SMS Nzuri: Meseji za Vihoja Vya Jumatano

Kichekesho cha mtalii na mbongo

Duh! Sikubali bora mbavu zituume wote!

Watalii wana dharau sana bana, Mtalii alikodi boti akazunguka nayo kwenye mto Rufiji kuangalia mandhari, akamuuliza kijana anayeongoza boti, “Do you know Biology, Psychology and Anthropology?” Kijana akajibu “NO,” Mtalii akamwambia “nothing you know under the sun? You are useless, and u’ll die with your illiteracy!” baada ya muda boti ikaanza kuzama, kijana akamwambia mtalii “Do you know kuogelealogy and kusepalogy from mambalogy? Mtalii akajibu huku ametoa macho “No” kijana akamwambia “You will kufalogy and mambalogy wil eat your matakology because of your bad-mdomology..๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚

Usichokijua kuhusu sungura, panya na jamii yao

JE WAJUA?

Sungura, panya na Jamii zao huwa na mwendo wa kukimbia na kuruka muda wote na umri wao wa kuishi ni miaka 15. Kobe ni mnyama mwenda pole, asiye na papara wala pilika, muda mwingi hujificha na kupumzika ndani ya jumba lake akikwepa maadui. Umri wa kuishi kobe hufikia hadi miaka 300.
FUNZO: Mazoezi ni kiinimacho na uongo mtupu. Jipumzikie mwaya!!!
๐Ÿƒ๐Ÿพ๐Ÿƒ๐Ÿฟโ€

Huyu jamaa bonge la bwege, ungekua wewe ndiyo rafiki ake ungemwambiaje?

RAFIKI: Vipi mbona leo huna uchangamfu
JAMAA: Wanawake bwana, mwanamke hata umpendeje atakugeuka tu
RAFIKI: Nini tena ndugu yangu? Mbona shemeji mtu fresh sana
JAMAA: Hata mimi nilikuwa najua hivyo, leo nimegundua kumbe ana siri kubwa sana
ananificha, mi naita huu ni usaliti wa ndoa.
RAFIKI: Nini tena?

JAMAA:Nimegundua mke wangu kumbe anafanya biashara ya kitimoto na hajawahi hata kuniambia
RAFIKI: Kitimoto? We umejuaje?
JAMAA: Leo asubuhi nilichelewa kuamka niliamua nijipumzishe kidogo kabla ya kwenda kazini, simu ya mke wangu ikalia, nikaamua kuipokea, kabla hata sijafungua mdomo, nikasikia sauti ya mwanaume mmoja akauliza, โ€œHuyo nguruwe umeshamuondoa?โ€™ Hebu we fikiria nilivyoshtuka, yaani mpaka sasa nashindwa kuamini kuwa mke wangu ananizunguka anafanya biashara ya nguruwe hajaniambia hata siku moja

Kilichotokea baada ya babu mzee kuibiwa nauli kwenye daladala

Mzee mmoja alipanda Gari Stend;
Wakati wa kugombania Siti,
Akaibiwa Nauli.

Akasimama katikati ya Gari-Akasema; “Jamani Naomba Aliyeniibia Pesa yangu Arudishe Haraka,
Tena Fasta kabla Sijafanya Tukio kama Nililofanya 1977″
Abiria kuskia hivyo wakaogopa.
Ikabidi Mwizi Ajitokeze,
Akarudisha Pesa na Kuomba Msamaha! Mtu Mmoja akauliza,
Mzee,
Kwani 1977 Ulifanya nn?
Si nilienda kwa Miguu mpaka Nyumbani!
Uscheke Peke Yako, wa2mie na wengine ili nao wacheke!

Angalia sababu ya mke Mtarajiwa kuzimia kabla ya harusi

*Jihadharini* na wachapaji wa kadi za harusi. Hakikisha unasoma maandishi yaliyochapwa kabla ya kadi kuchapwa na kusambazwa!

Mchapaji aliombwa aweke 1 Yohana 4:18 katika kadi ya harusi lakini mchapaji kwa makosa aliweka Yohana 4:18.

1 Yohana 4:18 panasema, “Katika pendo hakuna hofu, lakini pendo lililo kamili huitupa nje hofuโ€ฆ”

Lakini Yohana 4:18 tunasoma, “Kwa maana umekuwa na waume watano, naye uliye naye sasa siye mume wako.”

๐Ÿƒ๐Ÿƒ๐Ÿƒ๐Ÿƒ๐Ÿƒ๐Ÿƒ๐Ÿƒ๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚_MKE MTARAJIWA AKAZIMIA HAPA, TUNAMPEPEA_

Angalia sababu ya mwanamme kubadili jina na Kuitwa jina la kike, hii dunia ina mambo kweli

Rashidi alimpa ujauzito mwanafunzi, akashtakiwa.
Kumbe Rashidi ana bibi yake mtaalamu wa yale mambo yao ya Sumbawanga, akampachika Rashidi i jinsia ya kike.

