Ujumbe mzuri wa kimapenzi wa kumwambia mpenzi mapenzi huanza na wewe na yeye
Maneno huanza na ABC. Namba 123. Muziki na do re mi na
mapenzi huanza na mimi na wewe.
Maneno huanza na ABC. Namba 123. Muziki na do re mi na
mapenzi huanza na mimi na wewe.
Kipepeo kipeperushe kunipenda maamuz yako kamwe usijute
nakupenda mpz moyoni mwako unitulize.
Nakupenda mpz
Raha ya ucngz ni ucngz . . . .”tamu”ya penzi ni ndoto .
Na furaha ya ndoto ni yule umpendaye kwa dhati,nitafurahi
nikiwa mimi,
“Mimi sitaki kuwa kila kitu kwa kila mtu, lakini napenda
kuwa kitu kwa mtu.na mtu mwenyewe ni wewe”
nakupenda laazizi
“Kama mimi nilikuwa na maua kila wakati
mawazo yangu
yangekuwa juu yako,nisingefikiri wa kumpa mwingine kabla
yako je wewe ungekuwepo nayo
ungempa nani kwanza? “
Licha ya upole ulionao! Pia upendo wako ndio kishawishi cha kunifanya nikukumbuke siku zote. Jiulize! nina namba za watu wangapi ktk cmu yangu,na bado sijatamani kujua hali zao ila wewe! kwa kuwa, nakuthamini nakukujali, ndiyo maana nakutakia, SIKU NJEMA
Unaweza kutuma Ujumbe huu kwa Umpendaye hapa
Fikra hutawala mtima wangu,
Kwa madhila yalojaa duniani,
Kwa muhali wa yanayojiri,
Kwa machweo na mawio,
Kwa totoro ama nuruni,
Nao moyo hukosa ukamilifu,
Kwa utashi wa zake hisia,
Zinipazo sababu kuu,
Ya upendo juu yako,
Ya kukufanya daima uwe,
Mawazoni mwangu.
Mawazoni ama ndotoni,
Daima wewe hutawala,
Kila asubuhi niamkapo,
Nao usiku nilalapo,
U chakula changu akilini,
Nalo tulizo langu moyoni,
Daima huuwaza upekee,
Wewe uliojaaliwa,
Na hivyo naihisi furaha,
Daima wewe uwapo,
Mawazoni mwangu.
Mpenzi wangu kukutana nawe ilikuwa ni bahati, kukuchagua kuwa rafiki yangu ilikuwa ni maamuzi yangu, lakini kuanguka kwenye penzi lako haikuwa hiyari yangu. Umeniteka moyo na akili yangu pia.
Hakika wewe ndiye wangu mahabuba unayejua kunipa huba,
napenda unavyoniganda mithili ya ruba, nahahidi kukupa
mahaba yanayozidi shaba. Nakupenda.
“CHAI” bila sukari hainyweki.
“ASALI” bila nyuki haitengenezeki.
“PETE” bila kidole haivaliki.
Na “MIMI” bila ya kukusalimia wala siridhiki! ย ย pokea maneno yafuatayo “I LOVE YOU” pokea my lovely kiss “MWAAAAAAA” my best wishes mtumie umpendae
kama na mm nimo nirudishie.
Recent Comments