Meseji ya kumahidi mpenzi wako kumpenda daima
Mapenzi ni upepo,mimi sivumi na kupotea,mapenzi ni mahaba
sili nikamaliza,nikimaliza nitakula nini kesho?nakuahidi
kukupenda leo hata kesho ukiwepo na hata usipokuwepo.
Mapenzi ni upepo,mimi sivumi na kupotea,mapenzi ni mahaba
sili nikamaliza,nikimaliza nitakula nini kesho?nakuahidi
kukupenda leo hata kesho ukiwepo na hata usipokuwepo.
Dhamira kuu ya Moyo wangu ni Mapenzi, kukupenda kwa dhati bila kipingamizi, kuishi nawewe kihalali kwa kudra za wazazi, Nipende nikupende Tudumishe Mapenzi.
Ama baada ya salamu, mimi ni mzima wa afya njema. Mie ni ndege nipo angani na nimetafuta mti wa kutua kila pembe ya dunia lakini sijaupata bado. Je naweza nikatua kwako?
Simu huboa wakati mwingine, kwani ni lazima ufungue meseji
na kuzisoma, kuichaji simu kila mara, lakini usichoke
kwani ndiyo inayotuwezesha tuwasiliane
Nakuomba usiondoke, bali ubaki nami
Kwani wewe ndiye kamilisho la maisha
Yangu kwa sasa na siku za usoni
Ni vigumu kumpata mwenye mapenzi ya kweli na zaidi yule
atakayekuwa tayari kukupenda zaidi, hivyo nafasi
inapopatika si busara kuichezea tudumishe penzi letu
laazizi wangu.
Wewe ni wapekee ninaekupenda, sifikirii kukusaliti na wala
sina wazo la kukutenda, nakuomba
tuendelee kupendana siku zote habbity wangu
Leo ni siku ya furaha kwangu na kwa wakwe zangu,
unajua ni kwa nini? Ni siku waliyokuleta kwenye hii dunia,
happy birthday mpenzi!
Ukweli lazima nikwambiye kwa kuwa sina kimbilio nakupenda kijana mwenzio sijui kwanini hutaki kukisikia changu kilio, namwomba Mungu kila kukicha usikiye changu kilio, nakupenda na kama kukueleza hili nakukosea nisamehe kwani si langu kusudio,luv u mwaah.
Recent Comments