SMS Nzuri: Meseji za Vichekesho Vya Krismass
Je, hii ni kweli kwa wale wasichana wasiojibu meseji WhatsApp!!!?
Ukiona hivyo ujue ndio hivi
Mwanaume mwenzangu ukiona unamtext msg msichana WhatsApp kaisoma hajajibu, umetuma ya pili kasoma hajajibu, ukatuma ya tatu hajajibu mmmmmhπ¨π¨ hapo ujue mwenzio kaangalia kwenye profile yako, kakagua picha weee mwishoni akajisemea tuΒ “Huyu.mkaka hapana kwa kweli”π€£π€£π€£π€£π€£π€£
πββπββπββπββπββπββ
Nilichokifanya leo
Leo nmemlipa konda nauli, akasahau kunishusha kituoni. Na mimi nkakaa KIMYAAA kumkomoaβ¦..
*nataka ujinga kwan mimiπππ*
Sahv narudi zangu kwa mguuπ©
Kingereza sio mchezo, angalia huyu anavyojichanganya
Jamaa fulani alikuwa ame2lia beach mzungu akapita akamuliza “Are u relax ? Jamaa akawa hamuelewi akamjibu No! Mzungu mwengine akapita akamuliza vilevile akajibu No!
Akaona hapa anasumbuliwa akasogea mbele kidogo ya maji akamuona mzungu mmoja alikuwa ame2lia. Akamuliza “are u relax? Mzungu akajibu yes jamaa akamkata makofi mawili na kumwambia kumbe we ndo relax inuka unatafutwa na wenzakoβ¦..Shenz mkubwa mie nasumbuliwa na wenzako kule we umejikausha!!
Ziara za kushtukiza zinachekesha sana
Mimi Nimecheka sana
ππππππππππ
ZIARA ZA KUSHTUKIZAππ
Mimi ni msomaji mzuri wa magazeti, na msikilizaji mzuri wa redio, huwa naangalia luninga mara chache sana kama nikibahatika kupita mahala kuna luninga. Sasa wiki hii nimesikia mengi kuhusu hizi ziara za kushtukiza za viongozi wetu, nikaona hili ni jambo zuri tena linafaa kuigwa na sisi wananchi wapenda maendeleo. Nikaona nijipange na mimi nifanye ziara kadhaa za kushtukiza katika sehemu mbalimbali zinazonihusu.
Nikaona nianze na ziara ya kushtukiza pale shuleni kwa huyu mwanangu, maana kila siku anakunywa chai na kuondoka na daftari zake na mie sijawahi kwenda shuleni kwao toka nilipomuandikisha shule mwezi Januari. Nilifika shuleni na kumuona mwalimu mkuu, ambae alianza kutetemeka nilipomuambia kuwa nimekuja pale kwa ziara ya kustukiza, sijui alidhani mi ni mmoja wa Mawaziri wapya, maana nilimuona jasho linamtiririka ghafla. Akanikaribisha ofisi yake iliyokuwa na vitabu kila kona, na kuita waalimu wote na kunitambulisha kuwa ni kiongozi nimekuja kwenye ziara ya kustukiza.
Nilipojitambulisha kuwa ni mzazi, waalimu wote nikawaona waanza kupumua kwa raha. Nikawaambia kuwa mimi nina mwanafunzi pale na nilikuja ziara ya kustukiza kujua maendeleo yake. Baada ya mwalimu mkuu kusaka jina la mwanangu nae akanambia, βMzee huyu mtoto hajaja shule mwezi wa tatu sasa, tulijaribu kukutafuta ikashindikana, hatujui yu wapiβ Jasho likaanza kunitoka mimi, yule mtoto kila asubuhi nampa nauli anaenda shule, na mara nyingi ananiomba michango kumbe hata shule haji. Niliondoka bila kuaga presha ikiwa juu.
