SMS Nzuri: Meseji za Vihoja Vya Kukupa Mudi Mpya
Duh! Angalia alichokula huyu mwizi! Wizi mwingine bwana!
Baada ya mwizi kuvunja mlango huko Tarime, akaingia kwenye stoo akaona vinyama kwenye bakuli vikiwa vimekauka. Akaonja 1 akaona kitamu na kina chumvi! Akavila vyote. Alipomaliza akaangalia juu ya mlango akaona pameandikwa; “chumba cha UKEKETAJI WANAWAKE”. Unafikiri atakuwa amekula nini?
Je, hili nalo ulilipitia ulipokua Shuleni?
Hakuna Kitu Kilikua Kinaniumizaga Kipindi Nipo Shuleni.
Time Mmetoka Kwenye Mitihani Wa Mathematics Halafu Mpo Kikundi Fulani Either Mnarudi Nyumbani Au Mnapumzika Kwa Ajili Ya Next Exam.
Unasikia Jamaa Wanabishana Pale Jibu Lilikua 4 Mwingine Anasema 5, Na Wewe Ulijaza 80.
Cheki huyu jamaa anachomfanyia huyu mrembo kanisani
Jamaa kaenda kanisani akakaa karibu na mrembo.
Wakati mahubiri yakiendlea jamaa akaanza kuingiza vocal:
Jamaa: dada mi nakupenda saana
Dem: Kaka naomba umsikilize mchungaji
Jamaa: nipe nafasi uwe msimamizi wa serikali ya moyo wanguβ¦
Dem: niacheβ¦
Jamaa: kweli nakupenda mpnz
Dem: (kwa sauti kubwa) nmesema NIACHEEEE!!
Watu wote kanisani wakageuka⦠Jamaa kaona noma na ili atulize msala
Jamaa: sikuachi hadi ukiri YESU kuwa Bwana na mwokozi wa Maisha yako.
Angalia huyu bibi alichotufanyia kwenye gari
βtulikua kwenye gari kibao ad wengne mlangon likasmimama kituo kimoja kulikua kuna bibi anataka kupandaβ
Konda- bibi twende sit kibao ata utalala
Bibi – oooh sawa mjukuu
Konda – simama tu apo wanashuka mbele
Bibi – akacheka sana tu
Konda- mbona unacheka bibi
Bibi – mjukuu hawa wote hawashuki wanakufa apo mbele
Watu- simamisha gar
Saiv bibi kabaki mwenyewe amelala sit ya nyumaπππ ππ
Cha kufanya msichana akikukimbia halafu atake kukurudia
β¦β¦β¦ Kama msichana atakutupa kwa sababu huna pesa, na baadaye unapopata pesa akarudi tena kuomba msamahaβ¦ Ndugu yanguβ¦.. Msameheβ¦. Mpe ahadi ya ndoa, mwambie utamuoaβ¦. iambie familia yake unataka kufanya ukarabati wa nyumba yaoβ¦β¦ Ondoa paa lote la nyumba yao halafu TOWEKAβ¦..
πβ¦β¦β¦ πβ¦β¦.. π
Angalia huyu demu alivyo mbulula
Jamaa aliamua kumtoa demu wake out kwaajili ya chakula cha usiku kufika hotelini wakakaa mezani mhudumu akaja,
Mhudumu: kaka nikuhudumie nini,
Jamaa: afathal NILETEE MENU LISTI
Mhudumu: dada na wewe?
Demu akajibu kwa pozi tena kwakujishaua, “NA MIMI NILETEE MENU LIST ILA USIWEKE CHUMVI NYINGI”
Chezea mbulula weweβ¦!!!
