SMS ya kutuma kwa mpenzi wako asubuhi
Ewe mwanga angaza mboni ya penzi letu
Ndilo sababu ya nguvu yangu
Tangulia pembeni mwa macho yake
Asubuhi hii hadi usiku ujao
Ewe mwanga angaza mboni ya penzi letu
Ndilo sababu ya nguvu yangu
Tangulia pembeni mwa macho yake
Asubuhi hii hadi usiku ujao
Fikra hutawala mtima wangu, Kwa madhila yalojaa duniani, Kwa muhali wa yanayojiri, Kwa machweo na mawio, Kwa totoro ama nuruni, Nao moyo hukosa ukamilifu, Kwa utashi wa zake hisia, Zinipazo sababu kuu, Ya upendo juu yako, Ya kukufanya daima uwe, Mawazoni mwangu. Mawazoni ama ndotoni, Daima wewe hutawala, Kila asubuhi niamkapo, Nao usiku nilalapo, U chakula changu akilini, Nalo tulizo langu moyoni, Daima huuwaza upekee, Wewe uliojaaliwa, Na hivyo naihisi furaha, Daima wewe uwapo, Mawazoni mwangu.
Maji hunitosha nisikiapo kiu, chakula hinitosha nisikiapo njaa, lakini wewe hunifaa kwa kila kitu!
Nitafute wakati una huzuni, nitafute wakati hamna wa
kukusikiliza. Sijali kama mimi ni kimbilio lako la mwisho,
bali sipendi ulie peke yako.
kila niamkapo mawazo yangu huwa kwako na upepo uvumapo
huhitaji uwepo wako na hasa nikukumbukapo kumbato
lako,nakupenda mpenzi
mapenzi ni hisia zilizopo moyoni mwetu,hujidhihirishe pale
unapopata umpendaye,utamu wake ni zaidi ya sukari uchungu
wake ni zaidi ya shubiri je kwako yapo je?
Happy birthday mpenzi, nakuombea kwa mwenyezi
akupe maisha marefu na kukuepusha na maradhi,
pongezi kwa wako wazazi kwa kukuzaa mpenzi,
nakupenda la azizi.
Kila nikuonapo napata weweseko, yako miondoko si ya kitoto
na zaidi wajua kuweka mikogo, umeumbika si kitoto,
nahitaji uwe wangu mama watoto!
Njoo pendo langu nikutembeze
katika milango ya furaha
Nikuwakilishe mbele ya majamaa zangu
Nikuonjeshe asali ya pendo langu
Recent Comments