Ujumbe wa kumtumia mpenzi wako wakati anahuzuni kumwambia kuwa uko kwa ajili yake
Nitafute wakati una huzuni, nitafute wakati hamna wa
kukusikiliza. Sijali kama mimi ni kimbilio lako la mwisho,
bali sipendi ulie peke yako.
Nitafute wakati una huzuni, nitafute wakati hamna wa
kukusikiliza. Sijali kama mimi ni kimbilio lako la mwisho,
bali sipendi ulie peke yako.
Salamu yako ni nusu ya uhai wangu, kuikosa nisawa na kuidhulumu nafsi yangu, kuipata nisawa na ua ridi machoni mwangu, nakila ninapoipata huwa najisikia faraja moyoni mwangu, Nakupenda sana Muhibu wangu.
Usimpende mtu tuu kwa sababu uko mpweke
Au kwa sababu ana pesa, kwa sababu upendo
Sio pesa wala siluhisho la matakwa yako.
Uamkapo nitakupa langu tabasamu
Ukweli wa moyo utawale roho yako
Kwani macho yako ndo uzuri kwangu
Nakupenda sasa na milele kipenzi changu
Unaweza kutuma Ujumbe huu kwa Umpendaye hapa
yakumbuke haya sana katika maisha yako wahurumie wenye
kukupenda hasa mwenye pendo la dhati kama langu,wapende
wanaokupenda japo kwa chembe ya upendo,thamini pendo la
akupendae kwa kila mara japo sekunde moja.
Naomba niwe CHOZI ndani ya JICHO lako,
Nikitoka tu NIDONDOKE kwenye SHAVU lako,
Ukinipangusa NIGANDE kwenye KIGANJA chako,
Kwa sababu NAKUPENDA sana
Niseme nini ujue nakupenda? Nifanye nini ujue nakupenda?
Nikuite jina gani ujue ni wewe peke yako upo moyoni
mwangu? Hakika hakuna ila moyo wangu ndio unaosema kuwa
nakupenda, niamini mpenzi
Moyo wangu kwako hautavunjika kamwe. Tabasamu langu kwako halitafutika kamwe. Penzi langu kwako halitaisha kamwe. Nakupenda!
Tambua kuwa nakujali
Furahia kwamba nitakuwa na wewe
Katika siku zote za maisha yangu
Nitakupenda bila kikomo milele
Unaweza kutuma Ujumbe huu kwa Umpendaye hapa
Recent Comments