Wadada lenu hili. Mimi sipo
Wadada kama una sura mbaya subiri NEEMA YA BWANA..Sio kutuambia mna uzuri wa Ndani usioonekana..Sisi ni Wanaume,Sio MINYOO
๐๐๐๐
๐๐๐๐
WIFE: Baibie, yule ni nani? Ni Chris Brown??
HUSBAND: Yule ni Theo Walcott
WIFE: ile Yellow Card ni ya nini?
HUSBAND: ile ni ya Onyo, na Red Card inamaanisha mchezaji awache kucheza na atoke inje ya uwanja.
WIFE: Oooooh! Inakaa kama traffic light! Yellow- Ilani na Red – Simama
HUSBAND: Yeah yeah swity! Ndio hivyo.
WIFE: Na je Green Card??
HUSBAND: Aaaah! Hakuna kitu kama hicho.
WIFE: Nataka Arsenal ishinde world cup.
HUSBAND: [kimya]
WIFE: Ni nani yule mzee anakaa kama Mr. Bean??
HUSBAND: Yeees swity, yule ni kocha wa Arsenal, anaitwa Arsene Wenger.
WIFE: Oooooh! inamaanisha yule kocha mwengine ni Chelsea Wenger??
HUSBAND: [Kabadilisha channel]
Hapa mtaani kuna mwizi sugu ameshinda mil.10 za bahati nasibu ??.
Alipoulizwa atafanya nini na hela nyingi hizo
Akasema anataka kupanua shughuli zake. Mimi sijamuelewa na sasa hivi watu wameanza kuhama mtaaโฆ
๐๐
Basi juzi kati hapa sehemu ndogo ya ukuta wa Ikulu ya Magogoni ilianguka!..
Wakapelekwa contractors watatu ili achaguliwe mmoja atakayejenga vzr na kwa bei nafuu!..
Wakwanza alikuwa MUHINDI, wa pili MCHINA na MBONGO!โฆ
MUHINDI: “ntajenga kwa milioni 90!.., 40 za vifaa, 40 za mafundi na milioni 10 faida yangu”
MCHINA: “mi ntajenga kwa milioni 70!.., 30 za vifaa, 30 za mafundi na milioni 10 faida yangu”
MBONGO kuona vile akamvuta chemba msimamizi wa Magogoni!..
MBONGO: “mi ntajenga kwa milioni 270”
MSIMAMIZI WA MAGOGONI: “we una wazimu nn!.. yaani unathubutu kusema hivyo na unaona wenzako wametaja kiwango kidogo?!.”
MBONGO: “milioni 100 zako, 100 zangu alafu hiyo milioni 70 tunaajiri yule mchina”
Mama mkwe alimuuliza mkwewe “binti” samahani mbona mtoto hajafanana na mwanangu kabisa?
Binti akajibu, “bila samahani mama huku chini nina njia ya uzazi sio mashine ya photocopy”
mama mkwe hoii!! Chezea Wakwe Wa Bongo wewe.
Wanafunzi waliulizwa na mwalimu nani angependa kwenda peponi? Wote wakanyosha ila mmoja tu alipokwenda nyumbani akamuelezea mamake, mamake akamuuliza je wewe ulinyosha mtoto hapana mama yule mama akamuuliza kwanini.
mtoto kwa sababu mama uliniambia nikitoka shule nije moja kwa moja mpaka nyumbani nisiende kokote
1.Mwenye mpira Lazima acheze ata kama hajui mpira
2.Dogo mnene Lazima awe golikipa
3.Mwenye mpira ataamua nan acheze na nan asicheze
4.kama haujashiriki kufuma mpira unaweza ucpate namba
5.Ukichaguliwa mwishon ujue uwezo wako ni mdogo kuliko wote
6.Mwenye mpira akikaclika mpira umeisha
7.Inaruhusiwa kubadili golikipa kama ikitokea penat na baada ya apo ataendelea kudaka yule yule
8.Mechi itaisha pale giza linapoingia
9.wale ambao wamekosa namba kazi yao ni kufata mpira ukitoka
10.yule mtaalam wa soka {KM MIMI } huwa hakoc namba ata cku moja!
