Ujumbe wa mahaba wa kumtumia umpendaye kumwambia anahisia gani kuhusu mapenzi
mapenzi ni hisia zilizopo moyoni mwetu,hujidhihirishe pale
unapopata umpendaye,utamu wake ni zaidi ya sukari uchungu
wake ni zaidi ya shubiri je kwako yapo je?
mapenzi ni hisia zilizopo moyoni mwetu,hujidhihirishe pale
unapopata umpendaye,utamu wake ni zaidi ya sukari uchungu
wake ni zaidi ya shubiri je kwako yapo je?
Mungu akupe umri wa mnazi uishi mingi miaka.
Akupe thamani ya mnazi kila kitu chatumika.
Kuanzia kuti lake mpaka kwenye kidaka.
Kitale katikati yake ukila utaridhika.
Matamu na maji yake hukata kiu haraka.
Weupe watui lake lina ladha ukipika.
Kupaka mafuta yake mwili hulainika.
Na kwenye machicha yake kazi nying hufanyika.
Hata na upepo wake uvumapo utacheka.
Sikijui kitu chake kipi kisichotumika.usiku mwema
Nakuomba usiondoke, bali ubaki nami
Kwani wewe ndiye kamilisho la maisha
Yangu kwa sasa na siku za usoni
Ni vigumu kumpata mwenye mapenzi ya kweli na zaidi yule
atakayekuwa tayari kukupenda zaidi, hivyo nafasi
inapopatika si busara kuichezea tudumishe penzi letu
laazizi wangu.
kila niamkapo mawazo yangu huwa kwako na upepo uvumapo
huhitaji uwepo wako na hasa nikukumbukapo kumbato
lako,nakupenda mpenzi
sura yako haifutiki usoni mwangu kirahic,ingawa upo mbal
nami lkn penzi lako bado nalikumbuka,hakuna anayeweza
kukata kiu yangu zaidi yako,nakupenda mpenzi wangu!
Nakutakia kila la kheri katika maisha yako ya ndoa,wengi
watakuambia maneno kila kukicha,lakini nakuambia wapo
ambao kwa hakika watakaokuwa wamelenga kutia doa ndoa yako
,rafiki yangu kipenzi kwani wengi waitamani ndoa lakini
hawajapata wa kuwaowa
Happy birthday mpenzi, nakuombea kwa mwenyezi
akupe maisha marefu na kukuepusha na maradhi,
pongezi kwa wako wazazi kwa kukuzaa mpenzi,
nakupenda la azizi.
Nilikuwa nikifiria kwamba ndoto haziwezi kuwa kweli,
lakini nilibadili mawazo yangu pale tu nilipokuona wewe.
Recent Comments