SMS Nzuri: Meseji za Visa Vya Kisasa
Muda ambao unaweza kumzoea dingi
Muda pekee ambao unaweza kumzoea DINGI ni pale unapomfundisha kutumia SMARTPHONEβ¦.
Wanakuwaga wapole sana aisee unaweza hata kumuagiza maji ya kunywa akakuleteaβ¦.
πππππππ
Cheki huyu jamaa alivyoumbuka akiwa ndani ya dala dala baada ya kupokea simu ya mkewe
Jamaa kapokea simu kutoka kwa mke wake ndani ya daladala
jamaa: hellow hellow ( jamaa akawa hasikii vizuri ikabidi aweke loud speaker)
Mke: Umeweka wapi soksi zako yaani nyumba nzima inanuka.
Soma alichojibiwa huyu mzee baada ya kudai kutaka kumsikiliza Nyerere
Mzee: Dereva ongeza sauti tumsikilize Mwalimu Nyerere!!
Dereva: ungemsikiliza mwalimu wako miaka iyo saivi ungekua na gari yako
π π π π π π π π π
Hapo sasa!! Ni shida!!
Umeshawahi saidiwa homework na mzazi halafu unapata zero?
Hapo ndio unajua shida siyo wewe
πππππππππππππππ
Ulishawahi kukutana na hii? Maana yake ni nini?
Ulishawahi kutana na hiiβ¦.
Issa: mambo
Jeni:poa vp
Issa:poa nambie:
Jeni:poa aje ww:
Issa:poa nambie
Jeni:poa
Issa :bas poa
Jeni:poaβ¦.
Issa:poa badee basi
Jeni:haya
Issa:bai
ππππβ¦β¦..HII KIITALIANO INAITWA LACK OF SOUND ENGINEERING NA HII INASABABISHWA NA UOGAβ¦β¦
Jinsi Baba na mtoto wanavyoweza kuwaziana
Duh! Maisha
Ile time unawaza baba angekua MO DWEJI baba ako na ye anawaza mwanangu angekua MBWANA SAMMATA
Ni shetani tu anajaribu kucheza na akili zenu
ππππ
Kiingereza kinashida kweli, Angalia alichokisema huyu mwalimu
Kiingereza shidaaaaβ¦β¦!
Mwalimu wa chakula alipokuwa anaongea na wapishi akiwaeleza maharage kutoungwa vizur
Tcha: these beans are not well connected,,πππ
Huyu mme ni shida
MKE..mume wangu unaweza kuua simba kwasababu yangu???
MME: Hapana mke wangu, sema kingine
MKE:unaweza kunipa nione watsapp yako nione msgs?
MME: Haya sema huyo simba yukwap nikamuue
Ndoa zina mambo, cheki haya mambo ya mtu na mke wake
Mke: mume wangu leo 2badilishe stail kwani nimechoka kla siku hiyo hiyo tu
Mme: kwel mke wang hata mimi nilikuwa nataka nikuambie hivyo hivyo
Mke: sasa stail ya leo wewe utaosha vyombo mimo nitaangalia tv
Mme: huna haya wala hujui bayaβ¦!!!
we unadhani ni xtail gani mume aldhani???
Baada ya mwanamke kukataa kufungua mlango angalia kilichomkuta
MUME: Fungua mlango!
MKE: Leo sifungui! Nimechoshwa na ulevi wako.
MUME: kama hufungui najitupa kwenye hili shimo nife kabisa.
MKE. Kufa huna faida yoyote duniani!
MUMEΒ kachukua jiwe kubwa kalitupa kwenye shimo chubwiiiiiii!
MKE kajifunga kanga, kafungua mlango. Ghafla mume kaingia ndani na kumfungia mke nje.
MKE: Nifungulie la sivyo nitapiga kelele majirani waje.
MUME: Piga kelele na wakija uwambie unakotoka usiku huu na khanga moja.
Duh! Angalia alichokula huyu mwizi! Wizi mwingine bwana!
Baada ya mwizi kuvunja mlango huko Tarime, akaingia kwenye stoo akaona vinyama kwenye bakuli vikiwa vimekauka. Akaonja 1 akaona kitamu na kina chumvi! Akavila vyote. Alipomaliza akaangalia juu ya mlango akaona pameandikwa; “chumba cha UKEKETAJI WANAWAKE”. Unafikiri atakuwa amekula nini?
