Ujumbe mzuri kwa umpendaye
kiangazi aumasika
kukupenda nitawajibika kwenye chupa au birika chai yako
ya uhakika ,iwe ndoo au pipa ujazo wa penzi kimiminika.
kiangazi aumasika
kukupenda nitawajibika kwenye chupa au birika chai yako
ya uhakika ,iwe ndoo au pipa ujazo wa penzi kimiminika.
Salamu yako ni nusu ya uhai wangu, kuikosa nisawa na kuidhulumu nafsi yangu, kuipata nisawa na ua ridi machoni mwangu, nakila ninapoipata huwa najisikia faraja moyoni mwangu, Nakupenda sana Muhibu wangu.
Penzi lako ndiyo pumzi yangu nawezaje kukuacha laazizi,
ina maana nife??? Siwezi kukuacha nakupenda. Nitakupenda
mpaka mwisho wa uhai wangu.
Kila unachokifanya natamani niwepo, nikitumainia kila
ndoto yako itimie kila muda na sehemu, niwepo nikikutakia
mafanikio mema kwasababu nakujali.
mapenzi si pombe lkn yanalewesha, wala si kidonda lakini
yanatonesha,wala si maradhi lakini yanaumiza, wala si
njaa lakini yanakondesha ,mapenzi ni uvumilivu kwa
unaempenda
Najua kuna vishawishi vingi sana uko ulipo, lakini nikiwa
moyoni mwako, siku hii itakuwa nzuri zaidi kwetu,
tupendane daima lahazizi…
Si vibaya mimi kukusifia kwani wewe ni wangu, nivingi umejaaliwa, vinavyouvutia moyo wangu, ama hakika uzuri wako umedhibiti matamanio yangu “SINTOMPENDA MWINGINE ZAIDI YAKO”
Penzi, maisha yangu yote nimesoma juu ya neno hili,
nimeota juu yake, nimelilia, nimelihitaji. Sasa pamoja
nawe nimelipata.
Kama ningeweza kubadili herufi, ningeweka yangu na yako
kuwa pamoja
Recent Comments