Ukiikumbuka lazima utabasam!
Kuna maprofesa 40 walipanda AIR TANZANIA ili wasafari. Kabla ndege haijaanza kuondoka, Lilipita tangazo kama ifuatavyo:
Ndugu wasafiri wote, ndege unayotarajia kusafiri nayo imetengenezwa na wanafunzi wa Kitanzania.
Baada ya tangazo maprofesa wote waliteremka isipokuwa mmoja alibaki kwenye kiti chake
Walipomuuliza ni kwanini hakuondoka akajibu kwa haraka na furaha kuwa:
Kama ndege hii imetengenezwa na watanzania, hata kuwaka haitawaka!
Hiki ndiyo kifo.
๐๐๐๐
Jamaa mmoja dereva wa bajaji alianguka, sasa bajaji ikawa imem’bana akawa anafurukuta bila mafanikio Cha ajabu watu wakawa wanampita bila kumsaidia, Kumbe Nyuma ya Bajaji yake alikua Kaandika “NIACHENI KAMA NILIVYO, HII NDIO STYLE YANGU”ย ๐๐๐ย Mpaka sasa nimemwacha bado yuko hapoย *Sipendagi Ujinga mimi* ๐ถ๐ฝ๐ถ๐ฝ๐ถ๐ฝ๐ถ๐ฝ๐ถ๐ฝ
Kasuku alisimama mlango wa kuingia supermarket wakapita wanawake watatu akasema nyeupe, nyekundu, kijani. Wale wanawake wakatatizika baada ya mda wakajua ni chupi walizovaa. Wakasema basi kesho tubadilisheni. Siku ya pili wakapita tena kasuku akasema nyeusi, manjano, zambarau. Loh! Wanawake wakastaajabu sana. Wakasema lazima wamshinde yule kasuku kwa hekima. Wakaambiana basi kesho tusivae chupi tuone kama ni kweli anaona mpaka ndani. Siku ilipowadia wakapita mbele ya kasuku akasema- kipilipili, kipara, rastaโฆ
1) gari la kuvutwa halina overtake
2) kisigino hakikakai mbele
3) wimbo wa taifa haupgwi disko
4) feni haiwashwi beach
5) mshkaki hauchomwi kwa jiko la ges
6) mganga haagiz tembele
7) hata bibi alikuwa bint
8) mke wa mtu sumu,mume wamtu maziwa
9) kipara bila pesa ni kovu
10) mbwa hanenepi migiuu
11) picha ya rais haina bodyguard
12) mjini shule kijiji tuition
13) saa ya ukutani haivaliwi mkonon
14) heshima pesa shkamoo makelele
15) ulinz pesa bastora mzgo
16) kuku ni kuku jogoo mbwembwe
17) kusoma kuelewa kukesha mbwembwe
Jamaa mmoja alialikwa ktk harusi. Akafika mlango Wa 1 umeandikwa kulia ni ndugu Wa maharusi, kushoto ni wageni waalikwa, akaenda kushoto maana yy alialikwa. Akakuta mlango wa2 umeandikwa kulia wenye zawadi kushoto wasionazawadi yy hakuwa na zawadi. Mlango Wa 3 umeandikwa kulia wanawake kushoto waume akapita kushoto akajikuta ametokea mtaani
๐๐๐๐๐๐๐๐. Tujifunze kutoa wandugu
*hatupendagi ujinga sisi*
๐ถ๐ฟ๐ถ๐ฟ๐ถ๐ฟ๐ถ๐ฟ๐ถ๐ฟ๐ถ๐ฟ๐ถ๐ฟ
Recent Comments