Meseji Nzuri Kali Za Mapenzi

Ujumbe wa kuasa kuhusu upendo

UPENDO ni ubeti wa maneno yaliyo tamkwa mpaka sasa hajulikan nani alietunga!
PENZI ni hadithi iliyocmuliwa lakin mpaka sasa hafahamik nan muhucka, ndio maana kila mwenye KUPENDA au KUPENDWA hana uhakika muda wote huhis anasalitiwa.
PENZI Ni kama jengo lilokosa nguzo muda wowote unahic litadondokaโ€ฆ Ucnielewe vibaya ckukatazi KUPENDA au KUPENDWA, ila tazama wap UMEPENDA au UMEPENDWA!je eti nikweli kumpenda asie kupenda ni sawa na kusubiri boti airport

Ujumbe mzuri wa kumwambia mpenzi wako kuwa yeye tuu mdiye kakutawala

Fikra hutawala mtima wangu,
Kwa madhila yalojaa duniani,
Kwa muhali wa yanayojiri,
Kwa machweo na mawio,
Kwa totoro ama nuruni,
Nao moyo hukosa ukamilifu,
Kwa utashi wa zake hisia,
Zinipazo sababu kuu,
Ya upendo juu yako,
Ya kukufanya daima uwe,
Mawazoni mwangu.

Mawazoni ama ndotoni,
Daima wewe hutawala,
Kila asubuhi niamkapo,
Nao usiku nilalapo,
U chakula changu akilini,
Nalo tulizo langu moyoni,
Daima huuwaza upekee,
Wewe uliojaaliwa,
Na hivyo naihisi furaha,
Daima wewe uwapo,
Mawazoni mwangu.

SMS ya kumwambia mpenzi wako kuwa bado unampenda na hujabadilika

“Japokuwa”
“Kuku” “Haogi” “Yai” “Lake” “Litabaki” “Kuwa” “Jeupe” “Tu” “Namaanisha”
“Kuwa”
“Hata” “Kama” “Ukiona”
“Nipo” “”KIMYA”” Muda”
“Mrefu” “”UPENDO”” “Wangu” “Kwako”
“””Bado”””
“Uko” Pale pale!!!!!
Usijali
“Tupo Pamoja” “Kwa” “Asilimia 100%”.

Unaweza kutuma Ujumbe huu kwa Umpendaye hapa

SMS nzuri sana ya kutakia usiku mwema

Dah! Safari yetu ilikuwa ngumu kweli ila hatimaye tumefika japo ni usiku sana hebu tupige hodi tusije kabwa na vibaka hapa nje. Hodiiiiii, Hodiiiii, Tunaomba tufungulie Mlango,, sisi tunaitwa FURAHA, AMANI na UPENDO. Tumebeba HEKIMA, BUSARA na MAFANIKIO. Tulikuwa wengi HURUMA na UPOLE wanakuja nyuma. CHUKI na WIVU hawana nauli. TABU ni mahututi. SHIDA yuko jela. MATATIZO amepigwa shoti ya umeme. MIKOSI amefariki njiani. LAANA ameliwa na mamba. UVIVU ameungua na maji ya moto hajiwezi. Tutakuwa nawe daima maana tumefika kwa NEEMA . Mungu akulinde na mabaya yote katika dunia hii. ucku mwema.

Unaweza kutuma Ujumbe huu kwa Umpendaye hapa

Shopping Cart
๐Ÿ  Home ๐Ÿ“– Reading ๐Ÿ–ผ๏ธ Gallery ๐Ÿ’ฌ AI Chat ๐Ÿ“˜ About