Biashara ambayo imefeli
*TEACHER*: _nielezee biashara ambayo imefeli kutokana na uzembe
*STUDENT*: Changudoa akipata mimbaβ¦
*TEACHER*: _get Out!!!!!!!!!!!!!!_
ππ
*TEACHER*: _nielezee biashara ambayo imefeli kutokana na uzembe
*STUDENT*: Changudoa akipata mimbaβ¦
*TEACHER*: _get Out!!!!!!!!!!!!!!_
ππ
.
.
Soma vichekesho hivi;
Jamaa aliibiwa kadi yake ya benk akaulizwa kama ameripoti polisi akajibu “sijaripoti bado, mwizi mwenyewe hamfikii matumizi kama mke wangu.
Njia rahisi kusahau matatizo yako (japo kwa muda mfupi) vaa viatu vinavyokubana.
Tulikuwa bar moja jana mlinzi kaingia spidi, akamwambia jamaa mmoja aliyekaa kaunta, Mlinzi: Mzee gari lako limeibiwa Mzee: Umemtambua aliyeiba? Mlinzi: Hapana lakini nimeandika namba za gari hizi hapa.
Jamaa alikuwa anapita nje ya wodi ya vichaa akasikia mtu anasema, 13, 13, 13, 13, 13, 13,β¦.. akaamua kuchungulia kwenye kitundu alichokiona ajue kuna nini, ile kuchungulia tu akamwagiwa mchanga wa machoni, sauti ikabadili ikaanza 14,14,14,14,14β¦β¦
Jamaa alikuwa anaumwa sana, mkewe akamwita daktari, alipofika akamkuta jamaa kafumba macho;
Dokta: Huyu mbona amekwisha kufa?
Jamaa: Sijafa bwana
Mke: Hebu nyamaza bwana acha kubishana na wataalamu.
Dokta alipotembelea wodi ya mgonjwa wake aliyepata ajali. Mgonjwa akiwa amening’inizwa mikono juu akauliza “dokta ntaweza kweli kupiga kinanda nkitoka hospitali?”
Dokta: Bila shaka utaweza, wewe ni mpiga kinanda mzuri enh?
Mgonjwa: Hapana sijawahi kabisa bado.
Mwanaume alimnunulia pete ya almasi mkewe, rafiki akauliza “si ulisema anapenda gari yenye four wheel drive, mbona umenunua pete?” Mume akajibu “unadhani wapi ntapata rav4 feki?”
Trafiki polisi akihoji palipotokea ajali “ahaa! Sasa naanza elewa embu nielezee jinsi ajali ilivyotokea wewe ukiwa kama dereva mhusika.” Dereva akajibu “hata sikumbuki nlifumba macho”
Polisi alimdaka jamaa anakojoa pembezoni mwa ukuta.
Polisi: Wewe unajua panakatazwa kukojoa hapa?
Jamaa: Sasa nimebanwa nifanyaje?
Polisi: Faini yake elfu tano.
Jamaa akatoa noti ya elfu 10.
Polisi: Sasa chenji tunaipataje?
Jamaa: Tafuta chenji unipe changu.
Polisi: Basi kojoa tenaβ¦
Jamaa kaamka asubuhi sana Jumamosi, mvua inanyesha kang’ang’ania kuwa anaenda ofisini. Kawasha gari yake, kufika njiani hali ilikuwa mbaya kaamua kurudi. Kafika home kavua nguo kaingia tena kitandani, kamnong’oneza mkewe aliyekuwa usingizini; “Yaani hali ya hewa huko nje mbaya sana” Mke: Si ndio nimemshangaa huyu mpumbavu eti kaenda kaziniβ¦
Baba na mtoto:
Baba: Mwanangu ukiwa na hasira unafanya nini?
Mtoto: Naenda chooni.
Baba: Chooni? Kufanya nini?
Mtoto: Kusafisha.
Baba: Halafu ndio hasira zinaisha?
