SMS Nzuri: Meseji za Vichekesho Vya Vijana
Kama simu yako ina wifi
Kama simu yako ina Wi-fi ujue uko na mke wa mtuΒ ππππππππΌππΌππΌππΌππΌ
Hii ndio ngoma droo kwa wanaume kati ya wanawake
{ NGOMA DROO}
Sikuizi utawasikia wadada wakisema kuachwa na mwanaume asie na pesa nisawa na kuluhusiwa hospital
{Sasa na sisi} wanaume tunasema
Kuachwa na demu mpenda pesa nisawa na kumaliza mkopo benk ππππππ
Wanaume atutakagi ujinga!!!! Wanaume heeeeeeππΎββππΎββππΎββππΎββ
Padri Akimbia wakati wa kuungamisha, chanzo ni hiki
Padri alikuwa amekaa katika confession booth kanisani
peke yake.
Mara kukaingia jamaa mmoja akapiga magoti upande wa
pili, akafanya ishara ya msalaba kisha akaanza kuungama
{confess}
“Padri nimekuja kuungama dhambi zangu, leo nimefanya
dhambi kubwa sana.”
Padri, “Endelea⦔
“Bosi wangu aliniita nyumbani kwake, akaniambia
amegundua nimeiba shilingi millioni 100 kazini. Akasema
nisipozitoa atanipeleka polisi, sa kwa ukweli mi naogopa
kufungwa.
Nikatazama huku na huku nikagundua tuko wawili peke
yetu,nikatoa bastola nikamuuaβ¦.. Yesu atanisamehe?”
Padri: “Utasamehewa.”
“Basi wakati nataka kuondoka nikasikia mlango
unafunguliwa kutazama, Loh! Mke wa bosi, alipoona
kilichotokea akasema anapiga polisi simu.
Kutazama huku na huku nikagundua tuko wawili peke
yetu, nikamuua na yeye piaβ¦ Yesu atanisamehe hilo?”
Padri: “Utasamehewa.”
Nikatoka nje, nikawasha gari niondoke, lakini mlinzi
akakataa kunifungulia, ati amesikia mlio wa
bastola. Nikaona ataniletea kizuizi huyu.
Nikatazama huku na huku nikagundua tuko wawili peke
yetu, nikamuuaβ¦.. Yesu atanisamehe?”
Padri:”Utasamehewa.”
“Nikajifungulia geti mwenyewe nikaenda
nyumbani, wakati napanga kuja kuungama mtoto wa bosi
akabisha hodi, nikawaza mambo gani tena, akasema alirudi
nyumbani na kukuta yaliyotokea akanionesha diary ya
babake, inayoonesha nilikuwa na appointment naye
wakati nilipomuua. Nikamuuliza nani mwingine anayejua?
Akasema ameanzia kwangu kisha anaenda polisi.
Nikatazama huku na huku nikakuta tuko wawili peke
yetu, nikamuuaβ¦.. Yesu atanisamehe na hilo?”
Kimyaaβ¦.
“Padri yesu atanisamehe?”
kimyaβ¦.
Jamaa akatazama kwenye confession booth padri
hayupo, lakini kwenye kona moja akaona kabati la nguo
za mapadri linatikisika. Kufungua akaona padri kajificha ndani anatetemeka huku akitokwa na jasho.
Jamaa, “Sasa baba mbona umekimbia?”
Padri kwa taabu akajibu, “Nilitazama huku na huku
nikagundua tuko wawili peke yetuβ¦β¦.”
Huyu mlinzi bwana
High school Flashback!!
.
Watchman : Amkeni muende morning preps.
Allan : Mimi ni mgonjwa.
Watchman : Unaumwa na nini hiyo?
Allan : Bionomial Nomenclature.
Watchman : Eeh, lala tu kijana. Hiyo kitu ni
mbaya. Imeuwa watu South Africa.
ππππππππππ
#_Sipendagii ujinga kabisaa mimi
Huu ndio mlolongo wa michepuko kuwahi kutokea kati ya mke, mume mwanafunzi na boss
BOSS anamwambia sekretari wake: Wiki hii tutaenda wote Serena Hotel kwenye mkutano fanya mipango yote.
SEKRETARI (anamuaga mumewe): Tunaenda na bosi Serena hotel kwenye mkutano for 1 week.
MUME (anampigia mpango wa kando): Mambo safi, wife anaenda kikazi Serena, jitayarishe tujipe raha for 1 week
(Mpango wa kando) anamwambia mwanafunzi wake wa tution: wiki hii nina kazi fulani hakuna tution mpaka week ijayo.
MWANAFUNZI anampigia simu sugar daddy wake ambaye ndo (BOSS): Dear hakuna tution wiki hii nakuja kwakoβ¦..
