Ujumbe mzuri wa kimapenzi wa kumwambia mpenzi mapenzi huanza na wewe na yeye
Maneno huanza na ABC. Namba 123. Muziki na do re mi na
mapenzi huanza na mimi na wewe.
Maneno huanza na ABC. Namba 123. Muziki na do re mi na
mapenzi huanza na mimi na wewe.
Hakika nimepata tabibu, maradhi yangu wajua kujyatibu,
napenda jinsi unavyonitibu, huna papara yaani ni taratibu,
mpenzi usijemuonyesha mwingine hizo zako zabibu, maswahibu
yakatayonisibu hakuna atakayeweza kuyatibu, nakupenda
Si vibaya mimi kukusifia kwani wewe ni wangu, nivingi
umejaaliwa, vinavyouvutia moyo wangu, ama
hakika uzuri wako umedhibiti matamanio yangu “SINTOMPENDA
MWINGINE ZAIDI YAKO”
Kuna miezi 12 katika mwaka…siku 30 katika mwezi…siku 7
katika wiki, masaa 24 katika siku…dakika 60 katika saa……
lakini wewe ni mmoja tu maishani mwangu.
Mwanamke ni yule amfanyaye mwanamme auhisi uanaume wake,
wewe ni mwanamke mwenye sifa hizo.
Moyo wangu unajua kupenda katu haujui kutenda
mpz, nakupenda tukwepe fitina mpz.
Tone la mvua huonekana dogo sana, lakini kwa mwenye kiu hulisubiri kwa hamu kubwa. Sms ni kitu kidogo, lakini huonyesha mahali fulani yupo mtu ANAYEKUPENDA, ANAKUKUMBUKA, ANAKUOMBEA,
ANAKUJALI na,
ANAKUTAKIA mafanikio mema
nakupenda sana mpenzi wangu ,we ndo wa pekee mwenye kujua
furaha ya moyo wangu nikiwa na majonzi huwa upo karibu
nami,nikiwa na furaha huja kushea nami,ahsante wangu
tabibu ,we ndo wangu wa manani.
Moyo wangu umehifadhi hisia zako, nakuahidi kamwe sintopunguza upendo kwako, tunza sms hii ya ahadi kwenye simu yako, iwe kumbukumbu kila uisomapo! “NAKUPENDA MALAIKA WANGU”
Recent Comments