SMS Nzuri: Meseji za Vituko Vya Kushangaza

Jamaa mpenda michepuko kapatikana

…Upo kazini umeacha familia yako nyumbani mara ghafla unapigiwa simu kutazama unakutana na no ngeni na kuamua kuipokea ndipo unakutana na Sauti ya msichana ya kuvutia lakin kabla hajasema shida yake anaamua kukata simu. Unashikwa na hamu ya kujua ni nani. Tamaa ya mchepuko inakujia ghafla na kuamua kuipiga ile no tena kwa mara nyingine inakuwa haipatikani.

Siku hiyo hiyo usiku ukiwa umelala chumba kimoja na mkeo meseji inaingia tena kwenye cm yako kwa ile namba iliyokupigia mchana ikikuomba umpigie kwa mida ule na kusisitiza kuwa ana hamu ya kukufahamu. kila ukimtumia meseji ya kumdanganya upo sehemu mbaya hasikii anakubipu mara nyingi. Uzalendo unakushinda, unamuangalia pembeni mkeo kalala fofofo kajifunika shuka hadi usoni. Unaamua kuondoka kwa kunyata mpaka sebuleni kwenda kuipiga Ile namba kwa lengo la Kumwambia kesho mkutane. Ile unafika sebuleni na kuanza kuipiga ile cm ndipo unakutana na sauti hii:- MUME WANGU ACHA MCHEPUKO, NILIKUWA NAKUPIMA TU RUDI TU CHUMBANI TULALE 😋😋😋😋😋😋😋😋 Hapo ndo utajua kwann bata hata ale kokoto anaharisha 😂😂😂😂😂😂😂😂

Kichekesho cha mwalimu na wanafunzi

Mtoto: Mwalimu mimi nataka nisome darasa la nne kwani hili la3 halinifai.

Mwalimu: Kwa nini unasema hivyo?

Mtoto: Nina akili…

Basi mwalimu akamueleza mkuu wa shule na mkuu kaitisha interview kwa dogo. Maswali ni haya….

Mwalimu: Kwenye ndege kuna matofali 20 tukitoa moja tukalidondosha chini yatabaki mangapi?

Dogo: Yatabaki 19.

Mwalimu: Nipe hatua za kumuweka tembo kwenye friji.

Dogo: Unafungua friji unamuweka tembo kisha unafunga.

Mwalimu: Nipe hatua za kumuweka nyani kwenye friji.

Dogo: Unafungua friji unamtoa tembo ulemuweka..unamueka nyani kisha unafunga friji.

Mwalimu: Kuna sherehe ya siku ya kuzaliwa kwa simba, wanyama wote wameenda kasoro mmoja. Ni nani na kwa nini?

Dogo: Ni nyani kwa sababu tumemuweka kwenye friji.

Mwalimu: Bibi kizee amevuka mto unaokuwaga na mamba na viboko wakali, aliwezaje?

Dogo: Aliweza kwani mamba na viboko nao walienda kwenye sherehe ya kuzaliwa kwa simba.

Mwalimu: Ingawa bibi kizee alivuka mto, baadae alikufa. Unadhani ni kwanini alikufa?

Dogo: Alidondokewa na lile tofali tulotoa kwenye ndege na kutupa chini.

Mwalimu mkuu: Huyu dogo akasome chuo kikuu….
😆😆😆😆😆😆😆😆

Kilichotokea baada ya kichaa kumfumania mke wake na mwanamme mwingine

Jay akaruhusiwa kwenda nyumbani kutoka hospital ya Vichaa, akapakiwa ktk ambulance hadi karibu na nyumbani kwake, akaulizwa unapakumbuka? akajibu ndio nyumba yangu ileee, mara wakatoka watoto wawili wamevaa uniform akasema watoto wangu walee wanakwenda shule.. akatoka mwanamke akasema na mke wangu yulee, ghafla akatoka mwanaume Jay akasema na mimi yule naenda kazini. hivi Jay kweli kapona?

Shopping Cart
🏠 Home 📖 Reading 🖼️ Gallery 💬 AI Chat 📘 About