SMS Nzuri: Meseji za Vichekesho Vya Mchana Huu
Omba omba sio barabarani tuu
Boy:- baby ivi nikifa utakuja msibani?
Girl:-ntakuja ukinitumia nauli.
Hapo ndo unagundua kuwa sio kila omba omba yuko barabarani.
🤒🤒🤒🤒🤒🤔
Read and Write CommentsTofauti ya ukopaji wa mzungu na mswahili
MZUNGU: Hi, I need $100, will pay back on Monday
MSWAHILI: Kaka vipi, shwari? Dah.. hatuonani mzee, mishe vipi, mnatunyima nini? Juzi nimekuona kwa mbaaali… mzee shavu dodo, full kipupwe! Sie tupo bwana, shida tu, afu misiba mingi tu, wife nae kajifungua ghafla. Sasa, kuna cheque naisubiri haijatoka hadi leo, wanasema itatoka next week, hapa nimekwama kweli. Naweza pata ‘Laki Moja’ ya karibu hapo nitarudisha mwisho wa mwezi…?😂😂😂😂😂
Read and Write CommentsAngalia huyu house girl wa mzungu alichokifanya na anachokisema
House girl mmoja alipewa kazi na mzungu mara akavunja sahani.
Mzungu aliporejea,kazin akamuuliza ‘what happened to my plate?
House girl akajbu: ‘The dog wow wow friji paaa, mchuzi mwaaaa the vyombo pangalapangala the sahan ngelengenjee……the pasuka paaaaaaaa
😂😂😂😂hadi saiz mzungu bado anasoma dictionary hajui lugha gani imetumika
Sitasahau mwaka huu
Sitasahau mwaka ule ambapo nilipeleka barua ya maombi yangu ya kazi kwenye kampuni moja maarufu. Wakati nasubiri majibu siku moja nikaenda kwa mama ntilie kununua maandazi akanifungia vizuri, kufika nyumbani hamu yote ya maandazi iliniishia pale nilipogundua karatasi iliyofungiwa maandazi ni barua yangu ya kuombea kazi😂😂
Read and Write CommentsHawa Machizi wamezidi sasa
Chizi kakaa ukingoni mwa bahari analia kwa masikitiko na huku kakamata kijiko cha chai. Mwezake akamuuliza mbona unalia mwenzangu. Chizi akajibu nimetia vijiko vitatu vya sukari baharini, kila nikionja bado ina chumvi. Mwenzake akacheka sanaaaaaa akamwambia. Hujakoroga!!!!😂😂😂😂😂😂
Read and Write CommentsSoma hii, Nani haelewi kati ya hawa?
Dogo: Bro naomba nitumie hela.
Bro: Tumia tu mpaka uchoke.
Dogo: Hujanielewa,nitumie hela.
Bro: We ndo hunielewi, nimesema tumia tu…!!!
Read and Write CommentsMambo ya pesa haya..
MAMBO YA FEDHA AISEE……. Kuna jamaa alipewa shilingi 983628763600/= …acha uvivu, najua hujasoma ni kiasi gani hicho cha fedha na mbaya zaidi hujagundua kwamba katikati ya namba hizo kuna herufi A… safi sana, najua umeangalia tena kuiona hiyo herufi, bahati mbaya hujaiona. 😜😜😜😜😜😜😜
Dongo kwako kama una degree moja Halafu unachagua kazi
Mtu una degree 1 unachagua kazi! Wakati thermometer ina degree 100, inafanya kazi kwenye kwapa.
😃😄😆😆😆
Ni Utani tuuuuu!
Mcheki Chizi na daktari
Tafakari na ujumbe huuuu!!!…
DAKTARI :- Unajisikiaje?
CHIZI:-Kila siku naota nyani wanacheza mpira wa miguu.
DAKTARI :- Nitakupa dawa leo hautaota tena.
CHIZI:-hiyo dawa nipe kesho sababu leo wanacheza fainali. na nilibet
😂😂😂😂