Ujumbe wa mapenzi kwa mpenzi wako kumwambia unampenada na unamkumbuka
kila niamkapo mawazo yangu huwa kwako na upepo uvumapo
huhitaji uwepo wako na hasa nikukumbukapo kumbato
lako,nakupenda mpenzi
kila niamkapo mawazo yangu huwa kwako na upepo uvumapo
huhitaji uwepo wako na hasa nikukumbukapo kumbato
lako,nakupenda mpenzi
Natamani ningekuwa chozi jichoni mwako ambapo ningetelemka
na kuishia midomoni mwako, lakini kamwe sitamani uwe chozi
jichoni mwangu nitakupoteza kila muda niliapo.
Nina huzuni moyoni sijui kwa kuwa siku hizi sikuoni,
naishia kukuota ndotoni,
hivi kweli nipo kwako moyoni? Nakupenda
utamu wa penzi hunogeshwa na pendo la dhati pia utamu wa
penzi ni uwepo wangu na wako,ladha yake ni zaidi ya nazi
kwenye wali au royco kwenye mchuzi au pilipili kwenye
kachumbari, utamu wake ni zaidi ya asali au jam kwenye
mkate ,blueband kwenye uji.penzi tamu halina kifani
upendo ni jibu kwamba kila mmoja anataka… .
upendo ni lugha ,
kwamba kila mmoja anaongea,
upendo hauwez kununuliwa,
na isiyo kadirika na ya bure,upendo kama uchawi safi,ni
siri ya maisha matamu
nakupenda mpenzi
Kila unachokifanya natamani niwepo, nikitumainia kila
ndoto yako itimie kila muda na sehemu, niwepo nikikutakia
mafanikio mema kwasababu nakujali.
maumivu ya kulipoteza penzi lako ni kubwa, lakini ni
makubwa zaidi baada ya kugundua haukuwa yule nileyedhani.
inaniuma sana
Mpenzi kwa mara ya kwanza nilipokuana niliogopa kukuambia,
hata nilipokuambia niliogopa kukupenda, nilipokupenda sasa
naogopa mno kukupoteza. Kusema kweli siko tayari kukukosa
katika maisha yangu.
Katika nyuso za dunia, na kati ya miamba ya jangwani, Kuna SAUTI! Neno la pendo lako liotapo karibu yangu. Ni zaidi ya roho iendayo safarini.
Unaweza kutuma Ujumbe huu kwa Umpendaye hapa
Recent Comments