SMS Nzuri: Meseji za Vituko Vya Jumapili
Angalia alichojibu huyu mwanafunzi, Ungekua wewe ni mwalimu wake ungemfanyaje?
Mwanafunz alikuwa kila siku anachelewa shule, na kila siku alikuwa anachapwa, basi siku moja mwalimu akaona ngoja amuulize.
Mwalimu: Mbona unachelewa kila siku?
Mwanafunzi: Nakaa mbali mwalimu
Mwalimu: (huku ana hasira akauliza)Mbali mbinguni?
Mwanafunzi: Mbinguni kwa mbeleπππππ
Cheki kilichotokea stesheni ya treni, mambo mengine ukipaniki inakula kwako kama huyu jamaa
Jamaa Wawili Walifika Stesheni, wakakuta Treni ndo kwanza inaondoka. Wakaanza Kuikimbiza. Mmoja akafanikiwa kupanda akaondokaβ¦
Yule aliyebaki akaanza kucheka sanaa mpaka machozi yakamtoka. Watu wakamuullza, unacheka nini sasa wakati umeachwa? Akawajibu: “kinachonichekesha, yule aliyepanda alikuwa ananisindikiza.
Angalia ndoto nyingine zilivyo na Majanga
Ndoto zingine bwana usiombe zikupate
Mimi usiku wa kuamkia Leo nikiwa nimelala nimeota naendesha gari Yangu aina ya BMW mpya Mara gafla ikakwama kwenye tope .hivyo ikabidi nishuke ili kuisukuma loh! Yani kudadeki ile kuamka nikakuta nimesukuma kitanda hadi sebleni Daaa ilinisikitisha sana jiangalie sana sese hivi ndio narudisha kitanda chumbani .angalizo angalia ndoto unazo ota unaweza kuota upo baharini ukaamka unajikukuta unaogelea kwenye Jaba la Maji shauri yako.
Nilichomfanyia huyu aliyenizingua nilipomuazimisha pasi
ππππππ
Jana nimeenda kuazima pasi chumba jirani, ili ninyooshe nguo zangu, Jamaa wakaniambia nichukue nguo nikanyooshe room kwao maana hawataki pasi yao itoke.
Sasa leo amekuja mmoja wao kuazima mopper akasafishe room, nimemwambia aje adekie humu humuβ¦
Jamaa ameondoka nadhani atakua ameenda kuchukua maji
π€π€π€
Angalia kilichomkuta huyu msanii wa mziki na mashabiki wake
Msanii mmoja anaitwa ”KINYA” alikuwa ana perfom jukwaan..!!!
Kawaida kila msanii lazima ajitambulishe, mfano:-
”YEAH NI TEMBA hapa au
YEAH NI CHEGE hapaβ¦!!!
Yeye akasema: “YEAH NIKINYA HAPAβ¦!!!”
Watu wakapiga kelele ”UTAZOAAA” mwenyewe bwenge wee
JE, WEWE UNGEJITAMBULISHAJE NAITAJI JIBU LAKO TUONEβ₯
Lugha za namba ni noma
Leo kuna mdogo wangu nimemtumia meseji nimemuomba aniazime chaja yake ya simu. AkanijibuΒ 21002Β Nikawa mkali nikamuambia kuchajia mara moja tu ndio HELA yote hio si bora nikanunue Chaja yangu mpya. Akaniambia nimesema TUMIA TU ππmtatuua na lugha zenuπ
BREAKING NEWS: WAZIRI ANASWA KOFI
Mkazi wa Mbagala Kibondemaji, Waziri Salum (23) amejikuta akinaswa makofi baada ya kupishana kauli na jirani yake.
Punguzeni pombe. Cheki kilichompata huyu
Jamani punguzeni pombe,kuna jirani yangu amerudi amelewa sasa nachungulia dirishani naona anagonga mlango wake takribani masaa mawili,wakati hapa anaishi peke yake, kwakuwa sipendagi ujinga nimetoka nikamwambia mwenyewe kasafiri.Nae kaondoka.
Angalia alichokifanya huyu mtu baada ya kuokota wallet ya thamani
Jamaa aliokota wallet, alipofika nyumbani akapiga simu kwenye radio station “naitwa Juma nimepiga simu kutangaza kuwa nimeokota wallet ndani ina laki7, ATM card na karatasi yenye PIN ya ATM card na kijimfuko cha dhahabu” Mtangazaji akasema, kwa hiyo ungependa kumrudishia mwenyewe kama anakusikiliza? Jamaa akajibu; hapana, ninaomba kumuombea dedication wimbo wa R.Kelly usemao “U SAVED ME” umfikie popote alipo!!
Baada ya mwanamke kukataa kufungua mlango angalia kilichomkuta
MUME: Fungua mlango!
MKE: Leo sifungui! Nimechoshwa na ulevi wako.
MUME: kama hufungui najitupa kwenye hili shimo nife kabisa.
MKE. Kufa huna faida yoyote duniani!
