SMS Nzuri: Meseji za Vichekesho Vya Kukupa Mudi Mpya
Padri Akimbia wakati wa kuungamisha, chanzo ni hiki
Padri alikuwa amekaa katika confession booth kanisani
peke yake.
Mara kukaingia jamaa mmoja akapiga magoti upande wa
pili, akafanya ishara ya msalaba kisha akaanza kuungama
{confess}
“Padri nimekuja kuungama dhambi zangu, leo nimefanya
dhambi kubwa sana.”
Padri, “Endelea⦔
“Bosi wangu aliniita nyumbani kwake, akaniambia
amegundua nimeiba shilingi millioni 100 kazini. Akasema
nisipozitoa atanipeleka polisi, sa kwa ukweli mi naogopa
kufungwa.
Nikatazama huku na huku nikagundua tuko wawili peke
yetu,nikatoa bastola nikamuuaβ¦.. Yesu atanisamehe?”
Padri: “Utasamehewa.”
“Basi wakati nataka kuondoka nikasikia mlango
unafunguliwa kutazama, Loh! Mke wa bosi, alipoona
kilichotokea akasema anapiga polisi simu.
Kutazama huku na huku nikagundua tuko wawili peke
yetu, nikamuua na yeye piaβ¦ Yesu atanisamehe hilo?”
Padri: “Utasamehewa.”
Nikatoka nje, nikawasha gari niondoke, lakini mlinzi
akakataa kunifungulia, ati amesikia mlio wa
bastola. Nikaona ataniletea kizuizi huyu.
Nikatazama huku na huku nikagundua tuko wawili peke
yetu, nikamuuaβ¦.. Yesu atanisamehe?”
Padri:”Utasamehewa.”
“Nikajifungulia geti mwenyewe nikaenda
nyumbani, wakati napanga kuja kuungama mtoto wa bosi
akabisha hodi, nikawaza mambo gani tena, akasema alirudi
nyumbani na kukuta yaliyotokea akanionesha diary ya
babake, inayoonesha nilikuwa na appointment naye
wakati nilipomuua. Nikamuuliza nani mwingine anayejua?
Akasema ameanzia kwangu kisha anaenda polisi.
Nikatazama huku na huku nikakuta tuko wawili peke
yetu, nikamuuaβ¦.. Yesu atanisamehe na hilo?”
Kimyaaβ¦.
“Padri yesu atanisamehe?”
kimyaβ¦.
Jamaa akatazama kwenye confession booth padri
hayupo, lakini kwenye kona moja akaona kabati la nguo
za mapadri linatikisika. Kufungua akaona padri kajificha ndani anatetemeka huku akitokwa na jasho.
Jamaa, “Sasa baba mbona umekimbia?”
Padri kwa taabu akajibu, “Nilitazama huku na huku
nikagundua tuko wawili peke yetuβ¦β¦.”
Cheki huyu mtoto anachosema
sijui hili toto langu nilipeleke wapi, Leo limetoka shule eti nikaliuliza BIBILIA kwa kingereza inaitwaje likaniambia GRANDMOTHER CRY
π π π sijui nikabadilishane na kijiko cha chumviπ€π€π€
Huu ndio mlolongo wa michepuko kuwahi kutokea kati ya mke, mume mwanafunzi na boss
BOSS anamwambia sekretari wake: Wiki hii tutaenda wote Serena Hotel kwenye mkutano fanya mipango yote.
SEKRETARI (anamuaga mumewe): Tunaenda na bosi Serena hotel kwenye mkutano for 1 week.
MUME (anampigia mpango wa kando): Mambo safi, wife anaenda kikazi Serena, jitayarishe tujipe raha for 1 week
(Mpango wa kando) anamwambia mwanafunzi wake wa tution: wiki hii nina kazi fulani hakuna tution mpaka week ijayo.
MWANAFUNZI anampigia simu sugar daddy wake ambaye ndo (BOSS): Dear hakuna tution wiki hii nakuja kwakoβ¦..
