SMS Nzuri: Meseji za Visa Vya Wikiendi
Angalia huyu mtoto anachomjibu baba yake baada ya kutoka kwenye mtihani
BABA: mwanangu kwenye huu mtihani uliofanya natumaini utafanya vizuri.
DOGO: ndio baba nitapata mia kwa mia.
BABA: kwanini unasema hivyo?.
DOGO: kwasababu jana kanisani tulifundishwa “Yesu ni jibu” kwahiyo kote nimejaza Yesu.
BABA: kwel kazi ipo
JE UNGEKUWA WEWE HUYO NDO MWANAO UNGEMFANYAJE?
Kilichotokea wakati mchungaji akifungisha ndoa ya Mashoga
Mchungaji mmoja baada ya kuwafungisha ndoa “MASHOGA” wawili alipata wakati mgumu kutamka kuwa “sasa ninyi ni MKE na MUME”
atafanyaje wakati wote ni wanaume? mchungaji akapiga moyo konde na kusema “tangu sasa ninyi ni MAN UNITED”
Angalia alichokifanya huyu mtu baada ya kuokota wallet ya thamani
Jamaa aliokota wallet, alipofika nyumbani akapiga simu kwenye radio station “naitwa Juma nimepiga simu kutangaza kuwa nimeokota wallet ndani ina laki7, ATM card na karatasi yenye PIN ya ATM card na kijimfuko cha dhahabu” Mtangazaji akasema, kwa hiyo ungependa kumrudishia mwenyewe kama anakusikiliza? Jamaa akajibu; hapana, ninaomba kumuombea dedication wimbo wa R.Kelly usemao “U SAVED ME” umfikie popote alipo!!
Wanandoa wa Kijapani wakibishana
*Wanandoa wa Kijapan wakiwa wanabishana hadharani*
*Husband: Takamushi jiku.*
*Wife :hashi jiku mishihe*
*Husband: inamoto kushini hat a pi*
*Wife: jejeta takuna mota shinita*
*Husband: kituya sitina kutara*.
*Wife: totori yatika miniya*
_Uko busy kusoma utadhani unaelewa kijapan kuwaga serious saa zingine_
๐๐๐๐๐๐
Cheka kidogo: Majibu ya mhindi kwenye mtihani wa Kiswahili alipoambiwa ajibu methali
Mhindi kwenye mtihani wa kiswahili anaambiwa amalizie methali:
(a)Nyani haoniโฆ..valisa miwani!
(B)Debe tupuโฆ.weka dengu!
(c)Masikini akipataโฆ.iko acha iba!
(d)Penye kuku wengiโฆchinja bili,tatu!
(e)Asiyesikia la mkuuuโฆ.peleka yeye polisi!
(f)Penye wengiโฆโฆiko kutano ya chadema!
Angalia huyu polisi kitu alichonijibu
Nimefika hapa Polisi Station nimefarijika sana na Kustuka baada ya kumkuta Askari hapa Kaunta anasoma Biblia nikajisikia fahari kuona anasoma neno kituo cha Polisi. Nikamuukiza Afande ni Nani alimuua Goliathi? Akasema Muulize Afande Mwita mlango namba 2 ndo anausika na Kesi za Mauaji.๐๐
Mkwe kazua mpya, Hii dunia ina mambo sana
Mama mkwe alimuuliza mkwewe “binti” samahani mbona mtoto hajafanana na mwanangu kabisa?
Binti akajibu, “bila samahani mama huku chini nina njia ya uzazi sio mashine ya photocopy”
mama mkwe hoii!! Chezea Wakwe Wa Bongo wewe.
Januari kweli ngumu, soma hii
Januari kweli kiboko
Hii january sabuni za kuogea ni zile za kuoshea vyombo, yani unakutana mjini na mtu ana mchicha shingoniโฆ๐
Wanawake hii nayo ni romantic ?๐
Alaf wale Madem wanaowavua maboy wao KOFIA alaf wanakimbia nayo thinking its FUNNY and ROMANTIC.. Hiv nyie mkivuliwa MAWIGI wakakimbia nayo mtajiskiaje?๐ธ๐ธ
Utani wa wahindi, cheka kidogo
Mhindi afaulu mtihani wa Kiswahili
(1) Mfa maji ?โฆโฆโฆโฆโฆโฆ.. Tampa life jacket.
(2) Mwenda pole?โฆโฆโฆโฆ Tachelewa fika.
(3) Usipoziba ufa ?โฆโฆโฆ.. Mizi taona mpaka dani.
(4) Usilolijua ?โฆโฆโฆโฆโฆโฆ Uliza google.
(5) Mbio za utelezini ?โฆโฆ. Chafua guo yako.
(6) Ukipenda boga ?โฆโฆโฆ Ngoja mezi ya ramzani tapata.
(7) Ukiona vinaelea ?โฆโฆ.. iko nyepesi hiyo.
(8) Maji yakimwagika ?โฆโฆ Mambie dada tapiga deki.
(9) Chelewa chelewa ?โฆโฆโฆ Takosa guo ya sikukuuโฆ
(10) Kila ndege ?โฆโฆโฆโฆ.. โฆHutua Airport
(11) Bandu bandu ?โฆ.. โฆโฆ.Rafiki yake Jecha
(12) Mtaka cha Mvunguni ?โฆ Ondoa tanda
(13) Simba mwenda kimya?โฆ.Kama sio gonjwa basi haina njaa.