MUMEΒ kachukua jiwe kubwa kalitupa kwenye shimo chubwiiiiiii!
MKE kajifunga kanga, kafungua mlango. Ghafla mume kaingia ndani na kumfungia mke nje.
MKE: Nifungulie la sivyo nitapiga kelele majirani waje.
MUME: Piga kelele na wakija uwambie unakotoka usiku huu na khanga moja.
Soma alichokisema mlevi baada ya kukuta watu wakimpiga mwizi
Mlevi mmoja aliona wananchi wakipiga mwizi akawaambia “mwacheni msimpige, hii tabia yenu ya kupiga wezi mtakuja shtukia mnampiga Yesu, maana imeandikwa atakuja kama mwizi!”
BREAKING NEWS!!! Nyoka wa ajabu agundulika
HABARI MPASUKO..
jana katika taasisi ya wanyama pori ya Nat Geo ilitangazwa kuwa ametokea Nyoka hatar san Ambaye hajawah kutokea duniania.. wanadai kwamba nyoka huyo anaongezeka ulrefu wa 0.5sm kila akila chakula na huwa anakula chakula kuanzia sekunde 30 kurudi nyuma.. mpaka sasa hakuna siraha ya kuweza kumuua nyoka huyo isipokuwa akiji uma mwenye ndo anaweza kufa, wanasayansi hao walieleza japo uchunguz zaid bado unaendelea⦠huyu ni nyoka anayeua kuliko nyoka wote waliowah kutokea katika historia ya maisha ya mwanadam..
nyoka huyu hupatikana katika simu pekee za nokia toch katika sehem ya game inaitwa snake xenzia..
asanteni kwa kufurah na umakin mkubwa katika usomaji wa matini hiiβ¦
haya ni mambo ya wikiend jaman na iwe njema kwenu wote
Eti kwani wewe ni turubali?
Unakuta MTU mwaka Mzima
Umehudhuria,Β birthday parties 20 ,Β misiba 30,
Mikutano kanisani 40, Ndoa 80 na bado uko Single Kwani wewe ni turubai jaman??
πππππππππππ
Cheki huyu kiherehere alivyojibiwa
Za asubuhi?
Nzur sjui huko?
Huku kwema tuu
VP si ulimaliza chuo ww?
Ndio kwani vp?
Mbona hatuoni matunda yake?
Kwani mi nlienda na miche ya mipapai au miembe au umeambiwa TIA, IFM na IAA wanakodisha Mashamba ya nyanya ????????
Hamna sio hvyo umeenda mbali kaka
Kama kilomita ngapi?
Haya yaishe bhanaβ¦
Ukome kwa kiherehere
Nitukane tuu unakumbuka kuna SKU nlkupa buku ya nauli?
Nitajie namba yako ya tgo pesa nkuwekee hyo buku
Kwani mi nimesema unilipe
Utajua mwenyewe ila nakutumia kwenye namba uliyonitext wee si umefanya ujinga mi nafanya upumbavu
Simple lyke dat Viherehere huwa tunawajbu HVOβ¦β¦ππππππππππππππππππππππππππ
Huyu mlinzi bwana
High school Flashback!!
.
Watchman : Amkeni muende morning preps.
Allan : Mimi ni mgonjwa.
Watchman : Unaumwa na nini hiyo?
Allan : Bionomial Nomenclature.
Watchman : Eeh, lala tu kijana. Hiyo kitu ni
mbaya. Imeuwa watu South Africa.
ππππππππππ
#_Sipendagii ujinga kabisaa mimi
Kilichompata sista duu bishoo wakati akijidai kununua pete
Mwanamke mmoja aliingia duka la vito vya thamani, akaona pete moja ya dhahabu nzuri sana amabayo ilikuwa kwenye shelf ya chini, wakati anainama apate kuitazama vizuri kwa bahati mbaya (au nzuri!), shuzi likamtoka- druuuuuu, soni ikamuingia huku akigeuka haraka kuangalia kama kuna yeyote dukani pale ameliskia shuzi lake, macho yakagongana na mwenye duka ambaye alikuwa karibu huku uso ukiwa umejaa tabasamu zito, mwana mama hakuwa na uhakika kama amesikika au hakusikika, akaona atumie nafasi ile kuyeyushaβ¦Akauliza “Hii pete bei gani?” . Jamaa mwenye duka, huku akiangua kicheko, akajibu “Umeiona tu umejamba, je nikikuambia bei yake si utakunya kabisa?”
Huku ndiko kuumbuka bila chuki
Umeenda kutembea ukweni kwako baada ya chakula chausiku unapewa chumba chakulala inapofika usiku unatakakutoka kwenda kujisaidi kwasababu taa zimezimwa unapamia vyombo vya chakula sebleni kipindi unajalibu kupapasa uviweke sawa mala taa inawashwa na mama mkwe anaona umeshika vyombo anakwambia, baba kama ukushiba ungesema
Recent Comments