BOSS anamwambia sekretari wake: Siendi Serena tena coz mjukuu wangu atanitembelea.
SEKRETARI: Mume wangu hatuendi Serena
MUME (anampigia Mpango): dah! mpenzi, huyu mke wangu haendi tena. Shit! So hadi next time plz
Mpango wa kando a.k.a teacher (anampigia mwanafunzi): Darasa kama kawaida sorry for the earlier message.
MWANAFUNZI: darling tution inaendelea kumbe, so nakuja wiki ijayo!!
BOSS: Sekretari sorry jitayarishe ile safari ya Serena iko palepaleβ¦β¦
Hii sasa kali kweli kweli!!
MCHUNGAJI alitangaza kila mwanaume aliye na mke atoe sadaka kulingana na uzuri wa mke wakeβ¦bac watu wakaanza kutoa 50,000/= 30,000/= na 20,000/=.
Kuna jamaa akatoa 500/=.
MCHUNGAJI akamuita ofisin akamuuliza.
MCHUNGAJI:Ina maana mkeo siyo mzuri?. Jamaa akajibu: Ukimuona utanirudishia na chenji.
ππππππππππ
Sababu ya girlfriend π§ kuniblock
Nimeblockiwa bila kosa X Girlfriend From no where kanitext eti Hi; Vp na huko kwenu mvua inanyesha β¦Nimemjibu kwani nimekutumia text ina matope?
sipendangi ujinga mimi
Huyu jamaa kawaweza wapenda vya bure
Jamaa kaingia mgahawani kwa fujo
JAMAA :Β Nipe soda moja na kila mtu mpe yake maana ninapokunywa soda napenda kila mtu anywe
WATU :Β Ha! Ha! Ha! Haaaa!
JAMAA :Β Nipe mchemsho na kila mtu mpe wa kwake maana ninapokula mchemsho napenda kila mtu ale wake
WATU:Β Watu weweeee! Tena safari hii Na makofi juu..
JAMAA :Β Mhudumu, nipe bili na kila mtu mpe yake maana ninapolipa bili napenda kuona kila mtu analipa yake
πππππππ
Angalia huyu mke wa mtu anavyojichanganya hadi kwa mme wake
MUME: “Mke wangu nasikia John katembea na wake za watu wooote hapa mtaani kasoro mmoja tu!”
MKE: “Mmmh! basi huyo aliebaki atakuwa MAMA MBILINGE KISIKI, maana yule mama ndo ANAJIFANYAGA MGUMU sanaaa.!!”
Je, huyu mama angekuwa mkeo ungekuwa na swali lingine la kumuuliza?
Ujinga wa ndoto ndio huu
πUjinga wa ndoto ndiyo huu
β’β’Utaota umeokota dolla ukiamka emptyβ¦
β’β’Utaota umeokota dhahabu ukiamka kitandani patupu daadeeki OTA Sasa UMEKOJOAβ¦..
ππππππ
BREAKING NEWS!!! Nyoka wa ajabu agundulika
HABARI MPASUKO..
jana katika taasisi ya wanyama pori ya Nat Geo ilitangazwa kuwa ametokea Nyoka hatar san Ambaye hajawah kutokea duniania.. wanadai kwamba nyoka huyo anaongezeka ulrefu wa 0.5sm kila akila chakula na huwa anakula chakula kuanzia sekunde 30 kurudi nyuma.. mpaka sasa hakuna siraha ya kuweza kumuua nyoka huyo isipokuwa akiji uma mwenye ndo anaweza kufa, wanasayansi hao walieleza japo uchunguz zaid bado unaendelea⦠huyu ni nyoka anayeua kuliko nyoka wote waliowah kutokea katika historia ya maisha ya mwanadam..
nyoka huyu hupatikana katika simu pekee za nokia toch katika sehem ya game inaitwa snake xenzia..
asanteni kwa kufurah na umakin mkubwa katika usomaji wa matini hiiβ¦
haya ni mambo ya wikiend jaman na iwe njema kwenu wote
Recent Comments