Alichokisema mwizi baada ya kushinda bahati nasibu
Hapa mtaani kuna mwizi sugu ameshinda mil.10 za bahati nasibu ??.
Alipoulizwa atafanya nini na hela nyingi hizo
Akasema anataka kupanua shughuli zake. Mimi sijamuelewa na sasa hivi watu wameanza kuhama mtaaβ¦
ππ
Muda mzuri wa kulipa mahari
Amini Nawaambieni
Hakuna Muda Mzuri wa Kulipa Mahari Kama Mwezi January. Baba Mkwe Anapokea Hata Buku Kumiβ¦. ππππππ
Angalia kile kitabia cha kufuta namba kwenye simu kilivyomponza huyu jamaa
Jana nilijipa kazi ya kufuta vitu visivyo na umuhimu kwenye sm yangu. Katika futa futa si nimefuta namba ya bosi wangu. Halafu boss mwenyew wa kike. Mida ya Saa mbili usiku nikawa chumbani kwangu. Mara simu ýÀñgΓΉ ikawa inaita. Kucheki namba ngeni. Nikapokea baada ya salamu. Meβnani mwenzangu?? Bossβwe hunijui me ?? Meβusinijbu swali kwa swali Nita kublacklist sasa hiv. Sipendagi ujinga.. Kwa sasa nazurura tu mtaani na roba langu La machupa
Jinsi mzunguko wa elimu ulivyo
01.π Wale wanafunzi walioongoza
Mashuleni, wanaenda kwenye
Engineering na Medical school.
02.π Wale waliokuwa wa pili, wanachukua MBA na LLB na kuja kuwa Mameneja wa
wanafunzi walioshika nafasi ya kwanza.
03.π Wale waliokuwa wa tatu, wanageukia
Siasa na kuwaongoza wote hapo juu.
Yaani wa kwanza na wa pili.
04.π Wale waliofeli, wanaenda Jeshi, hawa wakigoma, basi hao wa juu
wote hawana raha.
05.π Wale waliopata Zero na waliokataa
shule wanakuwa waganga wa kienyeji,
wote hapo juu watamtafuta huyu, pale
mambo yao yanapokwenda kombo. Tuache kudharauliana, kila mtu ni boss akiwa kwenye nafasi yake.
ππππππππππΏππΏπππππ
Angalia kilichotokea baada ya dogo kupewa ada na kuitumia kubeti
Dogo kampigia simu baba yake;
DOGO: Baba katika zile shilingi laki mbili ulizonipa
nikalipe ada nimetumia shilingi alfu 30 kubeti
BABA : Unasema nini we mpumbavu mshenzi
mkubwa? Nimekukanya mara ngapi kuhusu kubeti?
DOGO : Lakini baba
BABA : Lakini baba nini ngoja urudi utaona
ntakachofanya.
DOGO : Nilitaka kukwambia kuwa nimeshinda
shilingi milioni 3
BABA : Ndio hayo ninayosema wewe mpumbavu
sana kwanini hukutumia laki nzima kubeti? Si
ungepata pesa nyingi zaidi? Ngoja urudi niwataarifu
ndugu zako kuhusu uulivyo na akili za kuamua
haraka mwanangu mpenziβ¦
πππππππππ
Angalia alichokifanya huyu mtu baada ya kuokota wallet ya thamani
Jamaa aliokota wallet, alipofika nyumbani akapiga simu kwenye radio station “naitwa Juma nimepiga simu kutangaza kuwa nimeokota wallet ndani ina laki7, ATM card na karatasi yenye PIN ya ATM card na kijimfuko cha dhahabu” Mtangazaji akasema, kwa hiyo ungependa kumrudishia mwenyewe kama anakusikiliza? Jamaa akajibu; hapana, ninaomba kumuombea dedication wimbo wa R.Kelly usemao “U SAVED ME” umfikie popote alipo!!
Mshahara usiobadilika
PAMOJA NA HALI NGUMU YA UCHUMI NCHINI HUWEZI AMINI MSHAHARA WA DHAMBI HAUJABADILIKA HATA KIDOGOβ¦BADO NI MAUTI VILEVILE
ππππ
Recent Comments