(14) Aisifuye mvua ?โฆโฆโฆ. Najua iko Mkulima hiyo
(15) Barabara ndefu ?โฆโฆ.. Ongeza mwendo au tachelewa fika.
(16) Mlanawe hafi nawe ila?โฆ. Takimbia
(17) Asie sikia la mkuu ? โฆโฆ.. Tapeleka jela
(18) Hasira za mkizi ? โฆโฆโฆโฆ..Tatafuna veve
(19) Mchamba wima ?โฆโฆ.. Karibu ya Hurumzi
(20) Akumurikae mchana ?โฆ.Kipofu hiyo
(21) Mficha maradhi ?โฆโฆ.. Taenda Loliondo
(22) Mkataa wingi ? โฆโฆโฆ.Taenda Chadema
(23) Bendera ?โฆโฆโฆโฆโฆ. Kama sio ya CCM, ya CUF
(24) Baniani mbaya ?โฆโฆ. Peleka Bombay Lakini sio HB kweli, naonea tu
(25) Akili nyingi ?โฆโฆโฆ. Tapasi mtihani yote
(26) Penye kuku wengi ? โฆโฆ.. Chija bili tatu ivi, hapana mtu najua.
Cha kufanya msichana akikukimbia halafu atake kukurudia
โฆโฆโฆ Kama msichana atakutupa kwa sababu huna pesa, na baadaye unapopata pesa akarudi tena kuomba msamahaโฆ Ndugu yanguโฆ.. Msameheโฆ. Mpe ahadi ya ndoa, mwambie utamuoaโฆ. iambie familia yake unataka kufanya ukarabati wa nyumba yaoโฆโฆ Ondoa paa lote la nyumba yao halafu TOWEKAโฆ..
๐โฆโฆโฆ ๐โฆโฆ.. ๐
Biashara ambayo imefeli
*TEACHER*: _nielezee biashara ambayo imefeli kutokana na uzembe
*STUDENT*: Changudoa akipata mimbaโฆ
*TEACHER*: _get Out!!!!!!!!!!!!!!_
๐๐
Punguzeni pombe. Cheki kilichompata huyu
Jamani punguzeni pombe,kuna jirani yangu amerudi amelewa sasa nachungulia dirishani naona anagonga mlango wake takribani masaa mawili,wakati hapa anaishi peke yake, kwakuwa sipendagi ujinga nimetoka nikamwambia mwenyewe kasafiri.Nae kaondoka.
Huyu jamaa kawaweza polisi watatu, cheki alichowaambia
Polisi::: hodi, hodi
Jamaa::: kimya
Polisi::: hodi, hodi
Jamaa::: we nani kwani?
Polisi::: sisi polisi
Jamaa::: mnataka nini?
Polisi::: kuongea na wewe
Jamaa::: kuongea na mimi?!
Polisi::: ndio
Jamaa::: mko wangapi?
Polisi::: tuko watatu
Jamaa::: kama mko watatu si muongee wenyeweโฆ!!!
Eti wanadamu walikuja vipi duniani
Mtoto wa miaka sita alimuuliza babake:
MTOTO: Baa, eti sisi wanadamu tulikuja vipi
duniani?
BABA: Mungu alimuumba Nabii Adam na Hawa.
Kisha wao wakaanza kuzaa watoto na watoto
wakazaa mpaka tukazaliwa sisi. (Mtoto hakuridhika
akamfuta mamake)
MTOTO: Mma, eti sisi wanadamu tulikuja vipi
duniani?
MAMA: Wanasayansi wamesema sisi tulitokana na
manyani baadae tukawa binadamu. (Mtoto akarudi
kwa baba)
MTOTO: Baa mbona mama ansema sisi tulikuwa
manyani mwanzo?Au wanidanganya?
BABA: Mwanangu, mimi nimekuelezea kuhusu ukoo
wetu. Mamako amekuelezea kuhusu ukoo wao๐๐๐ถ๐ผ๐ถ๐ผ๐ถ๐ผ
Cheki tabia za kuandika vimaneno vya ajabuajabu kwenye pikipiki na bodaboda ilivyomponza huyu
Jamaa mmoja dereva wa bajaji alianguka, sasa bajaji ikawa imem’bana akawa anafurukuta bila mafanikio Cha ajabu watu wakawa wanampita bila kumsaidia, Kumbe Nyuma ya Bajaji yake alikua Kaandika “NIACHENI KAMA NILIVYO, HII NDIO STYLE YANGU”ย ๐๐๐ย Mpaka sasa nimemwacha bado yuko hapoย *Sipendagi Ujinga mimi* ๐ถ๐ฝ๐ถ๐ฝ๐ถ๐ฝ๐ถ๐ฝ๐ถ๐ฝ
Utani kwa wadada wembamba
๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐
Wadada wembamba hebu nenepeni basi mnatupa tabu kusoma maneno ya kwenye kanga jamanii โฆโฆโฆmnaviringisha kanga mwili mara 3 mpaka maandishii hayaonekanii
๐คฃ๐คฃ๐คฃ๐คฃ
Kilichonitokea leo baada ya kuona nungunungu
Baada ya kukaa mda mlefu sijamuona nungu’nungu leo nikakuna nae nikajisikia furaha sana,
nikaona bora niende nikamkumbatie !! kutokana na kukaa cku nyingi sijamuona!
Dah! Alichonifanyia nung nung sitokisahau !!!
Recent Comments