SMS Nzuri: Meseji za Vichekesho Vya Wazee
Huyu mchungaji ni noma, cheki alichomwambia pedeshe
Mchungaji kamfuata pedeshe moja maarufu kwa
kumwaga pesa kwenye kumbi za muziki;
MCHUNGAJI: Kijana, tuko katika harakati za
kujenga kanisa, jitafutie nafasi katika ufalme wa
mbingu kwa kuchangia ujenzi huu. Na Mungu
atakubariki zaidi
PEDESHE: Samahani Mchungaji haitakuwa vizuri
mimi kuchangia kanisa, fedha zangu ni haramu,
huwa nazipata kwa utapeli na kuuza madawa ya
kulevya.
MCHUNGAJI: Yote ni heri, pesa yako tutatumia
kwa kujenga eneo la choo we toa tu!!!
Ulevi noma! Angalia huyu mlevi alichomfanyia huyu jamaa usiku! Ungekua wewe ungefanyaje?
Jamaa alikuwa amelaa na mkewe saa tisa ya usiku akastuka baada ya kusikia mtu anabisha hodi kwenda kufungua mlango
Akamkuta jamaa kalewa sana mlangoni kwao
JAMAA: Nini tena mheshimiwa kuamshana saa hizi?
MLEVI: Naomba uje unisukume.
Jamaa akiamini kuwa pengine kuna gari la huyu mlevi limezima jirani akamwambia subiri nikavae viatu. Baada ya kuvaa viatu akatoka na wakaanza kusindikizana na mlevi. Mlevi akaongoza njia
mpaka kwenye mabembea ya jirani akakaa kwenye bembea moja na kumgeukia jamaa na kumwambia.. Okay nisukume basi.
Mambo ya kijijini haya!
Kuishi kijijini kunahitaji moyo sana
..unaenda kuoga, unakumbuka kuwa umesahau sabuniβ¦unaenda kuchukua sabuni kurudi bafuni, unakuta ng’ombe amekunywa maji yote..unaamua kufuata mengne,unarudi unakuta mbuzi kala sabuniβ¦ππππ
Mzee wa kichaga na hela zake. Angalia anachofanya
Mzee moja alikuwa kila usiku anapita mbele ya bank anasimama,kisha anapiga honi,akitoka askari mlinzi,anaondoka.Hilo jambo likamkera sana askari mlinzi, askari akawa na mvizia yule mzee wa kichaga ,siku alipokuja tena akamkamata, akamuuliza kwa nini unakuja unapiga honi kisha unakimbia? Mzee akasema: Haki ya mungu babaangu , Nina pesa zangu ktk account hapa bank naogopa usilale usingizi ndo maana kila siku usiku napita kukuangalia kama umelala!!
ππππππ
Angalia alichojibu huyu mwanafunzi, Ungekua wewe ni mwalimu wake ungemfanyaje?
Mwanafunz alikuwa kila siku anachelewa shule, na kila siku alikuwa anachapwa, basi siku moja mwalimu akaona ngoja amuulize.
Mwalimu: Mbona unachelewa kila siku?
Mwanafunzi: Nakaa mbali mwalimu
Mwalimu: (huku ana hasira akauliza)Mbali mbinguni?
Mwanafunzi: Mbinguni kwa mbeleπππππ
Huyu mwanamke kazidi sasa
Jamaa: Mambo honey, upo ok?
Mrembo: Sipo ok my dear
Jamaa: Una tatizo gani baby?
Mrembo: Nimetoka hospitali kupima, nna mimba.
Jamaa: Weeh usiniletee balaa hiyo mimba imeingiaje wakati huwa tunatumia kinga?
MremboΒ Kwani nani kakwambia mimba ni yako, hebu tuliza mshono huo.
πππππππ
MTATUUA
Maisha ya Pwani ni Shidaaaaah
ππ ππππππ Jamaa kagombana na mkewe, akasusa kulaπ½π¨ kurudi kazini kamkuta mkewe amevaa kanga imeandikwaΒ ukisusa wenzio walaΒ ilipofika asubuhi mke akavaa kanga imeandikwaΒ ukitoka πΆπΆmwenzio anaingiaππ
jamaa akagoma kwenda kazini π¬π¬ mke akabadili kanga na kuvaa iloandikwaΒ nimemdhibiti ndo mana hatokiπ· jamaa akaenda kuomba ushauri kwa rafiki yake akaambiwa twende nyumbsni kwako, walipofika walimkuta mke kavaa kanga imeandikwaΒ ulidhani rafiki yako kumbe adui yakoπ€π€ jamaa akaamua kusafiri siku tano ili kupunguza hasira. Aliporudi akamkuta mke amevaa kanga imeandikwaΒ ni bora nimpe jirani kuliko kiozee ndani
ππππππππππ
hata kama hupendagi ujinga kwa maneno ya kwenye kanga utasanda tu
Tatizo la kukuta nywele kwenye chakula
Hapa ni shida
KUKUTA NYWELE KWENYE CHAKULA SIO TATIZO,TATIZO NI KUWAZA ITAKUWA IMETOKA SEHEMU GANI
π€£π€£π€£π€£π€£π€£π€£π€£
Recent Comments