SMS Nzuri: Meseji za Vichekesho Vya Watu Wote

Wanaume wote ni waaminifu

Hii ni kwa wanaume ila mwanamke anaweza kusoma na kujifunza kuwa wanaume wote ni waaminifu.

Mwanaume mmoja alienda kukata miti kwa ajili ya mkaa, bahati mbaya panga likadondokea mtoni, akaanza kulia sana. Malaika akatokea na kumuuliza kwanini analia. Jamaa akajibu; “Panga langu limedondokea mtoni na ndilo ninalotegemea kuendeshea maisha yangu”.

Malaika akazama mtoni na kuibika na panga la DHAHABU na kumuuliza, ndio hili?

Jamaa: Hapana.

Malaika akazama tena na kuibuka na panga la SHABA na kuuliza, ndio hili?

Jamaa: Hapana.

Malaika akazama tena mara hii akaibuka na panga la CHUMA na kuuliza ndio hili?

Jamaa: NDIYO.

Malaika akafurahishwa sana na uaminifu wake hivyo akampa mapanga yote matatu. Jamaa akafurahi sana.

Siku nyingine jamaa alikuwa anatembea na mkewe njiani ghafla mke akadondokea mtoni, jamaa akaanza kulia. Malaika akatokea na kumuuliza: Kwanini unalia?

Jamaa: Mke wangu kadondokea mtoni na nampenda sana.

Malaika akazama mtoni akaibuka na WEMA SEPETU na kuuliza; “huyu ndiye mkeo?”

Jamaa: NDIYO.

Malaika akakasirika sana na kumuuliza: kwa nini umenidanganya?

Jamaa: Nimesema ndiyo kwa sababu ningesema hapana ungezama tena na kuibuka na AUNT EZEKIEL na ningesema hapana tena ungezama na kuibuka na MKE wangu alafu ningesema ndiyo ungenipa wote watatu!

Sasa mimi maskini sina uwezo wa kuhudumia wote hao, ndio maana nikasema NDIYO kwa Wema Sepetu.

*FUNDISHO*
Wanaume huwa hatusemi uongo bila sababu na inakuwa sababu maalumu kwa faida ya wote.

WANAUME WOTE NI WAAMINIFU. Hii ndiyo kauli mbiu yetu.
😀😀😀😀

Utoto raha..! Angalia hawa watoto wanachokifanya sasa

Leo nimepulizia Air Fresh yenye Harufu ya Pilau nyumbani kwangu sasa watoto wa Jirani wamehamia Mlangoni kwangu ndio wanacheza hapo. Kila nikitoka wananisalimia. Mama yao ndio kanimaliza kabisa nimetoka akaniambia

“Kumbe wewe ni Mpishi mzuri, Hongera”

Imebidi nisirudi nyumbani maana wale watoto wanaweza kuingia ndani kabisa na pilau hakuna.

#UTOTO RAHA 😂

😂😂😂😂👆🏻👆🏻👆🏻

Wachaga kweli kiboko: Mcheki huyu mchaga na mbuzi!!!

Mchaga alinunua mbuzi akamwambia mpishi Nyama nusu ipike pilau na ingine itie kwenye friza. Kichwa fanya supu, miguu fanya mchuzi chukuchuku. Ngozi usitupe tutafanya mswala, utumbo pikia ndizi na mifupa tutawauzia wenye mbwa. Kinyesi kihifadhi kwa mbolea ya bustani.

Mpishi akamuuliza Hutaki na sauti ya mbuzi tufanye ring tone kwenye simu yako? Mchaga akajibu Yesuu! hivi inawezekana? bac fanya hivyo tuwauzie na wengine hiyo ringtone. 😄😄

Shopping Cart
🏠 Home 📖 Reading 🖼️ Gallery 💬 AI Chat 📘 About