SMS ya kimahaba ya kumwambia mpenzi wako yeye ndiye yupo kwenye ubongo wako
Bongo zenye fikra kali huwa na mawazo, suluhu na sababu;
ubongo wa kisayansi huwa na kanuni, nadharia na takwimu;
wangu una wewe tu!
Bongo zenye fikra kali huwa na mawazo, suluhu na sababu;
ubongo wa kisayansi huwa na kanuni, nadharia na takwimu;
wangu una wewe tu!
Nakupenda sana mwandani wangu ndiyo maana moyo wangu
hupatwa kidonda ninaokuona na mwingine hasa anapokuwa hana
sifa, nahisi kama anakutumia wewe kama mdori wake wa
kumfurahisha. Uwe makini ua la moyo wangu.
utamu wa penzi hunogeshwa na pendo la dhati pia utamu wa
penzi ni uwepo wangu na wako,ladha yake ni zaidi ya nazi
kwenye wali au royco kwenye mchuzi au pilipili kwenye
kachumbari, utamu wake ni zaidi ya asali au jam kwenye
mkate ,blueband kwenye uji.penzi tamu halina kifani
Wewe ni mng’arao machoni mwangu;
Tabasamu la midomo yangu;
Furaha ya uso wangu;
Kwa sababu bila wewe, mimi sinajipya.
Mpenzi kwa mara ya kwanza nilipokuana niliogopa kukuambia,
hata nilipokuambia niliogopa kukupenda, nilipokupenda sasa
naogopa mno kukupoteza. Kusema kweli siko tayari kukukosa
katika maisha yangu.
Wanafiki tusiwaombee kifo daima na milele washuhudie penzi
letu linavyozidi kukua,na tunavyopambana na mapito.
pongezi kwako mpenzi kuwa wangu mtetezi kwenye jahazi la
mapenzi,ufundi na ujuzi unao hasa tuwapo wawili
chumbani.penzi lako halichakai daima huzaliwa upya.
Kila mtu anataka kuwa jua linalong’arisha maisha yako,
lakini ni afadhali niwe mwezi, ili nikuangazie wakati wa
giza ambapo jua limechwea na haliangazi tena.
Ucku ulalapo jua kuna m2 akupendaye,mchana uwajibikapo
tambua yupo anayekuwaza ,jioni uwapo mazoezini jua yupo
anayekuonea wivu,hata uwapo kwenye kumbi za burudani
tambua mwenzio nakulilia,usitoe penzi kangu akilini hata
km upo mbali nami!moyoni mwangu hutafutika milele!
Recent Comments