Nikaona niende kwenye genge la mke wangu nae nikamfanyie ziara ya ghafla nimhadithie mambo ya mwanae, nilipofika pale nikakuta kuna mdada mwingine anauza genge. Nikamsalimu, na kumuuliza mwenye genge ntampataje, jibu lake lingeniua kama ningekuwa si mkakamavu, βMume wake kaja kumchukua na gari wameenda kununua shamba Bagamoyoβ. Nikaondoka nimechanganyikiwa, nikajuwa hapa dawa yangu moja tu, nayo ni Sabrina, mtoto wa Kinyaturu pale ambapo nikipata maudhi huwa naenda kubembelezwa.
Nikatwanga mguu kwa Sabrina nae nikamfanyie ziara ya ghafla ili anipoze moyo. Nilipogonga mlango wa chumba chake akatoka mbaba wa miraba minne, akanisalimia kwa upole, βSalama kaka unasemaje?β Jibu likanitoka βSamahani mie nilimkopesha huyu dada wa chumba hiki vitenge, nilikuja kuuliza kama ameshapata hela yanguβ Ziara za kushtukiza zinataka moyo wa chuma jamani
Huu ndio Umuhimu wa English katika mapenzi
HUU NDO UMUHIMU WA ENGLISH KATIKA MAPENZI
jaribu kumwita mpenzi wako “my sweet potato” atakuelewa ila mwite kwa kiswaili ” *kiazi wangu mbatata*”hiyo itakuwa vita ya tatu ya duniaππ
Angalia sababu ya mke Mtarajiwa kuzimia kabla ya harusi
*Jihadharini* na wachapaji wa kadi za harusi. Hakikisha unasoma maandishi yaliyochapwa kabla ya kadi kuchapwa na kusambazwa!
Mchapaji aliombwa aweke 1 Yohana 4:18 katika kadi ya harusi lakini mchapaji kwa makosa aliweka Yohana 4:18.
1 Yohana 4:18 panasema, “Katika pendo hakuna hofu, lakini pendo lililo kamili huitupa nje hofu⦔
Lakini Yohana 4:18 tunasoma, “Kwa maana umekuwa na waume watano, naye uliye naye sasa siye mume wako.”
πππππππππππ_MKE MTARAJIWA AKAZIMIA HAPA, TUNAMPEPEA_
Huyu mwanamke kazidi sasa
Jamaa: Mambo honey, upo ok?
Mrembo: Sipo ok my dear
Jamaa: Una tatizo gani baby?
Mrembo: Nimetoka hospitali kupima, nna mimba.
Jamaa: Weeh usiniletee balaa hiyo mimba imeingiaje wakati huwa tunatumia kinga?
MremboΒ Kwani nani kakwambia mimba ni yako, hebu tuliza mshono huo.
πππππππ
MTATUUA
Usichokijua kuhusu sungura, panya na jamii yao
JE WAJUA?
Sungura, panya na Jamii zao huwa na mwendo wa kukimbia na kuruka muda wote na umri wao wa kuishi ni miaka 15. Kobe ni mnyama mwenda pole, asiye na papara wala pilika, muda mwingi hujificha na kupumzika ndani ya jumba lake akikwepa maadui. Umri wa kuishi kobe hufikia hadi miaka 300.
FUNZO: Mazoezi ni kiinimacho na uongo mtupu. Jipumzikie mwaya!!!
ππΎππΏβ
Wasichana wa leo
Jamaa yupo ndani ya Range rover yake mpya na msichana ambaye ni mpenzi wake.
#Jamaa: kuna siri flani nimeitunza moyoni mwangu kwa muda mrefu na nikaona kama nitakuambia lazima utaniacha.
#Msichana: siri gani hiyo mpenzi wangu?
#Jamaaa: nimeoa.
#Msichanaa: HΙΙΙΙΙΙΙΙ! We umenishtua sana,mm nilifikiri hili gari sio lako!
πππ€π€
Recent Comments