Mtoto: Ndio. Nasafisha choo kwa mswaki wako.
Mgonjwa: Dokta nimekuja nahisi ninaumwa Malaria na kifua.
Dokta: Sasa ushajua unaumwa nini hapa umefuata nini kwangu?
Mgonjwa: Sasa si nimekuja kwa dokta.
Dokta: Wanaojua kuwa wanaumwa kama wewe wanapitiliza maabara.
Bachela mmoja aliyekua akiishi kwa muda mrefu peke yake kwenye nyumba aliyopanga siku moja alitaka kupika pilau kwa mara ya kwanza. Sasa asijue nini kinachobadilisha rangi ya wali kuwa rangi ya brown, yeye akapika kama kawaida (wali) kisha wakati wa kula akavaa miwani yenye rangi ambayo ukiuangalia wali unauona kama pilau wakati anakula.
Mwizi kaiba TV na kuanza kukimbia nayo, kumbe ile nyumba mlikuwa na chizi, akaanza kumkimbiza yule mwizi. Kila mwizi akiongeza mbio chizi nae huyo, mwishowe mwizi akasalimu amri na kusimama, yule chizi akamsogelea na kumwambia.. Daah umesahau remote hii hapa mwizi kafleti.
Baba akimuuliza chemsha bongo mwanae anayesoma shule ya chekechea “haya niambie kitu gani hakiwezi kuliwa wakati wa breakfast?” Mtoto akajibu “hiyo mbona rahisi baba, si lunch na dinner”
Misemo ya kina dada
walianza na halohalooo!
Wakaja unalo babu weee!
Ikafuata utajijuuu!
Ikafupishwa utajiJJ!
Mara ghafla kantangazeee!
Haikukaa sana kansajiriii!
Ikatoka nyingine nishiiiiida!
Unaijua iliyotoka Leo?
Heh! Heh! Heeeh! MB zenyewe 8 nikudownload unanini?
Kuishi kijijini kunahitaji moyo sana
..unaenda kuoga, unakumbuka kuwa umesahau sabuniβ¦unaenda kuchukua sabuni kurudi bafuni, unakuta ng’ombe amekunywa maji yote..unaamua kufuata mengne,unarudi unakuta mbuzi kala sabuniβ¦ππππ
Kuna mtoto wa jirani ananibore sana kila nkimtuma kitu dukani lazima aonje,
Jana nlimtuma sukari akala yote..Β
Sahii nmemtuma superglue haongeiΒ Sipendi ujinga mimiΒ
π‘π‘π‘π‘π‘π‘
Jamaa alikuwa amelaa na mkewe saa tisa ya usiku akastuka baada ya kusikia mtu anabisha hodi kwenda kufungua mlango
Akamkuta jamaa kalewa sana mlangoni kwao
JAMAA: Nini tena mheshimiwa kuamshana saa hizi?
MLEVI: Naomba uje unisukume.
Jamaa akiamini kuwa pengine kuna gari la huyu mlevi limezima jirani akamwambia subiri nikavae viatu. Baada ya kuvaa viatu akatoka na wakaanza kusindikizana na mlevi. Mlevi akaongoza njia
mpaka kwenye mabembea ya jirani akakaa kwenye bembea moja na kumgeukia jamaa na kumwambia.. Okay nisukume basi.
ππππππ
Boss;-Β kwa nini umechelewa kazini
Juma;-Β kuna mtu njiani alidondosha elfu1
Boss;-Β ohhoh kwa hiyo ulikuwaunamsaidia kuitafuta
Juma;-Β hapana nilikuwa nimeikanyaga
ππππππππππππππ
Jamaa alikuwa na tabia ya kutembea na binamu yakeβ¦.
Alikuwa anasubiri mjomba na mkewe walale tu halafu ananyata mdogo mdogo mpaka chumbani kwa binamu yake.
Siku moja umeme ulikuwa umekatika ikabidi aamue kuvua nguo kabisachumbani kwakeβ¦.
