Pale unapozamia kwenye Dinner Party ya Jumuiya Fulani, sasa Lengo la Jumuiya hiyo ni kupata Fedha za kutunisha Mfuko wa Jumuiyaā¦sasa unakakaa mbele kabisa ili Muda wa Msosi usichelewe na kukuta kwenye Buffee yamebaki maharage!
MC : “Papai zuri kabisa kutoka Newala, Papai Mwendokasi, hili ni Shilingi laki 1..jamani Papai,nipeni ofa!”
MOSHA : “Laki 3 hapaaa!”
“Jamani laki 3 pale kwa Mosha, Papai linaondoka jamani, papai hili ni self contained kabisaā¦.papai jamani”
KIBOLIBO: “Milioni 1 hapaaa”
“Jamani Mambo yanazidi kunoga hapa!ā¦Benedict Kibolibo anataka papai kwa milioni 1 jamani, linaondoka papai!”
RWEYEMAMU : “nitanunua Papai hilo kwa Milioni 5”
Haya sasa jamani Rweyemamu ametoa ofa ya Milioni 5 Jamani, nani mweingineee?”
Kimyaaaā¦
Haya jamani Papai kama hakuna Ofa basi Papai linakwenda kwa Rweyemamu!ā¦ā¦..haya sasa Kuna Kuku hapa Jogoo kabisa, bei yake ni laki 6 jamani Jogoo twitter huyu!”
WEWE “Milioni Mojaaa!”( hapa umejiwahi wa kwanza na wewe uonekane upo huku ukijua kabisa Wakina Mosha na Rweyemamu lazima watampandia Dau Jogoo, tena dau kubwa”
MC: ee sasa Kumekucha Jamani, Kabasele anamtaka Jogoo kwa Milioni 1 jamani!ā¦.ofa nyingineeee!”
Kimyaaaā¦
Jamani Jogoo anakwenda kwa Kabasele jamani!ā¦ofa nyinginee!
Kimyaaaā¦.
Kimyaaaā¦.
šššā¦hapa sasa ndio mfukoni kuna Buku jero,..huko kwengineko NMB nill balanceā¦sasa unageuza mimacho kumtazama Mosha kama atapanda dau kwa jogooš(mama wee Mosha anachezea Simu!)ā¦..unamtazama Rweyemamu (teh anatafuna Kuku)ā¦..mama weeeš
MC: Haya jamani kama hakuna Mwingine basi zoezi letu liishie hapa na limekwenda kwa Mafanikio, Mpatieni Kabasele Jogoo wake!
Hapa sasa unapokea jogoo wako wa MILIONI kwa Tabasamu la Maitiā¦.kule nyumbani Jogoo wako Mkubwa unauza elfu 20 lakini sasa haka kajogoo kapya Mkononi kanakuwa kazito utadhani umembeba John Cenašā¦Mama weee hapa sasa vidari ulivyotafuna unaviona kama vimerudi kwenye Ulimiā¦.Chicken wings zinataka kutokea Masikioniā¦..Uuuuwiiiii,ššš
Na hapa sasa kabla Dinner haijaisha ndipo unapojikuta Umebuni Cocktail ya Sparetta na Tomatoššššš.
chiel wie okee