Ujumbe wa mapenzi kwa umpendaye kwa dhati
Nakupenda usiku na mchana Nakuwaza siku zote za maisha yangu
Unaweza kutuma Ujumbe huu kwa Umpendaye hapa
Nakupenda usiku na mchana Nakuwaza siku zote za maisha yangu
Unaweza kutuma Ujumbe huu kwa Umpendaye hapa
Ni ngumu kwa watu wawili kupendana wanapoishi Dunia
tofauti, lakini Dunia hizo zikutanapo na kuwa kitu kimoja,
hiyo ndiyo maana ya kuitwa wewe na mimi.
upendo wa moyoni ndiyo dhati niliyoamini amini kwa haya
nisemayo nakupenda wewe ndiyo kaburi nitakalozikwa nalo
Mpenzi kwa mara ya kwanza nilipokuana niliogopa kukuambia,
hata nilipokuambia niliogopa kukupenda, nilipokupenda sasa
naogopa mno kukupoteza. Kusema kweli siko tayari kukukosa
katika maisha yangu.
Kila unachokifanya natamani niwepo, nikitumainia kila
ndoto yako itimie kila muda na sehemu, niwepo nikikutakia
mafanikio mema kwasababu nakujali.
Nimezunguka pande zote za Tanzania macho
nikiyaangaza
kumsaka mrembo
wakumkabidhi wangu moyo wenye upendo
ndani yake na kulila
TUNDA lake
kwa nafasi huku nikimpa mahaba ya dhati na sikuwahi kuhisi
kama wewe ndiye
ulie uteka moyo wangu.
nakupenda laaziz
»–——»>
Mshale huu unamtafuta mtu muhimu sana ktk
maisha yangu na kama umekutana nao
usiukwepe uache
uchome Moyo wako gharama
za matibabu juu yangu.
Fikra hutawala mtima wangu,
Kwa madhila yalojaa duniani,
Kwa muhali wa yanayojiri,
Kwa machweo na mawio,
Kwa totoro ama nuruni,
Nao moyo hukosa ukamilifu,
Kwa utashi wa zake hisia,
Zinipazo sababu kuu,
Ya upendo juu yako,
Ya kukufanya daima uwe,
Mawazoni mwangu.
Mawazoni ama ndotoni,
Daima wewe hutawala,
Kila asubuhi niamkapo,
Nao usiku nilalapo,
U chakula changu akilini,
Nalo tulizo langu moyoni,
Daima huuwaza upekee,
Wewe uliojaaliwa,
Na hivyo naihisi furaha,
Daima wewe uwapo,
Mawazoni mwangu.
Mpenzi wangu kukutana nawe ilikuwa ni bahati, kukuchagua kuwa rafiki yangu ilikuwa ni maamuzi yangu, lakini kuanguka kwenye penzi lako haikuwa hiyari yangu. Umeniteka moyo na akili yangu pia.
Recent Comments