SMS Nzuri: Meseji za Vihoja Vya Ijumaa

Huyu mama mkwe kazidi sasa

Eti kuna mkaka alitembelewa na mama yake mzazi. Wakiwa sebuleni yeye, mama na mke wake, mke wake akaanza kuonekana tofauti kama vile anajiskia vibaya. Akaenda chumbani. Baada ya muda mfupi yule mkaka akamfuata. Wakakaa sana huko kisha mkaka akarudi sebuleni kuendelea kuongea na mama yake. Lakini zipu ya suruali yake ilikuwa wazi. Mama akamuuliza, mkeo anaendeleaje? Akamuambia, anajisikia vzr sasa. Nimempa panadol. Mama akatabasamu na kumwambia mwanaye, sawa. Lakini siku nyingine ukishatoa panadol ukumbuke kufunga pharmacy๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚

Kichekesho cha mtalii na mbongo

Duh! Sikubali bora mbavu zituume wote!

Watalii wana dharau sana bana, Mtalii alikodi boti akazunguka nayo kwenye mto Rufiji kuangalia mandhari, akamuuliza kijana anayeongoza boti, “Do you know Biology, Psychology and Anthropology?” Kijana akajibu “NO,” Mtalii akamwambia “nothing you know under the sun? You are useless, and u’ll die with your illiteracy!” baada ya muda boti ikaanza kuzama, kijana akamwambia mtalii “Do you know kuogelealogy and kusepalogy from mambalogy? Mtalii akajibu huku ametoa macho “No” kijana akamwambia “You will kufalogy and mambalogy wil eat your matakology because of your bad-mdomology..๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚

Mtoto ni wa baba au wa mama? Angalia hoja za baba na mama kila mmoja anadai ni wake

Mtoto ni wa baba au wa mama?

Mume alimpa mkewe talaka wakaenda mahakamani ili hakimu aamue nani akae na mtoto.

MME: Akasimama akauliza hivi: Mheshimiwa hakimu hivi nikichukua ATM card nikaingiza kwenye mashine ikatoa pesa, sasa pesa zitakuwa ni za ATM au zakwangu?

MKE: Akasimama na kusema: Mheshimiwa hakimu hivi ukimwaga mbegu ktk shamba la mtu mti ukiota utakuwa wa kwako au wa mwenye shamba?.

Hebu tumsaidie hakimu aamue kesi hiiโ€ฆ

Wabongo ni noma! Angalia huyu mbongo anachokifanya

Basi juzi kati hapa sehemu ndogo ya ukuta wa Ikulu ya Magogoni ilianguka!..
Wakapelekwa contractors watatu ili achaguliwe mmoja atakayejenga vzr na kwa bei nafuu!..
Wakwanza alikuwa MUHINDI, wa pili MCHINA na MBONGO!โ€ฆ

MUHINDI: “ntajenga kwa milioni 90!.., 40 za vifaa, 40 za mafundi na milioni 10 faida yangu”

MCHINA: “mi ntajenga kwa milioni 70!.., 30 za vifaa, 30 za mafundi na milioni 10 faida yangu”

MBONGO kuona vile akamvuta chemba msimamizi wa Magogoni!..
MBONGO: “mi ntajenga kwa milioni 270”

MSIMAMIZI WA MAGOGONI: “we una wazimu nn!.. yaani unathubutu kusema hivyo na unaona wenzako wametaja kiwango kidogo?!.”

MBONGO: “milioni 100 zako, 100 zangu alafu hiyo milioni 70 tunaajiri yule mchina”

Utani wa wachaga

Wachaga wamegawanyika kama ifuatavyo, sio wote wajanja. Kuna:-

1. WAROMBO; Hawa wajanja sana kibiashara/wezi pia. wanapenda dili za magendo. Ni walevi sana hupeleka wake zao vijijini wakileta kiburi mjini. Wanaume wa Rombo wanachunwa sana na wanawake wa Marangu na wanawaita “vishohia”. Wanawake wa Rombo ni mama Huruma, wanaachia tu.. Ukioa Mrombo ujue umeolea kijiji.

2. WAMARANGU; Ni wazuri sana wa sura na umbo, wanavutia. Lakini wanawachuna sana Warombo. Wanawake wa Marangu wana dharau sana na wanaume ni waoga kuliko wanawake. Mwanaume wa Marangu kupigwa na mkewe si jambo la ajabu.

3. WAKIBOSHO; wanafanana na Warombo lakini ni wavumilivu zaidi. Biashara kubwa wanayofanya ni ya kuchinjaโ€ฆ wengi wanamiliki mabucha. Wana hasira sana na ni wakatili.. Akikuchoma kisu, siku ya mazishi anakuja kudai kisu chake.

4. WAMACHAME; hawa ni wezi sana, ukifanya nae dili umeliwa. Ni wasiri sana lakini wako makini mno hasa kwenye pesa. Wakiwa na hasira hawaoneshi waziwazi, so Mmachame anaweza kukuua huku akitabasamu. Sio waaminifu sana lakini wanaenda kanisani mara nyingi zaidi kuliko Wachaga wote. Wanawake wa machame wanaitwa ‘Wapalestina’.. Mume ukitajirika mkeo anakuua ili arithi mali.

5. WAURU; hawa hupenda kusoma sana lakini hawapendi maendeleo kabisa. Hadi leo eneo lao la Kishumundu linatumika ku-identify wachagga washamba. Wanawake wakifikisha umri wa miaka 40 hua wehu na wanaume huwa vichaa mapema zaidi. Wanaume ni wavivu, lakini wanawake ni wachapakazi hodari. Wanazurura mjini na mabeseni wakiuza ndizi mbivu.. Ukioa Uru jiandae kulea kichaa.

6. WASIHA; Kwanza hawapendi kuitwa Wachagga. Wanajiita watu wa West-Kilimanjaro. Ni mchanganyiko wa Wachagga na WaMeru. Hawapendi shule ila wanapenda zaidi kazi za ufundi na kilimo. Viazi vingi vya Chips Arusha na Moshi vinatoka kwao. Wanawake zao wana “vigimbi” mguuni sababu ya kulima mno.!

7. WAKIRUA; wanapenda sifa kama Wahaya. Wanawake wa Kirua ni wachawi kupindukia.. Wanaloga hata jiwe ili tu alikomoe.. Wanaume wa Kirua hawapendi kuoa kwao.. Hawapendi kuishi mjini maana wanaogopa gharama.. lakini siku wakija mjini wawili tu utadhani wako mia.

8. WA OLD-MOSHI; Hawa ni mafundi stadi wa ujenzi wa nyumba, japo hawajengi kwao. Mpaka leo hamna daladala ya kwenda Old-Moshi inayoanzia Moshi mjini, maana ni wabishi kulipa nauli na pesa inaishia kwenye mbege njiani. Wanaume wamezoea kutoka nyumbani saa kumi na moja alfajiri na kurudi saa sita ya usiku kwa miguu.!

Wachaga mnisamehe!
๐Ÿƒ๐Ÿƒ๐Ÿƒ๐Ÿƒโœ‹โœ‹

Shopping Cart
๐Ÿ  Home ๐Ÿ“– Reading ๐Ÿ–ผ๏ธ Gallery ๐Ÿ’ฌ AI Chat ๐Ÿ“˜ About