BOSS anamwambia sekretari wake: Siendi Serena tena coz mjukuu wangu atanitembelea.
SEKRETARI: Mume wangu hatuendi Serena
MUME (anampigia Mpango): dah! mpenzi, huyu mke wangu haendi tena. Shit! So hadi next time plz
Mpango wa kando a.k.a teacher (anampigia mwanafunzi): Darasa kama kawaida sorry for the earlier message.
MWANAFUNZI: darling tution inaendelea kumbe, so nakuja wiki ijayo!!
BOSS: Sekretari sorry jitayarishe ile safari ya Serena iko palepaleβ¦β¦
Mambo ya pesa haya..
MAMBO YA FEDHA AISEEβ¦β¦. Kuna jamaa alipewa shilingi 983628763600/= β¦acha uvivu, najua hujasoma ni kiasi gani hicho cha fedha na mbaya zaidi hujagundua kwamba katikati ya namba hizo kuna herufi Aβ¦ safi sana, najua umeangalia tena kuiona hiyo herufi, bahati mbaya hujaiona. πππππππ
Huyu jamaa bonge la bwege, ungekua wewe ndiyo rafiki ake ungemwambiaje?
RAFIKI: Vipi mbona leo huna uchangamfu
JAMAA: Wanawake bwana, mwanamke hata umpendeje atakugeuka tu
RAFIKI: Nini tena ndugu yangu? Mbona shemeji mtu fresh sana
JAMAA: Hata mimi nilikuwa najua hivyo, leo nimegundua kumbe ana siri kubwa sana
ananificha, mi naita huu ni usaliti wa ndoa.
RAFIKI: Nini tena?
JAMAA:Nimegundua mke wangu kumbe anafanya biashara ya kitimoto na hajawahi hata kuniambia
RAFIKI: Kitimoto? We umejuaje?
JAMAA: Leo asubuhi nilichelewa kuamka niliamua nijipumzishe kidogo kabla ya kwenda kazini, simu ya mke wangu ikalia, nikaamua kuipokea, kabla hata sijafungua mdomo, nikasikia sauti ya mwanaume mmoja akauliza, βHuyo nguruwe umeshamuondoa?β Hebu we fikiria nilivyoshtuka, yaani mpaka sasa nashindwa kuamini kuwa mke wangu ananizunguka anafanya biashara ya nguruwe hajaniambia hata siku moja
Angalia nilichomjibu huyu kuhusu kabila langu
Kuna mtu kanikeraΒ et nmemkubalia urafiki Leo tuΒ Facebook anataka kujua kabila langu
Bac akajifanya mjanjaa etΒ akaniuliza mbu kwenu mnawaitaje
Mimi nkamjibu hatuwaiti wanakujagaΒ wenyewe
πππππππ
Si kwamba cjamuelewa ila sipendagi Ujinga Mimi
Kilichotokea kwa binti na mvulana wake walipotaitishwa na baba yake msichana
Msichana alikuwa amekaa na baba yake kibarazani, mara akamuona MVULANAfriend wake akija, yule mvulana alipokaribia tu, yule msichana akamwambaia:
MSICHANA: Umekuja kuchukua kile kitabu chako, kinachoitwa “DADDY IS AT HOME?” by Ngozi Okafor
MVULANA: Hapana!, Nimekuja kuazima kitabu cha Maombi kama kinaitwa “WHERE SHOULD I WAIT FOR YOU?” by NgΕ©gΔ© wa Thiong’o
MSICHANA: Aaah! Icho sina ila ninacho kimoja kinaitwa “UNDER THE MANGO TREE” by Chimamanda Adichie
MVULANA: Ooh! Vizuri, Basi usisahau kuja nacho kesho kitabu cha Okot p’Bitek kile kinachoitwa “CALL ME IN 5 MINUTES BEFORE” Utakapokuja shule.
MSICHANA: Usijali, tena nina kitabu kipya kinaitwa “I WON’T LET YOU DOWN” by Chinua Achebe
Baba mtu akawatazamaaaa kisha akasema
BABA: Vitabu vyote hivyo, mbona vingi sana, atavisoma vyote kweli
MSICHANA: Ndio Daddy, huyu mvulana hupo smart sana na ana akili atavisoma vyote hivyo!
BABA: Sawa! Usisahau kumpatie na kile ambacho nimekiweka pale juu ya meza, kinaitwa “I AM NOT STUPID, I UNDERSTOOD EVERYTHING YOU’VE BEEN SAYING” by Shakespeare!
Na kuna kingine nimekiweka juu ya kabati la vyombo, kinaitwa “IF YOU GOT PREGNANT PREPARE TO GET MARRIED”
Recent Comments