Alipofika mahakamani kuhojiwa Rashidi akasema sijampa ujauzito kwa sababu mimi pia nina jinsia ya kike.
Kwa kuthibitisha Rashid wakaenda kumkagua basi akashinda kesi, kufika nyumbani Rashid akawakuta watu wamejaa wanalia, akauliza kulikoni?
Akaambiwa bibi yako amefariki. ๐Ÿ˜ญ๐Ÿ˜ญ๐Ÿ˜ญ๐Ÿ˜ญ๐Ÿ˜ญ๐Ÿ˜ญ๐Ÿ˜ฐ๐Ÿ˜ฐ๐Ÿ˜ฐ๐Ÿ˜†๐Ÿ˜†๐Ÿ˜†๐Ÿ˜†๐Ÿ˜†๐Ÿ˜†
Kwa sasa Rashid anaitwa Leila๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€

Tofauti ya mwanamke wa Kizaramo, Kitanga, Kihaya, na wa Kichaga

Mwanamke wakizaramo: Unampa hela ana nunua dela anaenda ana msutia jirani, analivaa dela bila nguo ya ndani mbele yako, unazidiwa anakupa kitu fresh unatoka unatabasamu.๐Ÿค๐Ÿฝ๐Ÿ™Œ๐Ÿฝ

Mwanamke wa kitanga:
Unampa hela anapika vitu mtaa mzima unasikia harufu ya chakula, chenji inayo baki ananunua kinga ukirudi unakula afu unakula..๐Ÿ‘๐Ÿผ๐Ÿ‘๐Ÿผ๐Ÿค๐Ÿฝ๐Ÿ™Œ๐Ÿฝ

Mwanamke wa kihaya:
Unampa hela ukirudi unakuta majirani wote wanataarifa kuwa wew uliacha hela, anakupkia vitu vzuri, usiku anakuhudumia ukimsifia anakuhudumia tena hata mara nne kwa usiku mmoja..we mle sifa tu๐Ÿ™Œ๐Ÿฝ๐Ÿ™Œ๐Ÿฝ๐Ÿคธ๐Ÿพโ€โ™€๐Ÿ‘Œ๐Ÿฝ.

Mwanamke wa kichaga:
Unampa hela anaenda ananunua dagaa anapika na michuzi mingi mpaka dagaa wanafufuka unakula kwa shida, dagaa wanakula utumbo wako unakufa.. Madaktari wanajitahidi wanakutibu unafufuka. Ukiwa hujapata akili vizuri anakuletea bili ya umeme, anakukumbusha deni la kwa Massawe, anakukumbusha kodi ya nyumba.. *Unashikwa na presha unakufa moja kwa moja*๐Ÿ™Œ๐Ÿฝ๐Ÿ˜‚๐Ÿ™†๐Ÿผโ€โ™‚๐Ÿƒ๐Ÿพ๐Ÿคธ๐Ÿพโ€โ™€

Angalia huyu secretary anavyomjibu bosi wake

Boss mmoja aliingia kazini kwake kasahau kufunga zipu ya suruali yake sasa secretary wake akamfuata na mazungumzo yakawa hivi:

SECRETARY: Boss leo umesahau kufunga geti nyumbani kwakoโ€ฆ

Boss akabaki anashangaaโ€ฆ Baadae wakati anakwenda chooni kujisaidia ile anataka kufungua zipu akaikuta iko wazi ndio akajua alichokuwa ameambiwa na Secretary wake.

Akarudi mpaka kwa secretary na mazungumzo yakaendelea:

BOSS: Bibie ulivyoona geti wazi je uliona benz langu lime paki auโ€ฆ?

SECRETARY: Hapana Boss niliona kitoroli kidogo kimepaki kina matairi mawili

Vichekesho vya kukuondoa mawazo leo

Soma vichekesho hivi;

Mwizi wa atm

Jamaa aliibiwa kadi yake ya benk akaulizwa kama ameripoti polisi akajibu “sijaripoti bado, mwizi mwenyewe hamfikii matumizi kama mke wangu.

Cheka kidogo

Njia rahisi kusahau matatizo yako (japo kwa muda mfupi) vaa viatu vinavyokubana.

Mlizi mbio mbio

Tulikuwa bar moja jana mlinzi kaingia spidi, akamwambia jamaa mmoja aliyekaa kaunta, Mlinzi: Mzee gari lako limeibiwa Mzee: Umemtambua aliyeiba? Mlinzi: Hapana lakini nimeandika namba za gari hizi hapa.

