ,nimetubu kanisani lakini nabii kaniambia niwaombe msamaha wote niliowakosea.
Nimemkosea sana mkeo kwa kumwibia mumewe na nimepanga kuja kumwomba msamaha kesho ntakuja na nabii na Mchumba wangu mpya nilie mpata kanisani.
Samahani kwa usumbufu uliojitokeza lakini hilo ni kwa ajili ya utukufu wa bwana!!!
Wako Manka wa Magorofani😅😅
Sifa mbaya: Cheki kilichompata huyu mwanaume mpenda sifa
SIFA MBAYA…
Jamaa alikuwa ndani ya daladala Mara simu ikaita alikuwa ni mkewe kwa sifa jamaa akaweka loud speaker ili watu wasikie wanavyopendana.
JAMAA;wife Mara hii umenimiss jaman
WIFE; kwa nini umekunywa uji wa mtoto?!!!
😂😂😂😂😂
Angalia nilivyomkomoa huyu dogo
Kuna mtoto wa jirani ananibore sana kila nkimtuma kitu dukani lazima aonje,
Jana nlimtuma sukari akala yote..
Sahii nmemtuma superglue haongei Sipendi ujinga mimi
😡😡😡😡😡😡
Vichekesho vya kukuondoa mawazo leo
Soma vichekesho hivi;
Mwizi wa atm
Jamaa aliibiwa kadi yake ya benk akaulizwa kama ameripoti polisi akajibu “sijaripoti bado, mwizi mwenyewe hamfikii matumizi kama mke wangu.
Cheka kidogo
Njia rahisi kusahau matatizo yako (japo kwa muda mfupi) vaa viatu vinavyokubana.
Mlizi mbio mbio
Tulikuwa bar moja jana mlinzi kaingia spidi, akamwambia jamaa mmoja aliyekaa kaunta, Mlinzi: Mzee gari lako limeibiwa Mzee: Umemtambua aliyeiba? Mlinzi: Hapana lakini nimeandika namba za gari hizi hapa.
13, 13…
Jamaa alikuwa anapita nje ya wodi ya vichaa akasikia mtu anasema, 13, 13, 13, 13, 13, 13,….. akaamua kuchungulia kwenye kitundu alichokiona ajue kuna nini, ile kuchungulia tu akamwagiwa mchanga wa machoni, sauti ikabadili ikaanza 14,14,14,14,14……
WATAALAM
Jamaa alikuwa anaumwa sana, mkewe akamwita daktari, alipofika akamkuta jamaa kafumba macho;
Dokta: Huyu mbona amekwisha kufa?
Jamaa: Sijafa bwana
Mke: Hebu nyamaza bwana acha kubishana na wataalamu.
Ya leo mgonjwa
Dokta alipotembelea wodi ya mgonjwa wake aliyepata ajali. Mgonjwa akiwa amening’inizwa mikono juu akauliza “dokta ntaweza kweli kupiga kinanda nkitoka hospitali?”
Dokta: Bila shaka utaweza, wewe ni mpiga kinanda mzuri enh?
Mgonjwa: Hapana sijawahi kabisa bado.
4WD
Mwanaume alimnunulia pete ya almasi mkewe, rafiki akauliza “si ulisema anapenda gari yenye four wheel drive, mbona umenunua pete?” Mume akajibu “unadhani wapi ntapata rav4 feki?”
Ajali ilivyotokea
Trafiki polisi akihoji palipotokea ajali “ahaa! Sasa naanza elewa embu nielezee jinsi ajali ilivyotokea wewe ukiwa kama dereva mhusika.” Dereva akajibu “hata sikumbuki nlifumba macho”
Faini ya kukojoa
Polisi alimdaka jamaa anakojoa pembezoni mwa ukuta.
Polisi: Wewe unajua panakatazwa kukojoa hapa?
Jamaa: Sasa nimebanwa nifanyaje?
Polisi: Faini yake elfu tano.
Jamaa akatoa noti ya elfu 10.
Polisi: Sasa chenji tunaipataje?
Jamaa: Tafuta chenji unipe changu.
Polisi: Basi kojoa tena…
Mume anaenda kazini
Jamaa kaamka asubuhi sana Jumamosi, mvua inanyesha kang’ang’ania kuwa anaenda ofisini. Kawasha gari yake, kufika njiani hali ilikuwa mbaya kaamua kurudi. Kafika home kavua nguo kaingia tena kitandani, kamnong’oneza mkewe aliyekuwa usingizini; “Yaani hali ya hewa huko nje mbaya sana” Mke: Si ndio nimemshangaa huyu mpumbavu eti kaenda kazini…
Hasira za mtoto
Baba na mtoto:
Baba: Mwanangu ukiwa na hasira unafanya nini?
Mtoto: Naenda chooni.
Baba: Chooni? Kufanya nini?
Mtoto: Kusafisha.
Baba: Halafu ndio hasira zinaisha?
Mtoto: Ndio. Nasafisha choo kwa mswaki wako.
Mgonjwa na Dokta
Mgonjwa: Dokta nimekuja nahisi ninaumwa Malaria na kifua.
Dokta: Sasa ushajua unaumwa nini hapa umefuata nini kwangu?
Mgonjwa: Sasa si nimekuja kwa dokta.
Dokta: Wanaojua kuwa wanaumwa kama wewe wanapitiliza maabara.
Pilau la bachela
Bachela mmoja aliyekua akiishi kwa muda mrefu peke yake kwenye nyumba aliyopanga siku moja alitaka kupika pilau kwa mara ya kwanza. Sasa asijue nini kinachobadilisha rangi ya wali kuwa rangi ya brown, yeye akapika kama kawaida (wali) kisha wakati wa kula akavaa miwani yenye rangi ambayo ukiuangalia wali unauona kama pilau wakati anakula.
Mwizi na chizi
Mwizi kaiba TV na kuanza kukimbia nayo, kumbe ile nyumba mlikuwa na chizi, akaanza kumkimbiza yule mwizi. Kila mwizi akiongeza mbio chizi nae huyo, mwishowe mwizi akasalimu amri na kusimama, yule chizi akamsogelea na kumwambia.. Daah umesahau remote hii hapa mwizi kafleti.
Chemsha bongo
Baba akimuuliza chemsha bongo mwanae anayesoma shule ya chekechea “haya niambie kitu gani hakiwezi kuliwa wakati wa breakfast?” Mtoto akajibu “hiyo mbona rahisi baba, si lunch na dinner”
Recent Comments