Kali ya mwaka iliyotokea Benki Baada ya wezi kuiba
Kuishi kijijini kunahitaji moyo sana
..unaenda kuoga, unakumbuka kuwa umesahau sabuniβ¦unaenda kuchukua sabuni kurudi bafuni, unakuta ng’ombe amekunywa maji yote..unaamua kufuata mengne,unarudi unakuta mbuzi kala sabuniβ¦ππππ
Tofauti ya ukopaji wa mzungu na mswahili
MZUNGU: Hi, I need $100, will pay back on Monday
MSWAHILI: Kaka vipi, shwari? Dah.. hatuonani mzee, mishe vipi, mnatunyima nini? Juzi nimekuona kwa mbaaaliβ¦ mzee shavu dodo, full kipupwe! Sie tupo bwana, shida tu, afu misiba mingi tu, wife nae kajifungua ghafla. Sasa, kuna cheque naisubiri haijatoka hadi leo, wanasema itatoka next week, hapa nimekwama kweli. Naweza pata ‘Laki Moja’ ya karibu hapo nitarudisha mwisho wa mweziβ¦?πππππ
Duh, hii sasa kazi
Wakati unafikiria dingi yako afe ili urithi nyumba, dingi nae anafikiria uanze kufa ili apangishe chumba unacholala.. hiyo inaitwa kufa kufaana.. πππππππππ #Hatutaki ujinga
Duh! Tamaa mbaya, cheki kilichompata Huyu
HAHAHAHAHAAAAAA DUH TAMAA MBAYA
Muokota makopo katika uokotaji wake wa makopo akaona chupa ambayo ndani kuna ki2, alipoifungua likatoka jitu la ajabu. Huku akitetemeka lile jitu likamwambia kijana asante sana kwa kuniokoa omba vi2 viwili sasa hivi. Kijana kwa hofu akaomba pesa za kumiliki magari na majumba ya kifahari. Ghafla fuko la hela na pete ya bahati vikadondoka. Akaambiwa ombi la pili,akasema nibadilishe niwe kivutio ili nipendwe sana nakina dada Hapohapo akageuzwa akawa chipsi yai.!!ππ€£π€£π€£
Kilichotokea baada ya mzungu na mbongo kukaa siti moja, bongo wasanii wengi
Mzungu akamdharau sana Mbongo nakujiona anajua kila kitu duniani!,
Akamwambia Mbongo waulizane maswali na Mbongo akishindwa anatoa sh.500 na endapo yeye atashindwa atatoa 100,000/=.
Mzungu akauliza ni nchi ipi ilishindwa kwenye vita kuu ya kwanza ya Dunia?
Mbongo akatoa 500 kuashiria hajui.
Na yeye akamuuliza Mzungu ni kitu gani kikienda juu kina miguu minne na kikirudi chini kina miguu mitatu?
Mzungu akafikiria akakosa jibu akatoa 100,000/= kuashiria hajui ila akataka kujua, akauliza ni nini hicho?
Mbongo akatoa 500 kuashiria hata yeye hajui!.
SHARE na marafiki kama umemkubali Mbongo kwa ujanja. Lakini unafikiri Mbongo huyu kwa akili hizi atakuwa ametokea mkoa gani!?.
Usichokijua kuhusu sungura, panya na jamii yao
JE WAJUA?
Sungura, panya na Jamii zao huwa na mwendo wa kukimbia na kuruka muda wote na umri wao wa kuishi ni miaka 15. Kobe ni mnyama mwenda pole, asiye na papara wala pilika, muda mwingi hujificha na kupumzika ndani ya jumba lake akikwepa maadui. Umri wa kuishi kobe hufikia hadi miaka 300.
FUNZO: Mazoezi ni kiinimacho na uongo mtupu. Jipumzikie mwaya!!!
ππΎππΏβ
Mtoto ni wa baba au wa mama? Angalia hoja za baba na mama kila mmoja anadai ni wake
Mtoto ni wa baba au wa mama?
Mume alimpa mkewe talaka wakaenda mahakamani ili hakimu aamue nani akae na mtoto.
MME: Akasimama akauliza hivi: Mheshimiwa hakimu hivi nikichukua ATM card nikaingiza kwenye mashine ikatoa pesa, sasa pesa zitakuwa ni za ATM au zakwangu?
MKE: Akasimama na kusema: Mheshimiwa hakimu hivi ukimwaga mbegu ktk shamba la mtu mti ukiota utakuwa wa kwako au wa mwenye shamba?.
Hebu tumsaidie hakimu aamue kesi hiiβ¦
Alichokisema mtoto baada ya kusikia baba na mama wakiongea mambo yao usiku
MUME: Mke wangu naomba nikubusu
MKE: Sitaki
MUME: Ntakununulia pete ya gold
MKE: Staki
MUME: Ntakununulia gari
MKE: Sitakiβ¦.mtoto wao aliyekuwa kalala alisikia haya maneno ya mwisho
MTOTO: Baba basi nibusu mimi uninunulie baiskeli
BABA: Pumbafu lala huko mjinga mkubwa
Sababu ya mwanaume kunya kitandani alipokuwa kalala na mke wake
Jamaa flani alikuwa amelala na mkewe. Mara akamuona mtu amesimama kitandani.
