SMS Nzuri: Meseji za Vituko Vya Kukupa Mood Mpya

Cheki kilichonipata sasa, ungekua wewe ungefanyaje?

Siku moja katika pitapita zangu nikakutana na mtoto mmoja mkali balaa yaani ni mzuri sanaaaa, moyo ukanituma nimuimbishe mtoto akakubali kwamba nitafute siku tukae tuongee vizuri akasema nimpe namba yangu ya simu.

 

Ebwana si akatoa simu hiyo inauzwa laki sita mimi hapa nina kisimu cha tochi tena nimefunga na rababendi
Je, wewe ungeendelea kumtajia namba zako!!!

Mzee wa kichaga na hela zake. Angalia anachofanya

Mzee moja alikuwa kila usiku anapita mbele ya bank anasimama,kisha anapiga honi,akitoka askari mlinzi,anaondoka.Hilo jambo likamkera sana askari mlinzi, askari akawa na mvizia yule mzee wa kichaga ,siku alipokuja tena akamkamata, akamuuliza kwa nini unakuja unapiga honi kisha unakimbia? Mzee akasema: Haki ya mungu babaangu , Nina pesa zangu ktk account hapa bank naogopa usilale usingizi ndo maana kila siku usiku napita kukuangalia kama umelala!!
😂😂😂😂😂😂

Cheki hawa wachungaji

CHEKA KIDOGO

Wachungaji watatu walikutana kwa siri na kuelezana matatizo yao ili waweze kuombeana.

MCHUNGAJI WA KWANZA: mimi tatizo langu ni wizi, kila nikimaliza ibada lazima niibe pesa za sadaka.

WA PILI: Mimi tatizo langu ni wanawake yani nimeshalala na wana kwaya wote pamoja na mke wa ASKOF.

WA TATU akaanza kulia badala ya kuongea.WENZAKE:

We vp unatatizo gani mbona unalia???

AKAJIBU: jamani mimi tatizo langu ni “umbea” haya yote tuliyoongea lazima nikaseme!

😂😂😂😂😂👆🏻😂😂

Tofauti ya ukopaji wa mzungu na mswahili

MZUNGU: Hi, I need $100, will pay back on Monday

MSWAHILI: Kaka vipi, shwari? Dah.. hatuonani mzee, mishe vipi, mnatunyima nini? Juzi nimekuona kwa mbaaali… mzee shavu dodo, full kipupwe! Sie tupo bwana, shida tu, afu misiba mingi tu, wife nae kajifungua ghafla. Sasa, kuna cheque naisubiri haijatoka hadi leo, wanasema itatoka next week, hapa nimekwama kweli. Naweza pata ‘Laki Moja’ ya karibu hapo nitarudisha mwisho wa mwezi…?😂😂😂😂😂

Kapresha kakiamua kuja kanakujaga tuu, cheki kilichompata huyu mme wa mtu mpenda michepuko

Kimchepuko chako kinakuandikia meseji kama hii…

…Samahani baby kama unavyojua nimeokoka ,nimetubu kanisani lakini nabii kaniambia niwaombe msamaha wote niliowakosea.

Nimemkosea sana mkeo kwa kumwibia mumewe na nimepanga kuja kumwomba msamaha kesho ntakuja na nabii na Mchumba wangu mpya nilie mpata kanisani.

Samahani kwa usumbufu uliojitokeza lakini hilo ni kwa ajili ya utukufu wa bwana!!!

Wako Manka wa Magorofani😅😅

Shopping Cart
🏠 Home 📖 Reading 🖼️ Gallery 💬 AI Chat 📘 About