Meseji ya kumkaribisha mpenzi wako
Njoo pendo langu nikutembeze
katika milango ya furaha
Nikuwakilishe mbele ya majamaa zangu
Nikuonjeshe asali ya pendo langu
Njoo pendo langu nikutembeze
katika milango ya furaha
Nikuwakilishe mbele ya majamaa zangu
Nikuonjeshe asali ya pendo langu
Kila nikuonapo napata weweseko, yako miondoko si ya kitoto
na zaidi wajua kuweka mikogo, umeumbika si kitoto,
nahitaji uwe wangu mama watoto!
kamwe cwez kuacha kukupenda,utaendelea kujificha moyo
mwangu cku zote za maisha yang,maana wewe ndiye mhimili wa
maisha yangu,tafadhal naomba unipende milele!
Furaha yangu kubwa ni kuliona tabasamu lako, kujua uko na
furaha, na kuhisi upendo wako. Najua kuwa maisha mara
nyingine huwa ni makatili, na hiyo ni sababu niko hapa
kukuonyesha kuwa maisha yanaweza kuwa mazuri kama kuna mtu
anayekujali.
Uchungu wa kifo hauna tofauti na maumivu nitakayoyapata ukiniachana, mpenzi usiniache nami siko tayari kukuacha.
Siku zote kwangu ni sherehe ni wewe unishereheshaye,ukweli
usio na kejeli mapenzi yako yanatii kiu yangu,moyoni
mwangu nimeridhiaโฆ .nakupenda daima mpenzi!
Dah! Safari yetu ilikuwa ngumu kweli ila hatimaye tumefika japo ni usiku sana hebu tupige hodi tusije kabwa na vibaka hapa nje. Hodiiiiii, Hodiiiii, Tunaomba tufungulie Mlango,, sisi tunaitwa FURAHA, AMANI na UPENDO. Tumebeba HEKIMA, BUSARA na MAFANIKIO. Tulikuwa wengi HURUMA na UPOLE wanakuja nyuma. CHUKI na WIVU hawana nauli. TABU ni mahututi. SHIDA yuko jela. MATATIZO amepigwa shoti ya umeme. MIKOSI amefariki njiani. LAANA ameliwa na mamba. UVIVU ameungua na maji ya moto hajiwezi. Tutakuwa nawe daima maana tumefika kwa NEEMA . Mungu akulinde na mabaya yote katika dunia hii. ucku mwema.
Unaweza kutuma Ujumbe huu kwa Umpendaye hapa
Raha ya ndege kichaka si tunduni asilani,
Raha ya Ndege ujumbe nakupa mpelekee
mwandani iwapo hukumkuta msubiri mlangoni,
Usije ukaondoka hakuchinji asilani,
Mwambie namkumbuka hatoki mwangu moyoni.
ucku mwema
Mapenzi ni kitu kisichotabirika, ndio maana kila mwenye KUPENDA au KUPENDWA hana uhakika na PENZI lake kwa yule AMPENDAE, Muda wote huhisi anasalitiwa. PENZI Ni kama JENGO lililokosa NGUZO muda wowote unahisi litadondokaโฆ Usinielewe vibaya sikukatazi KUPENDA au KUPENDWA, ila tazama wapi UMEPENDA au UMEPENDWA.kilalakher kwa umpendae
Recent Comments