13, 13โ€ฆ

Jamaa alikuwa anapita nje ya wodi ya vichaa akasikia mtu anasema, 13, 13, 13, 13, 13, 13,โ€ฆ.. akaamua kuchungulia kwenye kitundu alichokiona ajue kuna nini, ile kuchungulia tu akamwagiwa mchanga wa machoni, sauti ikabadili ikaanza 14,14,14,14,14โ€ฆโ€ฆ

WATAALAM

Jamaa alikuwa anaumwa sana, mkewe akamwita daktari, alipofika akamkuta jamaa kafumba macho;
Dokta: Huyu mbona amekwisha kufa?
Jamaa: Sijafa bwana
Mke: Hebu nyamaza bwana acha kubishana na wataalamu.

Ya leo mgonjwa

Dokta alipotembelea wodi ya mgonjwa wake aliyepata ajali. Mgonjwa akiwa amening’inizwa mikono juu akauliza “dokta ntaweza kweli kupiga kinanda nkitoka hospitali?”
Dokta: Bila shaka utaweza, wewe ni mpiga kinanda mzuri enh?
Mgonjwa: Hapana sijawahi kabisa bado.

4WD

Mwanaume alimnunulia pete ya almasi mkewe, rafiki akauliza “si ulisema anapenda gari yenye four wheel drive, mbona umenunua pete?” Mume akajibu “unadhani wapi ntapata rav4 feki?”

Ajali ilivyotokea

Trafiki polisi akihoji palipotokea ajali “ahaa! Sasa naanza elewa embu nielezee jinsi ajali ilivyotokea wewe ukiwa kama dereva mhusika.” Dereva akajibu “hata sikumbuki nlifumba macho”

Faini ya kukojoa

Polisi alimdaka jamaa anakojoa pembezoni mwa ukuta.
Polisi: Wewe unajua panakatazwa kukojoa hapa?
Jamaa: Sasa nimebanwa nifanyaje?
Polisi: Faini yake elfu tano.
Jamaa akatoa noti ya elfu 10.
Polisi: Sasa chenji tunaipataje?
Jamaa: Tafuta chenji unipe changu.
Polisi: Basi kojoa tenaโ€ฆ

Mume anaenda kazini

Jamaa kaamka asubuhi sana Jumamosi, mvua inanyesha kang’ang’ania kuwa anaenda ofisini. Kawasha gari yake, kufika njiani hali ilikuwa mbaya kaamua kurudi. Kafika home kavua nguo kaingia tena kitandani, kamnong’oneza mkewe aliyekuwa usingizini; “Yaani hali ya hewa huko nje mbaya sana” Mke: Si ndio nimemshangaa huyu mpumbavu eti kaenda kaziniโ€ฆ

Hasira za mtoto

Baba na mtoto:
Baba: Mwanangu ukiwa na hasira unafanya nini?
Mtoto: Naenda chooni.
Baba: Chooni? Kufanya nini?
Mtoto: Kusafisha.
Baba: Halafu ndio hasira zinaisha?
Mtoto: Ndio. Nasafisha choo kwa mswaki wako.

Mgonjwa na Dokta

Mgonjwa: Dokta nimekuja nahisi ninaumwa Malaria na kifua.
Dokta: Sasa ushajua unaumwa nini hapa umefuata nini kwangu?
Mgonjwa: Sasa si nimekuja kwa dokta.
Dokta: Wanaojua kuwa wanaumwa kama wewe wanapitiliza maabara.

Pilau la bachela

Bachela mmoja aliyekua akiishi kwa muda mrefu peke yake kwenye nyumba aliyopanga siku moja alitaka kupika pilau kwa mara ya kwanza. Sasa asijue nini kinachobadilisha rangi ya wali kuwa rangi ya brown, yeye akapika kama kawaida (wali) kisha wakati wa kula akavaa miwani yenye rangi ambayo ukiuangalia wali unauona kama pilau wakati anakula.

Mwizi na chizi

Mwizi kaiba TV na kuanza kukimbia nayo, kumbe ile nyumba mlikuwa na chizi, akaanza kumkimbiza yule mwizi. Kila mwizi akiongeza mbio chizi nae huyo, mwishowe mwizi akasalimu amri na kusimama, yule chizi akamsogelea na kumwambia.. Daah umesahau remote hii hapa mwizi kafleti.

Chemsha bongo

Baba akimuuliza chemsha bongo mwanae anayesoma shule ya chekechea “haya niambie kitu gani hakiwezi kuliwa wakati wa breakfast?” Mtoto akajibu “hiyo mbona rahisi baba, si lunch na dinner”

Shopping Cart
22
    22
    Your Cart
    Kitabu cha SMS Maalumu kwa Umpendaye
    Kitabu cha SMS Maalumu kwa Umpendaye
    1 X Sh2,500 = Sh2,500
    ๐Ÿ  Home ๐Ÿ“– Reading ๐Ÿ–ผ๏ธ Gallery ๐Ÿ’ฌ AI Chat ๐Ÿ“˜ About