SMS Nzuri: Meseji za Vichekesho Vya Jumanne
Eti ni kweli hii ni sababu wanaume wana Upendo Sana?
Wanaume wana upendo kwa kweli.
Mwanaume hata akipewa kundi la wanawake 90 achague mmoja!! Hata akichagua mzuri kupita wote bado roho itamuuma kuwaacha wale 89 waliobaki!!*
Kwa namna hii wanaume wana Upendo Sana
๐๐๐๐๐๐
Ungekua wewe ndio baba wa Huyu mtoto ungemjibu nini?
MTOTO: Hivi Baba wewe umezaliwa wapi?????
BABA: Mbeya
MTOTO: Mama nae kazaliwa wapi????
BABA: Tanga
MTOTO: Mimi jee?????
BABA: Dar
MTOTO: Sasa tulikutanaje????
๐๐ hapo wee kama baba ungemjibuje mwanao๐ณ๐ณ๐ณ
Duh. Chezeya kuhama!
Pale imebaki siku moja uhame kwenye nyumba ya kupanga af unakuta umebakiza unit 60 za umeme, inabidi tu uchemshe maji hadi yale ya kuflashia choo
๐ก๐ก๐ก๐ก๐ก
Huu ndio Umuhimu wa English katika mapenzi
HUU NDO UMUHIMU WA ENGLISH KATIKA MAPENZI
jaribu kumwita mpenzi wako “my sweet potato” atakuelewa ila mwite kwa kiswaili ” *kiazi wangu mbatata*”hiyo itakuwa vita ya tatu ya dunia๐๐
Sifa 10 za mwanaume ambaye kila binti anayetaka aolewe angependa aolewe naye!!
1. Awe na pesa nyingi
2.Siyo lazima awe mzuri wa sura
3. Ajenge ukweni
4.Awe mpole
5.Asimuonee wivu mke wake
6.Awe mwenye upendo wa dhati
7.Asishike simu ya mke wake.
8.Akimkuta na mwanaume apite tu, akitaka kujua ni nani asubiri nyumbani
9.Awe anamskiliza mke wake kwa kika kitu.
10.Asipende mwanamke mwingine zaid yake
UKIMPATA MWANAUME MWENYE SIFA HIZO KAPIME DNA LAZIMA ATAKUWA NI BABA AKO.
๐๐๐๐๐๐๐๐
Utajuaje kama unachoangalia ni filamu ya kibongo!!!!
Angalia hivi
-Mlinzi wa Getini lazima awe chizi
-Mtu yupo kijijini, maisha magumu ana Wave
kichwani.
-Kama bosi atakuwa na kampuni basi ni lazima
itakuwa ya Clearing and Forwading au ya uuzaji
Magari.
-Lazima waende Kununua nguo.
-Jambazi lazima avae koti lefu jeusi na Miwani.
-Mtu akichapwa kofi huangukia kwenye kochi
ama kitandani.
-Actress huwa hawapiki hata chai.
-Kwa mdada akiishi maisha ya kitajiri lazima
avae nguo inayoishia mapajani.
-Actress even after 5 yeas utakuta staili ya
nywele na rangi za kucha ni zile zile.
-Anaweka Sumu alafu anaonja kama imekolea.
-Movie zote wapenzi huitana Baby..
-Main actor wote ni wafanya biashara na lazima
wataongelea mizigo kutoka bandarini.
-Wakinywa Soda basi lazima wabakishe.
Angalia nilichomjibu huyu kuhusu kabila langu
Kuna mtu kanikeraย et nmemkubalia urafiki Leo tuย Facebook anataka kujua kabila langu
Bac akajifanya mjanjaa etย akaniuliza mbu kwenu mnawaitaje
Mimi nkamjibu hatuwaiti wanakujagaย wenyewe
๐๐๐๐๐๐๐
Si kwamba cjamuelewa ila sipendagi Ujinga Mimi
Hawa Machizi wamezidi sasa
Chizi kakaa ukingoni mwa bahari analia kwa masikitiko na huku kakamata kijiko cha chai. Mwezake akamuuliza mbona unalia mwenzangu. Chizi akajibu nimetia vijiko vitatu vya sukari baharini, kila nikionja bado ina chumvi. Mwenzake akacheka sanaaaaaa akamwambia. Hujakoroga!!!!๐๐๐๐๐๐
MAMBO KUMI YA KUFURAHISHA NA HUWEZI KUYAFANYA
1. Huwezi kuosha Macho kwa Sabuni;
2. Huwezi kuhesabu Nywele zako;
3. Huwezi kupumua kwa Pua na huku umetoa Ulimi;
4. Unajaribu kufanya namba 3
6. Umeona inawezekana, sanasana unakuwa Kama Jibwa;
7. Unatabasamu kwa kuwa umejiona Mjinga!
8. Umeruka namba 5;
9. Unahakikisha Kama kweli 5 haipo.
10. Unacheka kwa kuwa nimekubamba!
Recent Comments