SMS Nzuri: Meseji za Vichekesho Vya Weekend
Alichokisema mwizi baada ya kushinda bahati nasibu
Hapa mtaani kuna mwizi sugu ameshinda mil.10 za bahati nasibu ??.
Alipoulizwa atafanya nini na hela nyingi hizo
Akasema anataka kupanua shughuli zake. Mimi sijamuelewa na sasa hivi watu wameanza kuhama mtaaโฆ
๐๐
Kweli mitandao imeharibu watu, angalia huyu anachokisema sasa
๐๐ kweli nimeamin mitandao inahribu watu
Leo kuna jamaa kamuona Dada akipita barabaran kapendeza jamaa kamwendea Dada akamwambia!
Dada nice photoย ๐๐๐๐
Misemo 17 ya kuchekesha
1) gari la kuvutwa halina overtake
2) kisigino hakikakai mbele
3) wimbo wa taifa haupgwi disko
4) feni haiwashwi beach
5) mshkaki hauchomwi kwa jiko la ges
6) mganga haagiz tembele
7) hata bibi alikuwa bint
8) mke wa mtu sumu,mume wamtu maziwa
9) kipara bila pesa ni kovu
10) mbwa hanenepi migiuu
11) picha ya rais haina bodyguard
12) mjini shule kijiji tuition
13) saa ya ukutani haivaliwi mkonon
14) heshima pesa shkamoo makelele
15) ulinz pesa bastora mzgo
16) kuku ni kuku jogoo mbwembwe
17) kusoma kuelewa kukesha mbwembwe
Duh! Angalia alichokula huyu mwizi! Wizi mwingine bwana!
Baada ya mwizi kuvunja mlango huko Tarime, akaingia kwenye stoo akaona vinyama kwenye bakuli vikiwa vimekauka. Akaonja 1 akaona kitamu na kina chumvi! Akavila vyote. Alipomaliza akaangalia juu ya mlango akaona pameandikwa; “chumba cha UKEKETAJI WANAWAKE”. Unafikiri atakuwa amekula nini?
Kilichotokea baada ya jambazi kuvamia kanisa
Jambazi mmoja aliingia kanisani na bunduki akapiga risasi juu ya bati akasema “asiyempenda YESU atoke nje” wakatoka wote ispokuwa Mchungaji na Wazee wawili.
Jambazi likamwambia Mchungaji “unaweza kuendelea na ibada, nilikuwa nakuondolea wanafiki”, Mchungaji akasema “ungewaacha kwanza nichukue sadakaโฆ!
Kilichotokea kati ya mkaka na mdada walipokutana hotelini
Mkaka aliingia kwenye hoteli moja akaketi meza moja na mdada mrembo maarufu sana;
MKAKA: Samahani dada sijui saa ngapi?
MDADA: Nani kakwambia saa yangu ndio ya kuangalia kila mtu?
MKAKA: Samahani sanaโฆ.jamaa akachukua Galaxy yake akapiga simuโฆ.aise saa ngapi saa hizi? mi ndio nimeingia toka USA nataka kurekibisha saa yangu ifwate muda wa huku. Na wewe uwahi kuchukua iPad nimekuja nazo tatu tu za zawadi. Halafu ntafutie mtoto mzuri nimumwagie midola niliyokuja nayo, ok ciao tuonane badae.
MDADA: Kaka samahani saa hizi ni saaโฆ..
MKAKA: Achana na mimi wewe
Ha ha ha ha haaaaa!!
Angalia kilichotokea baada ya dogo kupewa ada na kuitumia kubeti
Dogo kampigia simu baba yake;
DOGO: Baba katika zile shilingi laki mbili ulizonipa
nikalipe ada nimetumia shilingi alfu 30 kubeti
BABA : Unasema nini we mpumbavu mshenzi
mkubwa? Nimekukanya mara ngapi kuhusu kubeti?
DOGO : Lakini baba
BABA : Lakini baba nini ngoja urudi utaona
ntakachofanya.
DOGO : Nilitaka kukwambia kuwa nimeshinda
shilingi milioni 3
BABA : Ndio hayo ninayosema wewe mpumbavu
sana kwanini hukutumia laki nzima kubeti? Si
ungepata pesa nyingi zaidi? Ngoja urudi niwataarifu
ndugu zako kuhusu uulivyo na akili za kuamua
haraka mwanangu mpenziโฆ
๐๐๐๐๐๐๐๐๐
Recent Comments