Jamaa akafoka, “Toka hapa, we ni nani mpaka unakuja kitandani mwangu?”
Yule mtu akajibu, “Mi ni malaika na hapa sio kitandani mwako uko mbinguni!”
Jamaa, “Huh! Inamaana nimekufa,mbona mi bado kijanaβ¦ naomba nirudishwe!”
Malaika, “Inawezekana lakini siwezi kukurudisha kama mtu labda urudi kama mbwa ama kuku.”
Jamaa akakumbuka mbwa wanavyopata taabu ya kulinda, akaonelea arudi kama kuku.
Malaika akamgeuza kuku, akamwambia ajifunze kutaga kabla hajapelekwa duniani.
Akachuchumaa na kuanza kujikamua; yai la kwanza likatoka. akajikamua tena, yai la pili likatoka. Akajikamua tena mara ya tatu.
Wakati yai la tatu linatokaβ¦ akashtukia amepigwa konde ikifuatwa na sauti ya hasira ya mkewe, “Pumbav*! Balaa gani hiiβ¦. unakuny* kitandani!!”
MAJIBU YA MAKONDA WA DALADALA ZETU GONGOLAMBOTO HUKU
1. wewe Dada unaturingia nini na matiti yako mawili , mbwa pia ana matiti nane na haturingii eboo !!!!
2. Ka wafikiri Una haraka sana Shuka ukimbie.
3. Nauli kulipa lazima ,Chenji ukikumbuka.
4. Kutapika ndani ndani ya Daladala fain 250/= ,ukijamba pia 250/= ,Sasa jamba tukujue viti vina alarm!β¦
5.Hatujasema wewe ni Mnene ila Ukikalia SITI mbili Lipiaβ¦.
6. Hio Elfu kumi yako nenda nunua avocado upake alafu uteleze hadi posta ,nauli ya daladala ni 350/=.
7. usifungue dirisha ungetaka upepo ungepanda pikipiki..
8. wewe Dada hebu sogea hukoo, Unaringa nini wakati asubuhi hii umeoga na sabuni ya kuoshea vyomboβ¦
Angalia huyu baba alichowafanya mtoto wake wa kike na boyfriend wake
BABA OYEEEEEEπͺπͺ
Soma hiiβ¦
Msichana alikuwa amekaa na baba yake kibarazani, mara akamuona MVULANA friend wake akija, yule mvulana alipokaribia tu, yule msichana akamwambia hivi:-
MSICHANA: Umekuja kuchukua kile kitabu chako, kinachoitwa “DADDY IS AT HOME?” by Ngozi Okafor
MVULANA: Hapana!, Nimekuja kuazima kitabu cha maombi kama kinaitwa “WHERE SHOULD I WAIT FOR YOU?” by NgΕ©gΔ© wa Thiong’o
MSICHANA: Aaah! Hicho sina ila ninacho kimoja kinaitwa “UNDER THE MANGO TREE” by Chimamanda Adichie
MVULANA: Ooh! Vizuri, Basi usisahau kuja nacho kesho kitabu cha Okot p’Bitek kile kinachoitwa “CALL ME IN 5 MINUTES BEFORE” Utakapokuja shule.
MSICHANA: Usijali, tena nina kitabu kipya kinaitwa “I WON’T LET YOU DOWN” by Chinua Achebe
Baba mtu akawatazama kisha akasema
BABA: Vitabu vyote hivyo, mbona vingi sana, atavisoma vyote kweli
MSICHANA: Ndio Daddy, huyu mvulana yupo smart sana na ana akili atavisoma vyote hivyo!
BABA: Sawa! Usisahau kumpatia na kile ambacho nimekiweka pale juu ya meza, kinaitwa “I AM NOT STUPID, I UNDERSTOOD EVERYTHING YOU’VE BEEN SAYING” by Shakespeare!
Na kuna kingine nimekiweka juu ya kabati la vyombo, kinaitwa “IF YOU GET PREGNANT PREPARE TO GET MARRIED” by Wole Soyinka.
Recent Comments