Akanyata taratibua akafungua mlango akazama chumbani kwa mjomba ake bila kujua, ghafla umeme ukarudiβ¦
MJOMBA; we mshenzi umefata nini chumbani kwangu tena uko uchi
JAMAA; nimekuja kukuaga kesho naondoka
MJOMBA; ndo uje uchi?
JAMAA; ndio kwasababu nimeshapaki kila kitu kwenye begi
ππππππππππππ
FUNDISHO : SAFARI NI SAFARI
Maisha ni ya ajabu sana, wakati mwingine maisha ni mazuri na mwingine ni mabaya, katika maisha yetu tumeshapitia safari nyingi sana na za aina mbalimbali kwa nyakati mbalimbali. Lakin kiukweli kila safari ni safari tuu.
Japokua kila safari ina changamoto zake lakini mwisho wake ni ule ule , kila safari ina uzuri na upekee wake.
Vile vile kila safari ina ubaya wake, kwa mfano kila safari ina gharama yake kulingana na upekee wake.
Usiwe na wasiwasi na mashaka na aina ya safari ulionayo, jipe moyo utaimaliza na kupata ulichokitarajia. Haya ndio maisha na wote tunatakiwa tuyafurahie.
Ingawa kila mtu ana safari yake bado wote tunatakiwa tufurahie pamoja kwa safari tuliyo nayo. Hata Uwe Na safar ya aina gani wewe furahi tuu. Hii ni kwa sababu safari mwisho wake ni mmoja kwa wote burudani ni ile ile
SafariπΊ ni safari πΊhata kama ni ya chupa au ya kopo mwisho wake π€π€
ππππππ
Ulijua ni nn??
Msanii mmoja anaitwa ”KINYA” alikuwa ana perfom jukwaan..!!!
Kawaida kila msanii lazima ajitambulishe, mfano:-
”YEAH NI TEMBA hapa au
YEAH NI CHEGE hapaβ¦!!!
Yeye akasema: “YEAH NIKINYA HAPAβ¦!!!”
Watu wakapiga kelele ”UTAZOAAA” mwenyewe bwenge wee
JE, WEWE UNGEJITAMBULISHAJE NAITAJI JIBU LAKO TUONEβ₯
Eti kuna mkaka alitembelewa na mama yake mzazi. Wakiwa sebuleni yeye, mama na mke wake, mke wake akaanza kuonekana tofauti kama vile anajiskia vibaya. Akaenda chumbani. Baada ya muda mfupi yule mkaka akamfuata. Wakakaa sana huko kisha mkaka akarudi sebuleni kuendelea kuongea na mama yake. Lakini zipu ya suruali yake ilikuwa wazi. Mama akamuuliza, mkeo anaendeleaje? Akamuambia, anajisikia vzr sasa. Nimempa panadol. Mama akatabasamu na kumwambia mwanaye, sawa. Lakini siku nyingine ukishatoa panadol ukumbuke kufunga pharmacyππ
Pale unapo gundua kuwa yule ulie mtukana kwenye bajaji ndio boss anaeenda kukufanyia interviewπ₯π₯π₯π
My freand apo ndo utagundua kwaanini wimbo wa Taifa tokea 1961 ni audio aujatolewa video
ππππππππ
(KIFO NI NIN)
KIFO ni pale unapokosea text na kumtumia
BABA yako kipindi mnakula
“hello Mrembo”ππ
Kama utazubutu kusema Samahani π
Dokta: Mama tumemchunguza mumeo kwa makini sana, jopo lote la madaktari tumekubaliana mumeo anahitaji mapumziko japo ya mwezi. Sasa tafadhali chukua hivi vidonge vya usingizi vitasaidia sana.
Mama: Asanteni sana, sasa niwe nampa mara ngapi?
Dokta: Unatakiwa wewe uwe unakunywa vidonge hivi kutwa mara tatu kwa mwezi mzima, mumeo atapona.
Recent Comments