SMS Nzuri: Meseji za Visa Vya Kimjin Mjini

Sababu za kumuacha mke kama umemchoka

Ukimchoka mkeo, waweza kumtaftia sababu za kumuacha kama hizi

_
1. Missed calls 16? Umeua betri la simu yangu. Kwa hiyo hata mimi unaweza kuniua… It’s Over!!!
_
2. Hata hunieshimu. Mi naongea na wewe lakini we upo bize unavuta pumzi? It’s over!
_
3. Nimekupigia umepokea simu hapohapo. Huna subira. It’s over!!
_

4. Nilikwambia huwa napenda chakula cha moto lakini hujanipashia ice cream. Hunijali. It’s over!
_
5. Nimekupa mayai mawili, moja uchemshe jingine ukaange. We umekaanga ambalo ulitakiwa kuchemsha na umechemsha ulilotakiwa kukaanga. Huniheshimu, It’s over!
_
6. Nimekuita DARLING na wewe ukaniita HONEY. Yani kwa maana nyingine unamuita mama yangu NYUKI. Huheshimu wazazi wangu, fungasha kilicho chako. its over.

😄😂😄😂😄😂😄😂😄

Cheki hawa washikaji wanachokifanya baada ya kuvuta bangi, Bangi si mchezo

Kuna washikaji walikuwa wakivuta bangi… kiberiti kikawaishia… wakamtuma mwenzao akatafute kingine… bangi lilikuwa limemkolea… akazungukazunguka hatimaye akarudi palepale kijiweni…

MSHIKAJI: oyaaa wanangu eeeh… niazimeni kiberiti mwanangu mwenyewe …..

WENZAKE: baharia ee subiria kimtindo kuna mwana tumemtuma akatafute kiberiti.

Angalia hawa kina mama, ni shida..!

Mama mdaku alishangaa kila siku mchungaji anaingia nyumba ya jirani yake ambaye hana mume, akawa anajiuliza anakwenda kufanya nini? Uzalendo ukamshinda akamuuliza “Mwenzangu, mbona kila siku mchungaji anakuja kwako, vipi anakuja kukuombea?” Akajibiwa “Nyoo, umbea tu! Mbona kwako kila siku anakuja mwanajeshi kuna vita! chefuuuu 😳😳😳😳😳

😂😂😂😂😂😂😂😂😂

Huyu jamaa kawaweza wapenda vya bure

Jamaa kaingia mgahawani kwa fujo
JAMAA : Nipe soda moja na kila mtu mpe yake maana ninapokunywa soda napenda kila mtu anywe
WATU : Ha! Ha! Ha! Haaaa!
JAMAA : Nipe mchemsho na kila mtu mpe wa kwake maana ninapokula mchemsho napenda kila mtu ale wake
WATU: Watu weweeee! Tena safari hii Na makofi juu..
JAMAA : Mhudumu, nipe bili na kila mtu mpe yake maana ninapolipa bili napenda kuona kila mtu analipa yake
😂😂😂😂😂😂😂

Eti wanadamu walikuja vipi duniani

Mtoto wa miaka sita alimuuliza babake:
MTOTO: Baa, eti sisi wanadamu tulikuja vipi
duniani?
BABA: Mungu alimuumba Nabii Adam na Hawa.
Kisha wao wakaanza kuzaa watoto na watoto
wakazaa mpaka tukazaliwa sisi. (Mtoto hakuridhika
akamfuta mamake)
MTOTO: Mma, eti sisi wanadamu tulikuja vipi
duniani?
MAMA: Wanasayansi wamesema sisi tulitokana na
manyani baadae tukawa binadamu. (Mtoto akarudi
kwa baba)
MTOTO: Baa mbona mama ansema sisi tulikuwa
manyani mwanzo?Au wanidanganya?
BABA: Mwanangu, mimi nimekuelezea kuhusu ukoo
wetu. Mamako amekuelezea kuhusu ukoo wao😂😂🚶🏼🚶🏼🚶🏼

Huyu mchaga kazidi sasa, angalia anavyomfanya huyu mbuzi

Mchaga alinunua mbuzi akamwambia mpishi Nyama nusu ipike pilau na ingine itie kwenye friza. Kichwa fanya supu, miguu fanya mchuzi chukuchuku. Ngozi usitupe tutafanya mswala, utumbo pikia ndizi na mifupa tutawauzia wenye mbwa. Kinyesi kihifadhi kwa mbolea ya bustani.

Mpishi akamuuliza Hutaki na sauti ya mbuzi tufanye ring tone kwenye simu yako? Mchaga akajibu Yesuu! hivi inawezekana? bac fanya hivyo tuwauzie na wengine hiyo ringtone. Chezeya mchaga!

Shopping Cart
🏠 Home 📖 Reading 🖼️ Gallery 💬 AI Chat 📘 About